Nafikiri wewe hujaelewa kwa nini watu wanadai muungano wa mkataba,ukiangalia kijografia tanganyika ndio inayo muhitaji zanzibar ukiangalia moja ni bahari kuu ya zanzibar. Hiyo ni moja tu ya mambo ambayo ita wacost . Sisi upande wetu tunataka uhuru hasa hata muungano hatuutaki kwa vile black coloni limetuganda ndio tunapapatua at least tupumulie hapo wa mkataba. But if there's possible to be independent defenetly we gonna be happy 4reva
acha nidhamu ya uoga.Taratibu jamani muungano usije ukatutoa roho, Mhe. lissu taratibu mtani roho za watanzania na damu zao zitakulilia.
we need our country back!
Watanganyika tuwe na misimamo mingine ambayo ni ya kizalendo kama hoja hii ya Tundu Lissu Bungeni.
Nmeipenda hoja ya Tanganyika.
Kama Wazanzibari wameweza kujitoa katika muungano na wakawa na sera moja juu ya muungano(iwe CCM au CUF).
Gazeti la Nipashe leo 5 Julai 2012, (uk. wa 4)lina kichwa cha habari:
"Lissu ataka Serikali ya Tanganyika irudi
Na Muhibu Said, Dodoma
Kambi ya upinzani Bungeni imesema muungano wa Tanganyika na Zanzibar unakabiliwa na hatari kubwa ya kuvunjika kutokana na kitendo cha Zanzibar kujitangazia uhuru, na kwa hiyo ni wakati mwafaka sasa wa kuanzishwa tena kwa Seikali ya Tanganyika."
Mh Lissu ametoa argument yenye mantiki ya kutosha Bungeni kutetea hoja hii.
Kama walivyokubaliana kule Zanzibar(CCM na CUF) , kambi ya CCM Bungeni tunawaomba waone mantiki ya hoja ya Mh Lisuu katika hili suala la Muungano na hatma yake.
Tanganyika inabidi irudishwe kutokana na yaliyotokea Zanzibar , na kuelekea kukubalika na viongozi wote.
Wabunge wa CCM tafadhali walione hili bila woga.
Nawasilisha
Mkuu naona hujaielewa hoja yangu.masopakyindi: Hao kina Tundu Lissu waache kutumia hoja ya utanganyika kwa ajili ya maslahi yao kisiasa! Hivi nani anaweza kutuelezea hapa umuhimu wa hoja hii kwa mwananchi wa kawaida? acheni kuchezea kodi zetu na kutuingiza kwenye matumizi yasiyo na mashiko kwa watanzania kwa sababu uchu wenu wa madaraka bana!
Mkuu naona hujaielewa hoja yangu.
Ni kwamba , hata kama tuanupenda muungano, swala hili limesha pitwa na wakati kwa sababu upande wa pili tunaoungana nao wameshaukana kwa maana ya kubadili kabisa vifungu vya serikali ya Zanzibar, ambavyo vinauweka muungano pemneni.
Nilivyo muelewa Tundu Lissu ni kwamba kama hkuna aliyediriki kuhoji mabadiliko hayo ya katiba ya Zanzibar, siye Tanganyika tunasubiri nini?
Ni heri Tanganyika yetu ikarudi tena.
Hiyo ndiyo argument nzima.
Kwa mfano rahisi unaoweza kuelwa ni kama umeoa bibi mzuri, hakutaki na karudi kwao kapokelewa kwa maandishi, sasa kujifaraguza kwa baba mkwe unasubiri nini? si kipigo na matusi ya wakwe tu?
Kama ni matusi , kuchomewa nyumba , makanisa hata kuwekewa vidole machoni, hilo waTanganyika tumeshafanyiwa, twasubiri nini!
GHIBUU,
..tuelimishe basi kuhusu suala la bahari kuu ya Zanzibar na faida tutakazopata wa-Tanganyika kwa kuwa na "muungano wa mkataba." kumbuka kwamba tumejumuika hapa kwa lengo la kufahamishana.
..mimi kwa upande wangu, nikizingatia hali ya kila upande kutokuridhika na muungano huu, na zaidi kuutuhumu upande wa pili, nadhani moving forward ni vizuri tukawashirikisha na wenzetu[eac au sadc] ktk mkataba wowote ule unaohusu Tanganyika na Zanzibar.
..tuchukulie hilo suala la bahari kuu. Kwa uelewa wangu Zanzibar inapaka na Kenya kwa upande wa baharini. Sasa kama kuna mkataba wowote ule kuhusiana na masuala ya bahari kuu basi ni bora ukahusisha Kenya,Tanganyika,Zanzibar, na hata nchi nyingine, ili kuepuka hali ya kutokuaminiana ambayo imekuwepo muda wote wa muungano wetu.
..pia kuna extreme theories kwamba the 10 miles coastal strip ya Tanganyika and east africa ni eneo la Zanzibar. bado hata ktk mazingira hayo naamini nchi[Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi,..] zote ambazo zitakuwa landlocked zitalazimika kuwa na mkataba wa Zanzibar. sioni ulazima wa kuwa na "muungano wa mkataba" mahsusi kwa ajili ya Tanganyika na Zanzibar.
..LET ZANZIBAR GO!!!!
Wewe ni mtu wa Oman, hata muungano ukivunjika utahusika vipi?Nafikiri kama mtaacha unafiki na kuwa wawazi na wakweli kama Tundu Lissu basi mumekwisha. Waliounda Muungano hawapo sasa mnaogopa ninhi?
mnatakiwa muwe na uthubutu na udhati kama walivyo Znz katika kutetea maslahi ya nchi yenu sio kulalama