Hoja za Mwigamba zikithibitika, natoa rai Dr. Slaa, Mbowe na Zitto watuachie CHADEMA yetu

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,282
Tuhuma alizozitoa Mwigamba dhidi ya chama nimezisoma vizuri JF, nasikitika kwa kiongozi wa nyadhifa yake kutumia mtandao wa kijamii kuyasema yale mbaya zaidi kwa kutumia jina la bandia. Wenzetu waliokuwa kwenye vikao vya maamuzi wanakikosoa chama kwa kutumia mitandao, je, sisi tusiokuwa kwenye hivyo vikao tutatumia nini?

Vijana wengi waCHADEMA tumekilaani na kukoseshwa raha na kitendo cha Mwigamba, pamoja na hayo, hoja alizokuja nazo hadharani Mwigamba si za kubezwa hata kidogo. Tulaani kwa upande mmoja na tujikite kwenye maudhui ya hoja zake kwa upende wa pili.

Tunaomba viongozi wetu wakuu wa CHADEMA waangalie namna wanavyopokea mawazo mapya, namna wanavyowasikiliza wachache, namna ya kutekeleza maamuzi ya wengi(wengi wape) na namna ya kutekeleza maamuzi na maagizo ya vikao vikubwa vya kichama. Moja ya hoja ya Mwigamba kuwa vikao na maamuzi yake haviheshimiwi na viongozi wakuu aliowataja, sitaki kuamini kuwa hizo kasoro alishawahi kuzisema kwenye vikao sema tu hao viongozi kama alivyosema hawasikilizi maamuzi ya vikao, kama hawasikilizi maamuzi ya vikao wataweza kumsikiliza mtu mmoja anaye wakosoa? kama ndivyo basi hii ndio sababu iliyopelekea kutoka hadharani.

Huenda namna ya hizo nilizozianisha hapo juu zikawa hazifanywi katika namna ya kuridhisha na kupendeza, kama ndivyo, majukwaa ya ndani ya chama yatakuwa yananyima fursa ya kupokea mawazo mapya na kukosoa utendaji wa ofisi za viongozi wakuu. CHADEMA ijitathimini kwa hili, isiishie kumchukulia hatua za kinidhamu tu Mwigamba bila kuzifanyia kazi hoja alizokuja nazo hadharani.

Nimefurahi kusikia kuwa ametakiwa kudhithibitisha tuhuma alizozitoa dhidi ya viongozi wakuu wa chama, natoa rai kama tuhuma hizi zikithibiti basi Dr.Slaa, Mbowe, Zitto, Arfi na viongozi kama hao wa upande wa Zanzibar wajiuzulu nyadhifa zao. Wabaki kama wanachama wa kawaida na tuingize uongozi mwingine, uongozi utakaokuja kuendeleza mazuri ya watu hao na kuacha mabaya ya watu hao.( kama hayo mabaya yapo na yakithibiti). Endapo haya mambo yakithibiti na wasipojiuzulu basi itakuwa ni ndoto kwa CCM kutoka ikulu na ni ndoto kwa CHADEMA kuingia ikulu.

Kama Mwigamba akishindwa kuthibitisha hizi tuhuma alizozitoa dhidi ya viongozi wakuu wa chama, asiishie kuvuliwa uongozi tu, lakini pia afukuzwe uanachama na ikibidi ashitakiwe mahakamani kutokana kitendo hichi kibaya na kichafu ili iwe fundisho kwa watu wote wenye tabia kama hii ambao bado hawajajulikana, kwa kufanya hivi hao wengine ambao bado hawajulikana wanaweza kuacha tabia hii kwa kuchelea kukutwa na kitakachompata Mwigamba. Nafikiri hii ndio itakuwa njia ya pekee ya kulinda nidhamu na heshima ya chama mbele ya wanachama na watanzania kwa ujumla ambao kimsingi ndio wanunuaji wa sera zetu. Tukilea ujinga huu watatokea wengi wa kutuvuruga kisa tu waliona Mwigamba kapewa adhabu ndogo au onyo la kulaza ukope.

Hata hivyo sisi tulio nje ya ya vikao tunaweza kujiuliza operesheni ya M4C imepotelea wapi? Au tumeicha mara baada ya kutokea tukio la Iringa na vurugu za gesi Mtwara? Hivi ni kweli CCM wanatuandalia matukio bila kujua? Je, wakiacha kuandaa hayo matukio kisa tu Mwigamba kawashutua ndio CHADEMA bai bai? Pia tunaweza kujiuliza uchaguzi wa chama utafanyika lini ikiwa ilisemekana hadi desemba mwaka huu uchaguzi ungekuwa umekwisha malizika kwa ngazi zote, tunajiuliza hili la uchaguzi nalo limepotelea wapi? Hizi ni baadhi ya hoja chache alizokuja nazo Mwigamba hadharani. Je, sisi wanaCHADEMA tuishie kuona usaliti wa Mwigamba bila kuzingatia hoja hizi? Kwanini viongozi wasizijibu hoja za Mwigamba?

Kwa vyovyote vile watazijibu, wakati Mwigamba akithibitisha hizi tuhuma, subira ndio kila kitu katika hili, kama katakiwa kuthibitisha na kwa vyovyote vile nasi twakiwa kusubiri, kama ndivyo huu wimbo wa usaliti usaliti unapata uhalali gani katika kipindi hichi cha kusubiri? Na wale wanawalaumu Mbowe na viongozi wenziwe waliotajwa katika bandiko la Mwigamba pia wanapata uhalali gani wa kufanya hivyo ikiwa bado Mwigamba hajathibitisha katika vikao halali na uthibitisho huo kukubalika? Tuvute subira kwani siku zote ndio huvuta heri, kinyume chake labda tunataka maamuzi ya chama juu ya hili yazingatie mbwembwe zetu badala ya uthibitisho wenyewe.

Pamoja na hayo, Mwigamba kama aliona mawazo yake hayasikilizwi na kutekelezwa, na kama aliamini mawazo yake ni sahihi na yako kwaajili ya kujenga chama, basi ni vema MOSI angejiuzulu; hakuna umuhimu wa kufanya kazi na watu usiowaamini na kuwakubali au wasiokusikiliza au wanaokubeza. Pili, angetoka hadharani, tena si kwakutumia jina bandia, bali angetumia jina lake halisi, angetangaza kujiuzulu kwake na mapungufu aliyoyasema angeyataja kama sababu ya kujiuzulu huko.

Kitendo cha kuusifia uongozi wa Dr.Slaa na Mh.Mbowe kwenye kikao halali cha chama, na kisha kwa kutumia jina la bandia akawa anaukandia huo uongozi kama vile hakuusifia muda fupi uliopita kwa wakati ule, ni usaliti kwa uzalendo wake kwa chama, usaliti kwa weledi wake ambao wengi wetu tunaujua na mwisho ni usaliti kwa uanaume wake; kwani hatutaraji kwa mwanaume kusema vitu sahihi na anavyoviamini kwa kutumia jina la bandia kisa tu asijulikane. Nitaendelea kumlaumu Mwigamba kwa hili haijalishi alichokisema ni sahihi au la!

Halafu hili suala la viongozi na wanachama kutumia mitandao vibaya na bila ridhaa ya CHADEMA yenyewe limekuwa kama vile limeota mizizi fulani vilee. Kipindi fulani tulishuhudia Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA akitupiana maneno na wajumbe wa kamati kuu kisa tu namba yake lilikuwa kwenye tamko la wajumbe hao walilolitoa kwa niaba ya chama, wengine tunajiuliza, kama lile lilikuwa tamko la chama lililobarikiwa na kamati kuu iweje Naibu Katibu mkuu alipinge hadharani ikiwa na yeye ni mjumbe wa kamati kuu ikiwa kimsingi na kikatiba yeye ni zao la tamko? Nimelitaja hili kwa lengo la kuonesha hii tabia ya kutumia mitandao ya kijamii kwa namna mbaya na chafu kwa Mwigamba si wa kwanza na limbuko.

Pia tulishuhudia vijana wakimtuhumu Zitto kuwa ni msaliti na mengi yalisemwa, vijana waliokuwa wanasema Zitto msaliti ni wanachama na wanajulikana vizuri, lakini hadi leo hii na kwa vyovyote vile hawajaitwa kuthibitisha usaliti wa Zitto na wanaendelea hadi sasa katika mitandao kumuandama Zitto. Hotuba aliyoitoa Zitto katika mkutano wa CHADEMA Tabora hivi karibuni aliwaasa vijana waache kuwagombanisha viongozi wakuu wa chama, alisema vijana wanashinda kwenye mitandao kugombanisha viongozi, kwa vyovyote vile Zitto alisema hivi huku akizingatia mambo yanayofanywa na baadhi ya vijana kwenye mitandao. Hili la Mwigamba ni matokeo ya CHADEMA kushindwa kuwadhibiti baadhi ya vijana wa CHADEMA wanaotumia mitandao kukichafua chama na inaonekana mwindelezo tu wa tabia za watu kudhani kuwa CHADEMA iko kwenye mitandao ingawa kiukweli CHADEMA iko kwenye mioyo ya wananchi.

[video=youtube_share;zh5tiBoZKjw]http://youtu.be/zh5tiBoZKjw[/video]
Zitto Kabwe akiwaasa vijana waache kugombanisha viongozi katika mkutano wa Tabora.

HITIMISHO:
Mara nyingi tunaambiwa wagawe kisha watawale. CCM inafanya kila hali kuhakikisha Viongozi wa CHADEMA na wanachama wao wanakuwa wanagawanyika ili wapate kutushinda na kututawala kwa muda mrefu watakavyo. Tunavyowakosoa viongozi wetu hadharani, kwa vyovyote vile CCM watajifanya kama vile wanaunga mkono ule upande unaokosolewa, lengo la kufanya hivyo ili wale wanaokosoa waone wale wanaowakosoa kuwa ni wasaliti kisa tu wanaungwa mkono na CCM. Hivyo sitoshangaa kuona CCM wakimuunga mkono Mwigamba kama vile wanavyojifanya wanamuunga mkono Zitto.

Hitimisho langu linalenga kwa sisi wanaCHADEMA tulio nje ya vikao vikubwa vya maamuzi, tuwaunge mkono viongozi wetu wote, kukiwa na ulazima wa kuwakosoa, basi tufanye hivyo kwa kuzingatia hoja na kwa kufuata utaratibu(kinyume chake vurugu na usaliti); kwa kufanya hivyo tutaweza kujadili hoja kwa kuzingatia maudhui ya hoja yenyewe na si kwa kuzingatia wasifu wa mtoa hoja ambao hausiani na hoja yake(upo wasifu wa mtoa hoja wenye kuhusiana na hoja yake) lakini kubwa tutaweza kujitoa kwenye ulimwengu wa macho ya nazi na ushabiki wa kichamchunga.

Hitimisho langu linalenga kutukumbusha kuwa hakuna wakati ambao CHADEMA yahitaji mshikamano na utangamano kama wakati wa sasa; wakati ambao CCM imeshagundua iko chumba cha wagonjwa mahututi na inajiandaa kisaikolojia kwa kushindwa uchaguzi ujao(Rejea hotuba ya Kikwete aliyoitoa tar 24 mjini Dodoma). Ili tuwe na mshikamano na huo utengamano ni lazima viongozi wakuu wa chama wakaonesha njia na kuwadhihirishia umma kuwa wao ni wamoja na hakuna matatizo miongoni mwao na wawatake watu wasiamini kuwa wao viongozi wakuu na migogoro kama watu wanaoshinda kwenye mitandao wanavyojaribu kuaminisha umma kuwa CHADEMA iko na migogoro. Tusipofanya hivyo, CCM itajiandaa kisaikolojia kwa kupokea ushindi badala ya kujindaa kupokea kipigo toka kwa CHADEMA.

Hitimisho langu linalenga kuwa si kila mwanaCHADEMA anayeikosoa CHADEMA na viongozi wake ni msaliti na katumwa na CCM hata kama huyo mkosoaji anaungwa mkono na CCM(Zingatia sababu za CCM kuwaunga mkono wakosoaji wa CHADEMA waliomo ndani ya CHADEMA), bali ifike mahala tukubali kuwa chama kimekua kikubwa na kina watu wengi na kila mmoja wetu yuko na uwezo wake wa kufikiri na kuyatazama mambo, kwa kuzingatia hilo, ni sahihi msimamo yetu na maoni yetu kutofautiana kama vile uwezo wa kufikiri kwetu unavyotafautiana. Ni hivi, lile ambalo waliona "sahihi" kwa uwezo wako wa kufikiri na mwingine kwa uwezo huo huo anaweza kuliona "si sahihi" kwa hivyo kuheshimiana, kusikilizana na kufuata mawazo ya wengi yaliyozingatia hoja za wachache ndio kila kitu katika maisha ya seti kuu iitwayo chama cha siasa, kinyume chake ni vurugu kama si udikteta uliodhahiri.

Hitimisho langu lanalenga kutoa waasa kwa vijana, kwa kuanzia mimi niliyeandika haya na kwa wenzangu wote, tusimamie misingi ya chama na tujenge hiyo misingi kwenye mioyo yetu, tuwe wanachama wa kumaanisha na si wanachama kadi au vumbi. Wanachama wa CHADEMA wa kumaanisha ni wale ambao hata kama Dr.Slaa akirudi CCM wao wataendelea kuwa CHADEMA, haturajii kwa mwanachama wa kumaanisha kuingia CCM kisa tu Zitto Kabwe kajiunga na CCM. Mwanachama aliye na msingi wa CHADEMA katika moyo wake hawezi kuwakosoa viongozi wake kinyume na taratibu na katu hawezi kuwatetea viongozi wake wabadhirifu kisa tu yuko na mahaba na hao viongozi.

BILA CHADEMA IMARA MAFISADI WATATAMBA MCHANA WA JUA UTOSI.

MIMI NA WEWE TUIFANYE KUWA IMARA.

MwanaCHADEMA.

Njano5
0784845394.
 
Chadema yenu?

Acha kuota ndoto mchana. Unajua Chadema imeanzishwa na pesa za nani na kwa madhumuni gani?

Kama umeshindwa ondoka, lakini usijidanganye kuwa kuna kitu kinaitwa Chadema yenu.

Usiingize siasa kwenye biashara za watu...
 
Acheni unafiki Jamani. Mbona kila siku ni wewe tu? Mnatumika vibaya sana!
 
Umekaribishwa kwenye shughuli ya watu, kuwa mpole. Usiwe kimbelembele.

Anzisha chama chako uone kama rahisi.
 
Acheni unafiki Jamani. Mbona kila siku ni wewe tu? Mnatumika vibaya sana!

Mkuu,

Jamaa anaingilia biashara ya watu. Hajui jinsi ya kula na kipofu.

Hajui watu wameingia gharama kubwa kuanzisha Chadema project. Yeye anadhani yaliyoandikwa kwenye katiba ya chadema ni kweli, kumbe ni kukidhi mahitaji ya msajili tu...
 
Binafsi naunga mkono hoja, chama ni taasisi, lazima maamuzi ya vikao yaheshimiwe! Wapi chuo cha uongozi wa chama pale kibaha? Je media ya chama wapi? Vipi kuendelea kupanga ofisi ya chama? Kwa nini isijengwe ofisi ya chama? Chadema bado inasafari ndefu, kukitetea chama ndani ili kisimame kama taasisi!
 
Tuhuma alizozitoa Mwigamba dhidi ya chama nimezisoma vizuri JF, nasikitika kwa kiongozi wa nyadhifa yake kutumia mtandao wa kijamii kuyasema yale mbaya zaidi kwa kutumia jina la bandia. Wenzetu waliokuwa kwenye vikao vya maamuzi wanakikosoa chama kwa kutumia mitandao, je, sisi tusiokuwa kwenye hivyo vikao tutatumia nini?

Vijana wengi waCHADEMA tumekilaani na kukoseshwa raha na kitendo cha Mwigamba, pamoja na hayo, hoja alizokuja nazo hadharani Mwigamba si za kubezwa hata kidogo. Tulaani kwa upande mmoja na tujikite kwenye maudhui ya hoja zake kwa upende wa pili.

Tunaomba viongozi wetu wakuu wa CHADEMA waangalie namna wanavyopokea mawazo mapya, namna wanavyowasikiliza wachache, namna ya kutekeleza maamuzi ya wengi(wengi wape) na namna ya kutekeleza maamuzi na maagizo ya vikao vikubwa vya kichama. Moja ya hoja ya Mwigamba kuwa vikao na maamuzi yake haviheshimiwi na viongozi wakuu aliowataja, sitaki kuamini kuwa hizo kasoro alishawahi kuzisema kwenye vikao sema tu hao viongozi kama alivyosema hawasikilizi maamuzi ya vikao, kama hawasikilizi maamuzi ya vikao wataweza kumsikiliza mtu mmoja anaye wakosoa? kama ndivyo basi hii ndio sababu iliyopelekea kutoka hadharani.

Huenda namna ya hizo nilizozianisha hapo juu zikawa hazifanywi katika namna ya kuridhisha na kupendeza, kama ndivyo, majukwaa ya ndani ya chama yatakuwa yananyima fursa ya kupokea mawazo mapya na kukosoa utendaji wa ofisi za viongozi wakuu. CHADEMA ijitathimini kwa hili, isiishie kumchukulia hatua za kinidhamu tu Mwigamba bila kuzifanyia kazi hoja alizokuja nazo hadharani.

Nimefurahi kusikia kuwa ametakiwa kudhithibitisha tuhuma alizozitoa dhidi ya viongozi wakuu wa chama, natoa rai kama tuhuma hizi zikithibiti basi Dr.Slaa, Mbowe, Zitto, Arfi na viongozi kama hao wa upande wa Zanzibar wajiuzulu nyadhifa zao. Wabaki kama wanachama wa kawaida na tuingize uongozi mwingine, uongozi utakaokuja kuendeleza mazuri ya watu hao na kuacha mabaya ya watu hao.( kama hayo mabaya yapo na yakithibiti). Endapo haya mambo yakithibiti na wasipojiuzulu basi itakuwa ni ndoto kwa CCM kutoka ikulu na ni ndoto kwa CHADEMA kuingia ikulu.

Kama Mwigamba akishindwa kuthibitisha hizi tuhuma alizozitoa dhidi ya viongozi wakuu wa chama, asiishie kuvuliwa uongozi tu, lakini pia afukuzwe uanachama na ikibidi ashitakiwe mahakamani kutokana kitendo hichi kibaya na kichafu ili iwe fundisho kwa watu wote wenye tabia kama hii ambao bado hawajajulikana, kwa kufanya hivi hao wengine ambao bado hawajulikana wanaweza kuacha tabia hii kwa kuchelea kukutwa na kitakachompata Mwigamba. Nafikiri hii ndio itakuwa njia ya pekee ya kulinda nidhamu na heshima ya chama mbele ya wanachama na watanzania kwa ujumla ambao kimsingi ndio wanunuaji wa sera zetu. Tukilea ujinga huu watatokea wengi wa kutuvuruga kisa tu waliona Mwigamba kapewa adhabu ndogo au onyo la kulaza ukope.

Hata hivyo sisi tulio nje ya ya vikao tunaweza kujiuliza operesheni ya M4C imepotelea wapi? Au tumeicha mara baada ya kutokea tukio la Iringa na vurugu za gesi Mtwara? Hivi ni kweli CCM wanatuandalia matukio bila kujua? Je, wakiacha kuandaa hayo matukio kisa tu Mwigamba kawashutua ndio CHADEMA bai bai? Pia tunaweza kujiuliza uchaguzi wa chama utafanyika lini ikiwa ilisemekana hadi desemba mwaka huu uchaguzi ungekuwa umekwisha malizika kwa ngazi zote, tunajiuliza hili la uchaguzi nalo limepotelea wapi? Hizi ni baadhi ya hoja chache alizokuja nazo Mwigamba hadharani. Je, sisi wanaCHADEMA tuishie kuona usaliti wa Mwigamba bila kuzingatia hoja hizi? Kwanini viongozi wasizijibu hoja za Mwigamba?

Kwa vyovyote vile watazijibu, wakati Mwigamba akithibitisha hizi tuhuma, subira ndio kila kitu katika hili, kama katakiwa kuthibitisha na kwa vyovyote vile nasi twakiwa kusubiri, kama ndivyo huu wimbo wa usaliti usaliti unapata uhalali gani katika kipindi hichi cha kusubiri? Na wale wanawalaumu Mbowe na viongozi wenziwe waliotajwa katika bandiko la Mwigamba pia wanapata uhalali gani wa kufanya hivyo ikiwa bado Mwigamba hajathibitisha katika vikao halali na uthibitisho huo kukubalika? Tuvute subira kwani siku zote ndio huvuta heri, kinyume chake labda tunataka maamuzi ya chama juu ya hili yazingatie mbwembwe zetu badala ya uthibitisho wenyewe.

Pamoja na hayo, Mwigamba kama aliona mawazo yake hayasikilizwi na kutekelezwa, na kama aliamini mawazo yake ni sahihi na yako kwaajili ya kujenga chama, basi ni vema MOSI angejiuzulu; hakuna umuhimu wa kufanya kazi na watu usiowaamini na kuwakubali au wasiokusikiliza au wanaokubeza. Pili, angetoka hadharani, tena si kwakutumia jina bandia, bali angetumia jina lake halisi, angetangaza kujiuzulu kwake na mapungufu aliyoyasema angeyataja kama sababu ya kujiuzulu huko.

Kitendo cha kutumia jina la bandia na kusifia uongozi wa Dr.Slaa na Mh.Mbowe kwenye kikao halali cha chama, na kisha kwa kutumia jina la bandia akawa anaukandia huo uongozi kama vile hakuusifia muda fupi uliopita kwa wakati ule, ni usaliti kwa uzalendo wake kwa chama, usaliti kwa weledi wake ambao wengi wetu tunaujua na mwisho ni usaliti kwa uanaume wake; kwani hatutaraji kwa mwanaume kusema vitu sahihi na anavyoviamini kwa kutumia jina la bandia kisa tu asijulikane. Nitaendelea kumlaumu Mwigamba kwa hili haijalishi alichokisema ni sahihi au la!

Halafu hili suala la viongozi na wanachama kutumia mitandao vibaya na bila ridhaa ya CHADEMA yenyewe limekuwa kama vile limeota mizizi fulani vilee. Kipindi fulani tulishuhudia Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA akitupiana maneno na wajumbe wa kamati kuu kisa tu namba yake lilikuwa kwenye tamko la wajumbe hao walilolitoa kwa niaba ya chama, wengine tunajiuliza, kama lile lilikuwa tamko la chama lililobarikiwa na kamati kuu iweje Naibu Katibu mkuu alipinge hadharani ikiwa na yeye ni mjumbe wa kamati kuu ikiwa kimsingi na kikatiba yeye ni zao la tamko? Nimelitaja hili kwa lengo la kuonesha hii tabia ya kutumia mitandao ya kijamii kwa namna mbaya na chafu kwa Mwigamba si wa kwanza na limbuko.

Pia tulishuhudia vijana wakimtuhumu Zitto kuwa ni msaliti na mengi yalisemwa, vijana waliokuwa wanasema Zitto msaliti ni wanachama na wanajulikana vizuri, lakini hadi leo hii na kwa vyovyote vile hawajaitwa kuthibitisha usaliti wa Zitto na wanaendelea hadi sasa katika mitandao kumuandama Zitto. Hotuba aliyoitoa Zitto katika mkutano wa CHADEMA Tabora hivi karibuni aliwaasa vijana waache kuwagombanisha viongozi wakuu wa chama, alisema vijana wanashinda kwenye mitandao kugombanisha viongozi, kwa vyovyote vile Zitto alisema hivi huku akizingatia mambo yanayofanywa na baadhi ya vijana kwenye mitandao. Hili la Mwigamba ni matokeo ya CHADEMA kushindwa kuwadhibiti baadhi ya vijana wa CHADEMA wanaotumia mitandao kukichafua chama na inaonekana mwindelezo tu wa tabia za watu kudhani kuwa CHADEMA iko kwenye mitandao ingawa kiukweli CHADEMA iko kwenye mioyo ya wananchi.

<font size="3">[video=youtube_share;zh5tiBoZKjw]http://youtu.be/zh5tiBoZKjw[/video]
Zitto Kabwe akiwaasa vijana waache kugombanisha viongozi katika mkutano wa Tabora.

HITIMISHO:
Mara nyingi tunaambiwa wagawe kisha watawale. CCM inafanya kila hali kuhakikisha Viongozi wa CHADEMA na wanachama wao wanakuwa wanagawanyika ili wapate kutushinda na kututawala kwa muda mrefu watakavyo. Tunavyowakosoa viongozi wetu hadharani, kwa vyovyote vile CCM watajifanya kama vile wanaunga mkono ule upande unaokosolewa, lengo la kufanya hivyo ili wale wanaokosoa waone wale wanaowakosoa kuwa ni wasaliti kisa tu wanaungwa mkono na CCM. Hivyo sitoshangaa kuona CCM wakimuunga mkono Mwigamba kama vile wanavyojifanya wanamuunga mkono Zitto.

Hitimisho langu linalenga kwa sisi wanaCHADEMA tulio nje ya vikao vikubwa vya maamuzi, tuwaunge mkono viongozi wetu wote, kukiwa na ulazima wa kuwakosoa, basi tufanye hivyo kwa kuzingatia hoja na kwa kufuata utaratibu(kinyume chake vurugu na usaliti); kwa kufanya hivyo tutaweza kujadili hoja kwa kuzingatia maudhui ya hoja yenyewe na si kwa kuzingatia wasifu wa mtoa hoja ambao hausiani na hoja yake(upo wasifu wa mtoa hoja wenye kuhusiana na hoja yake) lakini kubwa tutaweza kujitoa kwenye ulimwengu wa macho ya nazi na ushabiki wa kichamchunga.

Hitimisho langu linalenga kutukumbusha kuwa hakuna wakati ambao CHADEMA yahitaji mshikamano na utangamano kama wakati wa sasa; wakati ambao CCM imeshagundua iko chumba cha wagonjwa mahututi na inajiandaa kisaikolojia kwa kushindwa uchaguzi ujao(Rejea hotuba ya Kikwete aliyoitoa tar 24 mjini Dodoma). Ili tuwe na mshikamano na huo utengamano ni lazima viongozi wakuu wa chama wakaonesha njia na kuwadhihirishia umma kuwa wao ni wamoja na hakuna matatizo miongoni mwao na wawatake watu wasiamini kuwa wao viongozi wakuu na migogoro kama watu wanaoshinda kwenye mitandao wanavyojaribu kuaminisha umma kuwa CHADEMA iko na migogoro. Tusipofanya hivyo, CCM itajiandaa kisaikolojia kwa kupokea ushindi badala ya kujindaa kupokea kipigo toka kwa CHADEMA.

Hitimisho langu linalenga kuwa si kila mwanaCHADEMA anayeikosoa CHADEMA na viongozi wake ni msaliti na katumwa na CCM hata kama huyo mkosoaji anaungwa mkono na CCM(Zingatia sababu za CCM kuwaunga mkono wakosoaji wa CHADEMA waliomo ndani ya CHADEMA), bali ifike mahala tukubali kuwa chama kimekua kikubwa na kina watu wengi na kila mmoja wetu yuko na uwezo wake wa kufikiri na kuyatazama mambo, kwa kuzingatia hilo, ni sahihi msimamo yetu na maoni yetu kutofautiana kama vile uwezo wa kufikiri kwetu unavyotafautiana. Ni hivi, lile ambalo waliona "sahihi" kwa uwezo wako wa kufikiri na mwingine kwa uwezo huo huo anaweza kuliona "si sahihi" kwa hivyo kuheshimiana, kusikilizana na kufuata mawazo ya wengi yaliyozingatia hoja za wachache ndio kila kitu katika maisha ya seti kuu iitwayo chama cha siasa, kinyume chake ni vurugu kama si udikteta uliodhahiri.

Hitimisho langu lanalenga kutoa waasa kwa vijana, kwa kuanzia mimi niliyeandika haya na kwa wenzangu wote, tusimamie misingi ya chama na tujenge hiyo misingi kwenye mioyo yetu, tuwe wanachama wa kumaanisha na si wanachama kadi au vumbi. Wanachama wa CHADEMA wa kumaanisha ni wale ambao hata kama Dr.Slaa akirudi CCM wao wataendelea kuwa CHADEMA, haturajii kwa mwanachama wa kumaanisha kuingia CCM kisa tu Zitto Kabwe kajiunga na CCM. Mwanachama aliye na msingi wa CHADEMA katika moyo wake hawezi kuwakosoa viongozi wake kinyume na taratibu na katu hawezi kuwatetea viongozi wake wabadhirifu kisa tu yuko na mahaba na hao viongozi.

BILA CHADEMA IMARA MAFISADI WATATAMBA MCHANA WA JUA UTOSI.

MIMI NA WEWE TUIFANYE KUWA IMARA.

MwanaCHADEMA.

Njano5
0784845394.

Nikweli CDM sasa ina watu wengi na wenye mawazo na uelewa tofauti, viongozi walijue hili, na dunia sasa imebadilika sana njia za kujieleza nazo zimekuwa nyingi na rahisi viongozi walijue hili. ni muhimu saana viongozi watimize wajibu wao na kuzingatia sheria kanuni na maamuzi ya vikao itapunguza ama kuondoa misuguano hii. mi sipendi kufukuzana na sitaki kabisa viongozi kulopoka kwenye mitandao au kwenye media mambo ambayo yangezungumzwa kwenye vikao vya chama.
 
Mkuu,

Jamaa anaingilia biashara ya watu. Hajui jinsi ya kula na kipofu.

Hajui watu wameingia gharama kubwa kuanzisha Chadema project. Yeye anadhani yaliyoandikwa kwenye katiba ya chadema ni kweli, kumbe ni kukidhi mahitaji ya msajili tu...

Toka nizaliwe mpaka umri huu sijawahi kukutana na binadamu
Mjinga
Mnafiki
Mbea
Muongo
Kilaza
Taahira kama ZeMarcopolo!
 
Last edited by a moderator:
Chadema yenu?

Acha kuota ndoto mchana. Unajua Chadema imeanzishwa na pesa za nani na kwa madhumuni gani?

Kama umeshindwa ondoka, lakini usijidanganye kuwa kuna kitu kinaitwa Chadema yenu.

Usiingize siasa kwenye biashara za watu...

hujawahi kuwa na akili hata siku moja tangu ulipoacha kuvarishwa Nepi kuna chama kilidondoka toka mbinguni Tanu ilianzishwa na watu akina Sykeys Mtemvu RUpia, Akida akina Mbowe Marealle wote hao walitoa pesa zao kujenga chama acha ujinga wewe
 
Kaka yako wakuzaliwa na wewe ni mwanachadema halfu unakauka wewe si mdogo wake nguli la habari nchini au unajigeuza makengeza

Wewe na mama yako ndio iliyowatoa munajulikana nchi nzima acha ujinga
Posts Zako hizi sijui kama umeshirikisha vema ubongo wako. Wewe umekalia kushambulia watu tu badala ya kutafakari walichoandika
 
Back
Top Bottom