"Hongera JK kwa kukuza uchumi"-watanzania wa Australia

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Umoja wa Watanzania waishio Australia umempöngeza rais Kikwete kwa kukuza uchumi wa nchi,na kuifanya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi 10 dunian,ambazo uchumi wake unakua kwa kasi sana.
Pia wamempongeza kwa kuruhusu uhuru wa habari,kwani japo wao wapo ughaibuni lakin wanapata habari
sosi:habari kwa ufupi ya saa kumi alasiri@ radio one
 
Waambie wampe zawadi ya U-Prof hizo Phd anazo nyingi mno, akili zao zipo wapi hao wabongo waishio huko? wanajua matatizo ya huku nyumbani au wanampa sifa za kijinga huyo Fisadi?
 
Dola moja ya Marekani leo hapa Arusha tarehe 27/10/2011 inanunuliwa kwa shilingi 1800 kweli uchumi unakua kwa kasi mno!
 
ndallo nini tena?

Hawa wakimbizi wakibongo wamekimbia bongo kutokana na maisha magumu halafu wanampa jamaa kichwa kwakusema uchumi hapa unakua kwa kasi sasa si warudi kuja kuwekeza walichovuna huko? Nyambafuuuuu!
 
Hivi nyie watu wa Australia mna mawasiliano na watu wa nyumbani? Uchumi gani umekuwa sasa? au mnampamba tu ili aweze patiwa phd nyingine ya uchumi sio
 
Duh uchumi unakua sana kwa kweli maana kwa sasa kilo ya sukari ni 3000 na bado haipatikani na inabidi tununue kwa coupon
Duh kweli uchumi unakua kwa mujibu wa waishio Australia

Hivi kweli hao jamaa wanajua maisha ya mtanzania wa kule meatu au mfaranyaki au hungumalwa au kasulu au wanaongea tuu
 
Hao sio watanzania ni waaustralia hawajui lolote kuhusu nchi yetu,ndio maana wanapongezana kwa ujinga pumbavu sana.
 
Back
Top Bottom