Hoja Binafsi za Zitto na January:Je, Wabunge watalipa visasi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Leo, hoja ya Zitto kuhusu mkakati maalum wa kufufua zao la mkonge na ile ya January kuhusu umuhimu kulinda wapangaji zinawasilishwa bungeni. Je zitapita? Kwa mtazamo wangu, kuna uwezekano mkubwa kwamba, pamoja na umuhimu wa hoja hizi mbili, hoja hizi zitakwama, sababu kubwa ikiwa ni hasira ya wabunge juu ya msimamo wa Zitto na January kupinga ongezeko la posho.
 
Mh Zitto ametoa hoja binafsi nzuri sana kuhusu zao la mkonge.

Alidhamiria zao hilo litumike kuondoa umaskini Tz. Cha ajabu wabunge wa ccm wameikataa.

Hao ndio wanataka posho zaidi huku wakiwa hawana tija kabisa
 
Mi nilitegeme hilo tu hawa magamba wamelogwa na kibaya zaidi aliyewaloga alishakufa hivyo kifo nao kinawasubiri 2015
 
Wabunge wa CCM wanaongozwa na ilani ya chama chao ambayo haiwezi kumletea mtanzania maendeleo na kumtoa mwananchi kwenye lindi la umaskini.
 
Mh Zitto ametoa hoja binafsi nzuri sana kuhusu zao la mkonge.

Alidhamiria zao hilo litumike kuondoa umaskini Tz. Cha ajabu wabunge wa ccm wameikataa.

Hao ndio wanataka posho zaidi huku wakiwa hawana tija kabisa

Mkuu hoja ilikuwaje? Mkonge ungeondoaje umasikini Tanzania? Kama unayo hiyo hoja imwage hapa tuione tafadhali.
 
Huu ni zaidi ya umbumbumbu, hawa wabunge wa CCM mambo ya kuweka maslahi ya chama mbele kuliko maendeleo ya nchi yatazidi kudidimiza nchi hii.
Yani mbunge wa Tanga ni wa kupinga hoja ya mkonge kweli kweli? kama wao hawakuwa na akili ya kutoa mapendekezo hayo siku zote na sasa wanaona aibu CHADEMA itapata umaarufu Tanga ni matatizo yao wenyewe na mawazo mgando yao wasiotaka kushughulisha vichwa vyao wasitake kutukwamisha maendelea ya nchi.
Nawaasa hawa wabunge wa CCM wakiendelea hivi ndio wanazidisha hamu ya kuwaondoa madarakani
 
Hakika binafsi nimefurahishwa sana na hoja za hawa wabunge vijana....hususani hoja ya J.Makamba inayotetea haki za wapangaji.
Yaani hiyo hoja imenigusa sana....maana wenyenyumba wa Bongo wakilala na wakiamka asubuhi wanakupandishia kodi tu
from no where.
 
Mh Zitto ametoa hoja binafsi nzuri sana kuhusu zao la mkonge.

Alidhamiria zao hilo litumike kuondoa umaskini Tz. Cha ajabu wabunge wa ccm wameikataa.

Hao ndio wanataka posho zaidi huku wakiwa hawana tija kabisa

Kwa nini usimshauri kuwa badala ya kuipeleka bungeni hiyo hoja ambayo imetoka kwa jamaa zake akina Dr Idris Rashid na Dr. Dau angewaambia wakaongee na JK tu mambo yangekwisha.
 
Mh Zitto ametoa hoja binafsi nzuri sana kuhusu zao la mkonge.

Alidhamiria zao hilo litumike kuondoa umaskini Tz. Cha ajabu wabunge wa ccm wameikataa.

Hao ndio wanataka posho zaidi huku wakiwa hawana tija kabisa

wabunge wa ccm wananisikitisha sana. Wanapinga hata mambo ya maendeleo ya wananchi tena mbnge wa korogwe ndo anashabikia kabisa.
 
Kweli hawa jamaha ni vilaza kuliko wabunge wa bunge lolote lile duniani!hoja ya zitto ilikua na maslahi sana na taifa,wao wanachojua ni kusema ndioo!wabunge gani hawa wasioweza fanya research hata kidogo?wao ni kulala na ndio tu?wanasikitisha sana,hata makinda uwezo wake ni mdogo sana,leo amezidi kudhihirisha ilo!ndio tatizo la kua kwy kiti kwa matakwa ya wachache
 
UKILA NA KIPOFU........................... zitto we ilete hiyo mipango yako kwenye bunge huru la Watanzania uone! mi siamini kupitia wabunge hasa wa CCM. MIBUNGE YA CCM NI JANGA LA TAIFA
 
Kama kuna Mbunge kutoka Tanga aliyepinga hili MUNGU AMSAMEHE KWA KUWA HALIJUI ATENDALO!
 
Naomba mniwie radhi kwa makosa kisodo kwenye kichwa cha thread: ilitakiwa isome hivi: Hoja Binafsi za Zitto na January:Je, Wabunge watalipa visasi

Leo, hoja ya Zitto kuhusu mkakati maalum wa kufufua zao la mkonge na ile ya January kuhusu umuhimu kulinda wapangaji zinawasilishwa bungeni. Je zitapita? Kwa mtazamo wangu, kuna uwezekano mkubwa kwamba, pamoja na umuhimu wa hoja hizi mbili, hoja hizi zitakwama, sababu kubwa ikiwa ni hasira ya wabunge juu ya msimamo wa Zitto na January kupinga ongezeko la posho.
Kwa kuongezea tu, wanaona hawa vijana wawili wanajipatia umaarufu kwa kasi, kwahiyo lazima wawakwamishe.
 
Wamesema Serikali imeshaunda Tume ambayo inaangalia matatizo yanayoukabili uzalishaji wa Zao la Mkonge nchini na Tume hiyo iliundwa baada ya katika moja ya mikutano iliyopita ya Bunge Mheshimiwa Ngonyani (Profesa Maji marefu) kuihoji Serikali kuhusiana na kudorora kwa zao la Mkonge...eti sasa wanasubiri majibu ya tume hiyo ili waone shida iko wapi juu ya uzalishaji wa Mkonge....na kutoka hapo sasa hata hOJA BINAFSI YA MHESHIMIWA ZITTO KABWE inaweza kujadilika bungeni tofauti na sasa.
 
Kwa mawazo wa kiitikadi, hatutafika!!! Hoja hii ilikuwa na mshiko na maazimio mema kwa ardhi iliokuwa pori kuedelezwa, ajira kwa vijana, na kuongeza mapato ya nchi. Hoja ya Zito ilishafahamika, na jamaa hawa wakajikita kwenye kuupinga. hawa ni wapinga maendeleo kwa hakikia. kwa watz makini walio nje ya bunge wanajua wajibu wao kuwahukumu hawa.
 
hii generation mpya ya wabunge inaonyesha mwelekeo mzuri katika ku-address issues za kitaifa... big up, kazeni buti and don't entertain parochial partisan politics
 
hoja ya makamba ni contradicting, wote twajua gharama za ujenzi zilivyo juu, na watu wengi hukopa ili kujenga, leo hii utamwambia nin mtu huyu eti kodi ni ya miezi 2 tu maximum...
 
Back
Top Bottom