Hongera Tundu Lissu: Hoja ya kurudisha Tanganyika!

Tukiweka ushambenga na ushabiki kando Lissu ana hoja nzito sana kuhusu mustakabali wa taifa na muungano wetu! hizo ndio hoja ambazo mwanasheria mkuu AG Alitakiwa kuzi adress na ku clarify wakati anachangia sio kumrukia prof. Shivji na kuanza kumkashifu lissu! Kuna mgongano mkubwa sana wa kisheria kati ya katiba ya zanzibar ya sasa na katiba ya JMT! Haya mambo yakiendelea kufumbiwa macho yafumuka yenyewe na madhara yake ni makubwa sana kuliko ambavo yangejadiliwa sasa!!
 
Bila kujali itikadi zetu za kisiasa, Watanganyika tupiganie haki ya kuwa na nchi yetu tena kama wanavyofanya Wazanzibari mara zote.
Hongera Lissu kwa kupasua jipu.
TANGANYIKA INAKUJA.
 
yah..imefika wakati watanganyika tuseme ukweli,,kwa muda mferu tumekuwa kimya kama silaha ya kuulinda muungano..udhaifu huu umewajenga upande wa pili kujiona kana kwamba sisi tunanufaika na huu muungano..wamekuwa wakisema maneno makali hata tukiwa makazi..tumeonyesha moyo wa unyonge kuepusha marumbani..but now is a time....tunaitaka tanganyika..tumechoka na huu mzigo..tunawabeba kwa kila kitu..hivi tunachowang'ang'ania nini hawa....tumewachoka...lets them gooooo
 
hivi ZITTO yupo mjengoni(bungeni) kweli? bado sijaupata moto wake wa siku zote,zitto tupe raha bhana!
 
Nampa hongera sana lissu,ila katika uchambuzi wake inaonekana amekerwa na mabadiliko ya 10 ya katiba ya zanzibar kuitangazia uhuru.
Wakati huo huo unachambu katiba ya muungano na kukubali kuwa kuna makose yametendeka moja ni kuongeza mambo ya muungano kinyume na sheria.
Unafahamu kuwa muungano umeundwa na nchi mbili ambazo zilikuwa huru ? Sasa wewe umekerwa nini zanzibar kujitangazia uhuru wake ? Ile sio arusha wala mtwara.
Hoja ya lissu sio ya kudai tanganyika bali ilikuwa hoja ya kulalamika tu kwa sababu wazanzibari wamejinyakulia madaraka yao kwenye muungano !
Ikiwa kweli chadema na watanganyika wote munaipenda nchi yenu kwa nini mumeshindwa kuonyesha hisia zenu kama uwamsho walivyo waamsha wazanzibari kudai kura ya maoni huku wakidai uhuru wa zanzibar na mamlaka yake yote ambayo yamo kwenye muungano ?
Nikiangalia chadema ni sawa G55 ambayo iliyokuwa ikiongozwa na kikwete mmoja,g55 walidai tanganyika ,nyerere akawaita na kuwaweka kitako,aliwaambia kuwa tanganyika ni hii tanzania tunataka kuimeza zanzibar,na nakumbuka ile nguvu ya chadema ya hapo awali haipo tena,kikwete ameshawaeka kitako,mumekaa kimya,kama kweli wanaume na munaipenda tanyanyika ! Pelekeni mswada maalum wa kuirudisha tanganyika,hoja binafsi hiyo .
Pelekeni bungenii ! Musiwe wanafiki.
 
Hata Mh.Nahodha aliunga mkono na kusema ni kweli tupu, ila si vizuri kuusema. Kwakweli hapo alinichanganya kidogo.
Wazanzibari wana mkakati ambao inaelekea viongozi wetu aidha wana dharau-at our peril- au wanaogopa.
Sioni kwa nini WazaNzibari wanatekeleza matakwa yao tena kwa mbwembwe zote hadharani na bila kificho ili kuibuat utaifa wa Zanzibar na sisi huku Tanganyika tuna dily daly.
Viongozi wote wa Zanzibar wana msimamo mmoja, Zanzibar first, Muungano ni wa kuibeba Zanzibar at the expense of Tanganyika.
Ni jambo la kusikitisha kuwa si wengi kati ya viongozi wetu toka Tanganyika wanao tambua hilo.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nampa hongera sana lissu,ila katika uchambuzi wake inaonekana amekerwa na mabadiliko ya 10 ya katiba ya zanzibar kuitangazia uhuru.
Wakati huo huo unachambu katiba ya muungano na kukubali kuwa kuna makose yametendeka moja ni kuongeza mambo ya muungano kinyume na sheria.
Unafahamu kuwa muungano umeundwa na nchi mbili ambazo zilikuwa huru ? Sasa wewe umekerwa nini zanzibar kujitangazia uhuru wake ? Ile sio arusha wala mtwara.
Hoja ya lissu sio ya kudai tanganyika bali ilikuwa hoja ya kulalamika tu kwa sababu wazanzibari wamejinyakulia madaraka yao kwenye muungano !
Ikiwa kweli chadema na watanganyika wote munaipenda nchi yenu kwa nini mumeshindwa kuonyesha hisia zenu kama uwamsho walivyo waamsha wazanzibari kudai kura ya maoni huku wakidai uhuru wa zanzibar na mamlaka yake yote ambayo yamo kwenye muungano ?
Nikiangalia chadema ni sawa G55 ambayo iliyokuwa ikiongozwa na kikwete mmoja,g55 walidai tanganyika ,nyerere akawaita na kuwaweka kitako,aliwaambia kuwa tanganyika ni hii tanzania tunataka kuimeza zanzibar,na nakumbuka ile nguvu ya chadema ya hapo awali haipo tena,kikwete ameshawaeka kitako,mumekaa kimya,kama kweli wanaume na munaipenda tanyanyika ! Pelekeni mswada maalum wa kuirudisha tanganyika,hoja binafsi hiyo .
Pelekeni bungenii ! Musiwe wanafiki.

GHIBUU,

..hoja ya Tundu Lissu iko very clear. Kama wa-Zanzibari wamepewa haki ya kuwa na serikali yao, pamoja na bunge lao, basi wa-Tanganyika na sisi tunastahili haki hiyohiyo.

..hakuna mahali ambapo Tundu Lissu amedai kwamba serikali ya Zanzibar ifutwe. Msome vizuri ktk conclusion aliyotoa ambapo ametamka wazi kwamba TANGANYIKA inapaswa kurejeshwa.

..Tundu Lissu anapigania USAWA ktk MUUNGANO, badala ya dhuluma na udhalilishaji unaoendelea dhidi ya wa-Tanganyika.

..Badala ya kuwabeza na kuwakatisha tamaa, wa-Zanzibari mnapaswa kuziunga mkono juhudi za wa-Tanganyika kama Tundu Lissu na wengine wenye msimamo kama wake.

..LET ZANZIBAR GO!!!

NB:

..G-55 came before their time. The same way kama ilivyokuwa kwa Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi ambaye aliu-challenge muungano na watu kama Seif Sharrif Hamad wakampinga. Msimamo wa Maalim Seif kuhusu muungano umebadilika sana toka mwaka 84 mpaka leo hii.

..Actually sasa hivi Maalim Seif "amelainika" kiasi kwamba badala ya kurejeshwa kwa Zanzibar "huru" kama ili ya mwaka 1963 na kabla ya hapo. Maalim Seif anapendekeza kuwepo kwa "muungano wa kimkataba." Swali la kujiuliza ni kwamba, Nyerere na Karume walisaini kitu gani kama siyo mkataba wa muungano??
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nampa hongera sana lissu,ila katika uchambuzi wake inaonekana amekerwa na mabadiliko ya 10 ya katiba ya zanzibar kuitangazia uhuru.
Wakati huo huo unachambu katiba ya muungano na kukubali kuwa kuna makose yametendeka moja ni kuongeza mambo ya muungano kinyume na sheria.
Unafahamu kuwa muungano umeundwa na nchi mbili ambazo zilikuwa huru ? Sasa wewe umekerwa nini zanzibar kujitangazia uhuru wake ? Ile sio arusha wala mtwara.
Hoja ya lissu sio ya kudai tanganyika bali ilikuwa hoja ya kulalamika tu kwa sababu wazanzibari wamejinyakulia madaraka yao kwenye muungano !
Ikiwa kweli chadema na watanganyika wote munaipenda nchi yenu kwa nini mumeshindwa kuonyesha hisia zenu kama uwamsho walivyo waamsha wazanzibari kudai kura ya maoni huku wakidai uhuru wa zanzibar na mamlaka yake yote ambayo yamo kwenye muungano ?
Nikiangalia chadema ni sawa G55 ambayo iliyokuwa ikiongozwa na kikwete mmoja,g55 walidai tanganyika ,nyerere akawaita na kuwaweka kitako,aliwaambia kuwa tanganyika ni hii tanzania tunataka kuimeza zanzibar,na nakumbuka ile nguvu ya chadema ya hapo awali haipo tena,kikwete ameshawaeka kitako,mumekaa kimya,kama kweli wanaume na munaipenda tanyanyika ! Pelekeni mswada maalum wa kuirudisha tanganyika,hoja binafsi hiyo .
Pelekeni bungenii ! Musiwe wanafiki.

Nadhani umeipitia hoja ya Lissu kwa haraka haraka. Lissu 'hajakerwa' na Zanzibar kujitakia uhuru wake, infact kama umeangalia vizuri ameonesha jinsi mambo yamekuwa yanaongezwa kinyemela beyond yale 11.

Nakubaliana na wewe kwamba muungano ni wa nchi mbili huru, na sasa moja imeshajitangazia uhuru wake. Sasa, Tanganyika nao wanataka haki yao na kuhusu namna ya kudai serikali ya Tanganyika, si lazima kufanya copy & paste style ya UAMSHO.

Najua so far watoa maoni wengi Zanzibar wanataka serikali mbili lakini kuwe na muungano wa mkataba! But I say, LET ZANZIBAR GO. Mkataba tukafanyie kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki au SADC OR NEVER.

Kwenye red: sijakuelewa. nguvu ipi, kwenye nini? na umepima vipi?
 
JokaKuu
wazanzibari hata wasiposaidiwa na chadema au chama chochote kila basi kama ni lengo ukombozi basi utatimia inshallah ,hivi hivyo unavyo zani wewe hiyo hoja alie ipeleka tundu lissu wazanzibari hawaijui ? Kwa taarifa yako wazanzibari wauelewa zaidi huu muungano kuliko hata watanganyika,na ndio ukaona tunadai haki zetu za msingi ambozo tumepokonywa kikatiba ya muungano.
Kwa kumalizia lisu hakupeleka hoja kuwasaidia wazanzibari bali kapeleka hoja kuwa zanzibar imejitangazia uhuru tu,na kama si hivyo basi neno tanganyika hivi sasa lisingelikuwa midomoni mwenu,sisi tunavyofahamu tanganyika ni hii tanzania,imeinyang'anya zanzibar mamlaka yake kwa kuvaa ya koti la muungano.

Namalizia kusema acheni kuilalamikia zanzibar kama tanganyika munaipenda na munataka tuendee ya muungano ambao utakao kuwa wa haki kwa pande zote mbili. Peleka hoja binafsi bungeni kurudishwa kwa tanganyika,jamuhuri ya tanganyika ! Lissu upo ?
 
Last edited by a moderator:

GHIBUU, kama unavyosema kwa sasa Zanzibar "imerudisha haki zetu za msingi ambozo iliipokonywa kikatiba na muungano"
Naomba unisaidie, kwanini huu uhuru mlijitangazia usiwe 100% kwamba hakuna cha mkataba waka baba yake na mkataba? Kwanini bado kama kuna kunin'ginia kwenye mti huu wa muungano
 
Namuomba Mungu azidi kunipa pumzi ili niwe mmojawapo wa watakao sherehekea kurudi kwa Tanganyika yetu,hawa masharobaro tuwaachie Makunduchi yao
 
JokaKuu
wazanzibari hata wasiposaidiwa na chadema au chama chochote kila basi kama ni lengo ukombozi basi utatimia inshallah ,hivi hivyo unavyo zani wewe hiyo hoja alie ipeleka tundu lissu wazanzibari hawaijui ? Kwa taarifa yako wazanzibari wauelewa zaidi huu muungano kuliko hata watanganyika,na ndio ukaona tunadai haki zetu za msingi ambozo tumepokonywa kikatiba ya muungano.
Kwa kumalizia lisu hakupeleka hoja kuwasaidia wazanzibari bali kapeleka hoja kuwa zanzibar imejitangazia uhuru tu,na kama si hivyo basi neno tanganyika hivi sasa lisingelikuwa midomoni mwenu,sisi tunavyofahamu tanganyika ni hii tanzania,imeinyang'anya zanzibar mamlaka yake kwa kuvaa ya koti la muungano.

Namalizia kusema acheni kuilalamikia zanzibar kama tanganyika munaipenda na munataka tuendee ya muungano ambao utakao kuwa wa haki kwa pande zote mbili. Peleka hoja binafsi bungeni kurudishwa kwa tanganyika,jamuhuri ya tanganyika ! Lissu upo ?

GHIBUU,

..nakubaliana na wewe by 90%.

..nisichokubaliana na wewe ni pale unapodhani kwamba Tundu Lissu anapinga jitihada za Zanzibar kujitambulisha kama taifa huru.

..anachodai Tundu Lissu ni kuundwa kwa serikali ya Tanganyika, na ikiwa muungano utadumu basi serikali hiyo itakuwa ni mbia sawa na serikali ya Zanzibar ktk masuala ya muungano.

..hakuna ulazima wa kupeleka bungeni hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika wakati tayari kuna tume inazunguka nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi kuhusu suala la katiba mpya.

..Ghibuu, hakuna haja ya kugombea fito wakati nyumba tunayojenga ni moja. wewe unaitaka Zanzibar yako, na sisi tunaitaka Tanganyika yetu.

..sana sana tunachowaomba wa-Zanzibari ni kwamba muachane na jitihada za kuleta muungano wa "mkataba", na badala yake Tanganyika na Zanzibar tushirikiane kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki.

..LET ZANZIBAR GO!!
 
Nafikiri wewe hujaelewa kwa nini watu wanadai muungano wa mkataba,ukiangalia kijografia tanganyika ndio inayo muhitaji zanzibar ukiangalia moja ni bahari kuu ya zanzibar. Hiyo ni moja tu ya mambo ambayo ita wacost . Sisi upande wetu tunataka uhuru hasa hata muungano hatuutaki kwa vile black coloni limetuganda ndio tunapapatua at least tupumulie hapo wa mkataba. But if there's possible to be independent defenetly we gonna be happy 4reva
 
Nampongeza sana Lissu hakika huyu ndio mtu pekee miongoni mwa waTanganyika mwenye uthubutu wa kuzungumza ukweli na bayana tena mchana kweupeeeeeeee bila kuogopa. HAKUNA MTANGANYIKA HATA MMOJA MWENYE UTHUBUTU WA KUZUNGUMZIA TANGANYIKA HADHARAni kama pale Bungeni.

Hongere sana Mwana Ilboru.
 
Tukiweka ushambenga na ushabiki kando Lissu ana hoja nzito sana kuhusu mustakabali wa taifa na muungano wetu! hizo ndio hoja ambazo mwanasheria mkuu AG Alitakiwa kuzi adress na ku clarify wakati anachangia sio kumrukia prof. Shivji na kuanza kumkashifu lissu! Kuna mgongano mkubwa sana wa kisheria kati ya katiba ya zanzibar ya sasa na katiba ya JMT! Haya mambo yakiendelea kufumbiwa macho yafumuka yenyewe na madhara yake ni makubwa sana kuliko ambavo yangejadiliwa sasa!!

Ujasiri wa Lissu ni kuwa yupo katika kufuata katiba yenu ya Muungano na siku zote anasimamia hapa
sharia hiyo ya Muungano inayobainisha Mamlaka ya JMTz No 15 Ibara ya 9 ya mwaka 1984. Kifungu cha 34. inayonena hivi

34.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano

katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengine yote

yahusuyo Tanzania Bara.

(2) Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatahusu

utekelezaji na hifadhi ya Katiba hii na pia mambo mengineyo yote

ambayo Bunge lina mamlaka ya kuyatungia sheria.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya

mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia

juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara,

yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii,

madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa

ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu

madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika

utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Back
Top Bottom