johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,635
- 142,977
Palikuwepo na Vikundi kama Green guards, Red brigade, Blue brigade nk nk kwenye vyama vya Siasa hususan CCM, Chadema, CUF na Nccr Mageuzi lakini Msajili wa Vyama akavipiga Marufuku
Baada ya kufuatilia kwa makini kinachoendelea Gaza niseme wazi Msajili wa Vyama vya Siasa alitumia busara na Hekima ya hali ya juu kupiga Marufuku mgambo kwenye vyama vya Siasa
Mungu ni mwema Wakati wote
===
Mwaka 2015 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu alipiga marufuku vikundi hivyo vya vyama vya siasa ambavyo vina muonekano na muundo wa vyombo vya usalama, kwani ni kinyume cha katiba na sheria ya nchi. Alivitaka vyama hivyo kuhakikisha vinafuata muongozo uliotolewa na Ofisi ya Msajili wa vyama hivyo na kama vikienda kinyume jeshi litapambana navyo.
Alivitaja vikundi hivyo na vyama vyao kwenye mabano kuwa ni Green Guard (CCM), Red Brigade (Chadema) na Blue Guard (CUF), ambavyo hutumiwa na vyama vya siasa hususan katika mikutano yao.
IGP Mangu aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Polisi uliokuwa ukijadili namna ya kuondoa vikundi hivyo pamoja na namna ya kuboresha shughuli za uendeshwaji wa vikundi hivyo. Alisema vikundi hivyo vipo kinyume cha sheria na kwamba kuendelea kuvimiliki kwa kisingizio chochote ni uvunjifu wa Katiba ya nchi na sheria ya vyama siasa, jambo ambalo polisi haliwezi kulivumilia.