Hongera kwa JK zasababisha Bushoke kuzomewa tamasha la Fiesta

Wasanii wetu wengi hawaangalii mbali wanaendekeza njaa sana badala yakujipanga nakuwa na malengo ya muda mrefu,nimakosa makubwa sana msanii kutumia usanii wake katika kufanikisha malengo ya chama fulani(chama chochote kile) hayo nimakosa makubwa sana na wengi sana watapotea mazima kama wasipo badilika.Msanii ana fans wake na hawa fans ni wapenzi na wanachama wa chama tofauti mpenzi wa msanii anabadilika muda wowote ule ila unapokuja kwenye swala la vyama ile ni zaidi ya mapenzi ni itikadi yaani inaingia hadi inakuwa Imani ya mtu juu ya kile chama.Nilisoma interview moja ya Nonini wa kenya jinsi anavyoepuka kujihusisha na chama chochote na akachambua kabisa kwa kina madhara yake katika kazi yake huyu Jamaa hata umpe bei gani kama ni function ya Chama apigi show za namna hiyo kabisa,msanii anaweza kuwa mwanachama wa chama fulani na tukalijua hilo iyo haina shida kwa cc fans ila kuitumia kazi yake kwaajili ya chama ndo inaleta shida na chuki.
 
jamani achenu kutataja hilo lichama, huku mie kichefuchefu nisaidieni kwa kuacha kuwatjataja hao magamba
 
Kwani hyo fiesta ilifanyka Msoga b'moyo eeeh...!? By then itabidi mdogo mwngne wa ****** akioa kule ikulu ndogo bagamoyo itabidi apelekwe akatumbuize.
 
ina maana faizafoxy hana airtime au mgonjwa??malari sugu je??sijaona gamba lolote likitetea
 
Tena mi nliumia sana,mana nilienda pale si vile napenda sana Fiesta,bali mtaani kwetu ilikuwa zamu ya Mgawo,so nikaona usiku utakuwa mrefu...kwa iyo nilikuwa pale na hasira za Mgao!Jamaa alipoanza..kwel shetani alipta nilitukana Bonge la tusi!Ila siku yangu ilirudi vizuri alipoingia yule jamaa na kibwagzo cha " Zomea Tanesco" watu "woooooooo"....BUSHOKE ALINIHARIBIA SANA SIKU
 
Hivi hizi habari mmempelekea huko Face bOOK ili ajue kinachoendelea? Hawezi kuleta uso wake kwenye hili jukwaa la wanaume mpelekeeni FB wakamchambue huko pia.
 
Nilishindwa kuamini jinsi msanii bushoke alipozomewa na kuonyeshwa ishara za kuwa atoke jukwaani baada ya kutoa pongezi kwa Kikwete.

Jamaa alipaniki mpaka akasahau hata kuchukua tuzo aliyotunukiwa na clouds kwa ajili ya ushiriki wa fiesta.

Siasa na Fiesta wapi na wapi? Hawa wasanii waache kujipendekeza sasa umezuka mtindo hasa nyakati za kampeni wanabadili nyimbo zilizopendwa na mashabiki wao zinakuwa za kisiasa, huku ni kujiua kisanii maana tayari unaleta mgawanyiko na chuki zisizokuwa za lazima leo hii ule wimbo wa pipiii! wa Marloo sijui marluu hata kuandika jina lake nimesahau, siupendi hata kuusikia kwa vile tu umekengeushwa ukatumika kwenye kampeni za CCM. Sijui kama wasanii wananielewa, na si hivyo tu hata kukengeusha wimbo kwa ajili ya matangazo ya biashara mfano Dully sykes, huu ni uzembe na ni dalili ya kutokuwa na ubunifu, inamaana hawawezi kabisa kutunga maalum kwa ajili hiyo?
 
Hivi msanii Dokii aliishia wapi vile, maana naye wakati wa kampeni alijifanya kuwapenda sana magamba!!!!!!!!!
 
NJAA mbaya jamani, anajaribu bahati yake Jk amwone, kwani kuna viti maalumu kwa wanaume ambavyo bushoke anaweza kuzawadiwa one day?
 
Binafsi sioni kama kuna tatizo mtu kumshukuru yoyote kwa mazuri aliyomfanyia hasira au ushabiki mwingine tunapeleka pasipostahili,i dont like that!
 
Nilishindwa kuamini jinsi msanii bushoke alipozomewa na kuonyeshwa ishara za kuwa atoke jukwaani baada ya kutoa pongezi kwa Kikwete.

Jamaa alipaniki mpaka akasahau hata kuchukua tuzo aliyotunukiwa na clouds kwa ajili ya ushiriki wa fiesta.

Kweli hali ni mbaya.

Huyu njaa sasa hivi inamsumbua anacho fanya nikujikomba kwa JK imradi aongeze safari za kwenda chooni.
 
Bushoke na marlaw sinunui cd zao na hata mtandaoni ninazihack, waende kwenye siasa waache mziki. Cd zao ninazipiga vita.
 
Nchi hii imekuwa nzuri sana maana watu wanajua wanachokitaka. Kuna dogo mmoja wa Mbeya ameibuka na verse " ZOMEA TANESCO"
 
Mi nafikiri alitoa pongezi mahali ambapo hapastahili akijua kuwa labda jamaa wamelewa...............siasa hadi kwene starehe...................alitaka akumbukwe kwenye kampeni za Igunga......................
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom