Naipongeza sana Taasisi hii ya The Islamic Foundation kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya hapa nchini kwetu Tanzania.
Pia naupongeza sana uongozi wa Manispaa ya Morogoro chini ya Meya wake Mhe Nondo na Mkurugenzi Bw Jorvis kwa kutambua mchango wake hadi kuitunuku Taasisi hii Cheti cha shukrani "Certificate of appreciation" katika kuleta maendeleo ya watu bila kuzingatia dini ama itikadi ya mtu.
Katika kipindi kifupi, The Islamic Foundation imefanikiwa kuchimba visima virefu na vifupi vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 300 katika kata mbalimbali za manispaa ya Morogoro. Kata ya Mji mkuu imebahatika kupata visima viwili (2) na pia inajengewa ofisi ya kata ya kisasa kabisa.
Katika kata ya Kilakala kwa mujibu wa diwani wa kata hiyo Bw Ribon Mkali, The Islamic Foundation imewekeza katika ujenzi wa vyumba vinne (4) madarasa vinavyojengwa kwa matofali ya block yaliyolazwa. katika ujenzi huo wananchi wa kata hiyo walichangia kiasi cha Tsh 200,000/ na Islamic Foundation imechangia zaidi ya Tsh milioni 40.
Katika kata ya Mji mpya, kwa mujibu wa Diwani wa kata hiyo Bw Wenceslaus, Taasisi ya The Islamic Foundation imechangia kiasi cha Tsh milioni moja kwa ajili ya kufanya ukarabati wa mfumo wa maji katika zahanati katani humo.
Samweli Msuya wa kata ya Mbuyuni anaielezea The Islamic Foundation kama Mkombozi wa kweli kwa jamii ya wana Morogoro na Tanzania kwa ujumla. Ameelezea kuwa viongozi wake ni wasikivu, wenye huruma na wenye imani.
Kwa kila kisima kirefu kilichochimbwa wamefunga jenereta kwa ajili ya kuvuta maji (kwa maeneo yasiyo na umeme)na wameweka Tank lenye ujazo wa lita 5,000.
Pia kwa kujali elimu na kuizingatia, The Islamic Foundation wanamiliki shule saba (7) na wameweza kujenga misikiti 700 nchi nzima. Pia wanatoa ufadhili kwa watoto wanaoshindwa kulipia gharama za masomo katika shule za msingi na sekondari na wanategemea kuanzisha bodi ya mikopo ya elimu ya juu.
Zaidi katika kuisaidia serikali kupambana na umasikini wameweza kutoa mitaji kwa wajane na vijana na pia wameanzisha kitengo maalumu kwa ajili ya councelling kwa vijana waathirika wa madawa ya kulevya.
Kuhusu haki ya kupata habari, wamewezesha kusimama imara kwa Radio Imaan na Tv Imaan.
Tunashukuru: "Mmeahidi, mkatimiza. Na ALLAH ni Shahidi"
Mwenye macho haambiwi Tazama