Mchaka Mchaka
JF-Expert Member
- Jul 20, 2010
- 4,516
- 1,404
Nilipata kumwona Zitto kwenye kipindi cha jambo Tanzania akielezea hoja yake hiyo. Aliielezea vizuri, akaonyesha ni vipi mapato ya fedha za kigeni yaongezeka sana kutokana na mauzo ya mazao ya mkonge. Nakumbuka to have said that " the world is now turning to organic products". Akatoa hata data ya deficity ya katani katika world market maana kwa sasa ni Brazil inayozalisha mkonge ila haina ardhi ya kutosha! Akaeleza magari yote ya kifahari duniani kwa sasa yanavyohitaji mazuria natural rather than artificial. Kwa hiyo soko lipo kama tutawekeza kidogo tu katika mkonge. Kama hoja hii imetupwa HATUNA BUNGE!!
Upo sahihi. Tukianza na hoja ya Zitto. Mkonge kwa miaka mingi sana ulikuwa utatupatia Tanzania karibia 60% ya mapato ya fedha za kigeni wakati wa nyerere. Tanzania ilikuwa one of the top producers wa zao hili, kama sio number one in the world. Zao hili lilikuja kudondoka baada ya introduction ya synthetic fibre kwenye soko la dunia, ambayo ikawa a substitute to sisal based products kwa haraka sana mwisho wa miaka ya 70 hadi mwanzoni mwa 80; Lakini zao hili limeanza kuwa na soko zuri sana, hasa kutokana na mahitaji yake kwenye uzalishaji katika new industrialized countries kama China na kwingineko. Hivi sasa Brazil ndio number one producer, na hii ni nchi ya kumi kwa utajiri duniani in terms of GDP.
Sasa kama nchi kubwa kama Brazil wanaweka mkazo kwenye mkonge, kwanini isiwe sisi ambao tuna uwezo kabisa wa kuwa hata number moja kwa uzalishaji duniani? Pia Kilimo cha mkonge kikiendeshwa kwa ufanisi, kina uwezo wa kutuzalishia umeme ulio sawa na ule wa Richmond au IPTL i.e 100 MW; kinachohitajika kufanikisa hili la umeme wa 100 MW ni kutumia tu mabaki ya mkonge, ambayo hivi sasa yanatupwa tu porini. Hivyo, mkonge unaweza kuokoa nchi hii kiuchumi kwa kutupatia mapato ya kigeni, kutoa ajira kwa vijana huko vijijini na pia kutuzalishia umeme.
Hoja ya January pia ni muhimu sana kwani inalenga uanzishwaji wa Mamlaka ya kudhibiti Makazi na Ujenzi, kwani hivi sasa ujenzi huo unaenda kiholela holela, na hausaidii pato lolote la maana kwa taifa. Tanzania ni moja ya majiji yanayokuwa kwa kasi sana afrika in terms of real estate, na sekt ahii ina mchango mkubwa sana kwa GDP kutokana na ujenzi unaondelea kwenye kila kona ya majiji makuu ya Tanzania, lakini ukuaji wa sekta hii hauendi sambamba na ongezeo la mapato ya serikali kupitia kodi ya majengo/makazi, esp property tax. Kwa mfano, kama Dubai, na kwingineko, michango wa Real Estate kwenye GDP ni mkubwa sana kwa sababu ya udhibiti wa sekta hii. Nchi kwetu vilevile kuna tatizo la nchi kutokuwa na sheria juu ya makazi, hasa inayomlinda mpangaji dhidi ya mwenye nyuma; Hii ni mbaya hasa kwa kuzingatia kwamba katika mahitaji muhimu ya binadamu, makazi ni moja wapo kwani mahitaji ya msingi ya binadamu ni food, clothing and shelter/nyumba, chakula na malazi.
Hoja zote mbili za waheshimiwa hawa ilitakiwa ziungwe mikono na miguu, lakini kuanguka kwake ni dhahiri kwamba bunge letu halipo kwa ajili ya maslahi ya watanzania, bali maslahi binafsi ya wahusika.
Hivi kama zitto kaweka hoja mezani lazima alikua na point za kuitetea hoja.... je wamempa nafasi ya kuitetea hoja?
Na je hao waliopinga wana sababu gani kupinga.. tukiyajua hayo tunaweza kujadili vizuri
Leo, hoja ya Zitto kuhusu mkakati maalum wa kufufua zao la mkonge na ile ya January kuhusu umuhimu kulinda wapangaji zinawasilishwa bungeni. Je zitapita? Kwa mtazamo wangu, kuna uwezekano mkubwa kwamba, pamoja na umuhimu wa hoja hizi mbili, hoja hizi zitakwama, sababu kubwa ikiwa ni hasira ya wabunge juu ya msimamo wa Zitto na January kupinga ongezeko la posho.
Kama kawaida yako mchambuzi umezichambua hoja hizi mbili kwa ufupi na umahiri mkubwa, mkazo wangu ukiwa maeneo niliyoweka rangi nyekundu.
Suala la mkonge likiwa ni eneo mojawapo tu linaloweza kutuondoa kwenye janga hili la umaskini na kuwa tegemezi wa kuomba omba misaada kwa wazungu (nasema kwa uchungu mkubwa) achilia mbali madini, utalii, uvuvi na utajiri mwingine wote ambao nchi hii inao lakini inakosa usimamizi mzuri na kuliwa na mafisadi wachache.
Angalia nchi ilivyo na matatizo makubwa mfano umeme, angalia wizara ya nishati na madini inavyogubikwa na tuhuma kibao za ubadhirifu wa trillions of money.
Angalia nchi inavyokumbwa na janga la ukosefu wa ajira kwa vijana.... ufumbuzi tunao lakini still Serikali inajifanya kipofu.
Kwanini isijifunze kula na kipofu? kama imeamua kun'gata, basi ingeuma pia kidogo japo kutupunguzia machungu waTanzania!
Kwanini kila siku tushike nafasi za juu kwenye umasikini na kuwa ombaomba wakati tunazo opportunities za kuweka good records kama vile wazalishaji wakuu wa mkonge duniani?
Angalau Kidogo January yeye alipata nafasi ya kuzungumza baada ya Waziri Tibaijuka kujibu hoja yake. January kikubwa aliomba Spika awaachie wabunge wengine watoa mchango na Spika Makinda akakubali na ndipo Ole Sendeka na Mbowe wakapewa fursa hiyo na kimsingi, kukubaliana na January. Lakini tofauti na January, kilichofanyika juu ya hoja ya Zitto ni udikteta uliotukuta wa Spika Makinda, kwani tofauti na january ambae alipewa dakika kadhaa kujibu mapigo ya Waziri Wa ardhi na pia kukubaliwa ombi lake la kuwapa wabunge nafasi ya kutoa michango yao, kwa upande wa Zitto, yeye hakupewa nafasi kujibu mapigo ya Waziri wa Kilimo na wala hakuna mbunge yeyote aliyepewa nafasi kufanya hivyo mbali ya Halima Mdee ambae aliomba mwongozo wa Spika na kupewa nafasi hiyo lakini huku akiingiliwa ovyo na Spika. Kina Lissu na wengine hawakufanikiwa katika jitiada za kuiokoa hoj ahii kwani miongozo yao ilizibiwa masikio na Makinda. Hoja ya Halima Mdee ambayo ili base kwenye kanuni, ingeweza kuokoa hoja ya Zitto iwapo Makinda angeacha kuikinga serikali katika hoja ile.
Hivi kama zitto kaweka hoja mezani lazima alikua na point za kuitetea hoja.... je wamempa nafasi ya kuitetea hoja?
Na je hao waliopinga wana sababu gani kupinga.. tukiyajua hayo tunaweza kujadili vizuri
Angalau Kidogo January yeye alipata nafasi ya kuzungumza baada ya Waziri Tibaijuka kujibu hoja yake. January kikubwa aliomba Spika awaachie wabunge wengine watoa mchango na Spika Makinda akakubali na ndipo Ole Sendeka na Mbowe wakapewa fursa hiyo na kimsingi, kukubaliana na January. Lakini tofauti na January, kilichofanyika juu ya hoja ya Zitto ni udikteta uliotukuta wa Spika Makinda, kwani tofauti na january ambae alipewa dakika kadhaa kujibu mapigo ya Waziri Wa ardhi na pia kukubaliwa ombi lake la kuwapa wabunge nafasi ya kutoa michango yao, kwa upande wa Zitto, yeye hakupewa nafasi kujibu mapigo ya Waziri wa Kilimo na wala hakuna mbunge yeyote aliyepewa nafasi kufanya hivyo mbali ya Halima Mdee ambae aliomba mwongozo wa Spika na kupewa nafasi hiyo lakini huku akiingiliwa ovyo na Spika. Kina Lissu na wengine hawakufanikiwa katika jitiada za kuiokoa hoj ahii kwani miongozo yao ilizibiwa masikio na Makinda. Hoja ya Halima Mdee ambayo ili base kwenye kanuni, ingeweza kuokoa hoja ya Zitto iwapo Makinda angeacha kuikinga serikali katika hoja ile.
Hilo nalo neno?!!! Hii ni kutokana na ubinafsi, umbumbu na ushabiki wa wabunge wa CCMLeo, hoja ya Zitto kuhusu mkakati maalum wa kufufua zao la mkonge na ile ya January kuhusu umuhimu kulinda wapangaji zinawasilishwa bungeni. Je zitapita? Kwa mtazamo wangu, kuna uwezekano mkubwa kwamba, pamoja na umuhimu wa hoja hizi mbili, hoja hizi zitakwama, sababu kubwa ikiwa ni hasira ya wabunge juu ya msimamo wa Zitto na January kupinga ongezeko la posho.
Niliisikia hoja binafsi ya Mhe Zitto lakini skupata fursa ya kuisikia ya Mhe Makamba. Mhe Zitto alitoa data nyingi sana za kuthibitisha hoja yake laikini alipochemsha ni kutaka Bunge lipitishe azimio kuwa Serikali iufanye mwaka 2012 uwe mwaka wa kupanda mkonge. Azimio hili lilitosha kuondoa mantiki nzima ya hoja yake a mbunge aliyomba kurekebisha hoja hii japo niliweza kubaini hakuwa msomi kama Mhe Zitto aliweza kumgaragaza kikweli kweli kwa kuwa haiwezekani kwa mtu msomiambaye tayari amekwish kuonyesha ni uwekezaji kiasi gani unahitajika ili Tanzania iweze kurejesha hadhi yake katia akilimo cha mkonge aweze kupendekeza kupitishwa kwa azimio kuwa mwaka 2012 uwe mwaka wa kupanda mkonge ilihali hivi sasa tupo Februari 2012.
Kwa maoni yangu Mhe Zitto kwa kutumia kiburi cha usomi alitaka kulitrumia bunge kujipatia umaarufu katika kupendekeza kitu kisichowezekana.
acha longo longo picha ya kamanda hiyo
Wadau kumbukeni mashamba yote ya mkonge yalishauzwa wa wawekezaji uchwara ambao wameshindwa kuyaendeleza. Na wengine ni viongozi ndani ya serikali. Hoja hii ingepita, ingeibua madhambi mengine yaliyojificha kwenye sekta ya kilimo cha mkonge.
Lakini hoja kutokupitiswa leo, si kifo cha wazo hilo za Zitto Kabwe. Kama kweli kuna potential ecomonic benefits kwa nchi, zinaweza kuvunwa hata bila ya kupitishwa na hoja ya wabunge waoasinzia Bungeni na kugonga gonga meza bila hata kujua walitendalo.
Naelewa hoja yako lakini kikubwa hapa ni kwamba tunaelekea bajeti ya 2012-2013, mimi nadhani Zitto angeitumia bajeti ijayo itakayowasilishwa bungeni mwezi June, kama reference wakati wote wa kujenga hoja yake, na hii ingeipa hoja yake nguvu kubwa zaidi - kwa kusema kwamba kutokana na umuhimu wa zao hili....ni matarajio yangu kwamba kuanzia bajeti ya mwaka huu wa fedha, wizara ya kilimo itafanya haya haya na haya kuhusu zao la mkonge;
Iwapo zitto angefanya hayo kwa kulink na bajeti ijayo, waziri angeingia tu mtego wa kutoa ahadi kemkem kwamba watafanya hili na lile kwenye bajeti, then zitto kumsibiria na bajeti yake na kuanza nae upya.