Hongera ITV kumhoji Tundu Lissu. Hongera sana Tundu Lissu kuzungumza kistaarabu kwa lugha za staha. Ruksa kuhisi chochote, sio fair kutaja majina!

Kumtaja Magufuli siyo kosa. Kwenye kampeni mtu aweza jenga hoja kwa stage mbili; 1. statement of problems, 2) statement of solutions. Hivyo mtu aweza taja matatizo yaliyopo na mtu aliye yaleta, kisha akataja solutions za hayo matatizo.

Kwa maouvu aliyofanya Magufuli, si vema kuyafunmbia macho. Ameondoa freedom of speech, right to peaceful assembly, ameteka watu na wengine wamepotea hatuwaoni tena. Ameweka watu ndani kwa makosa ya uongo, ameua biashara n.k. Sasa utaachaje kumtaja?

Kama maovu ya Magufuli yangekuwa yameelekezwa kwenye ilani ya CCM, basi hapo lawama zingeenda kwa chama. Haya ni mambo yake yeye Magufuli binafsi, hivyo lazima atajwe.
 
Ulinambia kwamba if you can not beat them, then join them. Lakini, mimi nadhani ni vema ukawa na msimamo wako binafsi. Mayalla, we have our morals, our values and principles. Government regimes may change but you need to stand by your values and principles. Do not join a nonsensical regime simply because you desire to become an affluent individual. Remain an upright person regardless of the regime.
 
Pascal acha kuanza kupoteza mjadala wa leo wa Lissu kuwafunika vibaya sana CCM na mgombea wenu. Hoja kuu ya leo ni Lissu alivyoonesha uwezo wake mkubwa kwenye upeo na maono ya kuipeleka hii nchi mbali.

Huu mjadala unaoanzisha hapa kuhamisha hoja kuu ya leo, napenda kukwambia umeshafeli kabla hujaanza. Hakuna hata moja ambalo Lissu amekosea kwenye kujibu kwenye kipindi cha dk 45.
Hahaha blaza ule ndio uwezo kweli Uwezo wa kutokujua umeme wa Maji na mwingine upi ni umeme rahisi kabisa duniani? Nadhani Tundu lisu hajui kuwa Kuna Miradi ya umeme wa Jua Kigoma na Same, hajui kuna Mradi wa umeme wa Upepo Singida ambako ni kwao?

Mgombea anaeongea kuhusu mfuko wa mafuta wa Norway ambao hajui kazi yake ni nini?...Uwiii .Mgombea anayeongelea Universal health care bila kuchambua atafikiaje hiyo universal health care....hahaha VIVA MAGUFULI KANYAGA TWENDE
 
Tatizo lako umeacha kuchukua hoja ya msingi kuwa 2017 imetungwa sheria ya kudhibiti vyama visiweze kuungana bila msajiri kukubali huo muungano ndiyo hoja yake ya msingi. Lakini pia kama mtu amekuteau kuna kosa gani kumuuliza hata kama hawezi kukuondoa anapokuteua maana yake unafanyakazi kwa niaba yake kama siyo hivyo kwanini akuteue yeye.

Hii hoja ya kila siku kusema mtu akiteuliwa anakuwa independent kivipi na tumeona CAG Prof Asad amefungashiwa virago akiwa na miaka 58 sasa hiyo independent unayoongelea wewe ni ipi. Vyama vya Siasa vilizuiwa kufanya Siasa miaka 5 na vimepewa usajiri wa kudumu havina wabunge havikufanya Siasa kabisa hadi uchaguzi umefika na msajiri wa vyama yupo independent ipi hapo unayoiongelea hasa.
 
Hahaha blaza ule ndio uwezo kweli Uwezo wa kutokujua umeme wa Maji na mwingine upi ni umeme rahisi kabisa duniani? Nadhani Tundu lisu hajui kuwa Kuna Miradi ya umeme wa Jua Kigoma na Same , hajui kuna Mradi wa umeme wa Upepo Singida ambako ni kwao?....Mgombea anaeongea kuhusu mfuko wa mafuta wa Norway ambao hajui kazi yake ni nini?...Uwiii .Mgombea anayeongelea Universal health care bila kuchambua atafikiaje hiyo universal health care....hahaha VIVA MAGUFULI KANYAGA TWENDE

Unaonesha jinsi ulivyo na uelewa mdogo kwanza hajasema universal health care amesema universal health insurance ndiyo maana hukuelewa. Kuhusu Norway yuko sahihi alichosema kwasababu ametolea mfano namna nchi zingine zinavyonufaika na rasilimali lakini nchi ya Equatorial Guinea ilivyo masikini pamoja na kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta kutokana na uongozi mbaya.
 
Back
Top Bottom