HLRC kuiburuza serikali mahakamani kuhusu NSSF

Mnajua maana ya Social Security?
Tuelezee rafiki vizuri. kwa nchi za wengine nadhani ina include kutunzwa ukikwa mzee lakini pia ukiwa huna kazi kuna unemployment benefit, sasa hapa kwetu inaaply, au security uzeeni wakati sisi tunaofanya kwa mikataba kibarua kikiota majani ntakufa njaa au kwa frustration kama sijapata kibarua kingine? kwa sababu hakuna mipango ya kuwajali watu watu wakiwa hawana kazi, ndio maana mtu anachukua chake ili anendeshe maisha yake wakati anatafuta. ili aweze hata kulipa kodi ya nyumba.
 
MNYONGE MNYONGENI, HAKI YAKE MPENI. . . ni vile tu naiogopa ban la sivyo ningewatus hawa mafisadi mpaka server ingekuwa slow. angalia PAYE walivyoipandisha, haitosh na NSSF & PPF zetu pia watupangie muda wa kuzichukua jaman jaman jaman tumechoka kunyanyasika.

Hapo bado unaambiwa uwe mzalendo kwa kuipenda nchi yako. ukisoma nje ya nchi unaambiwa urudi kuitumikia nchi yako. wallah kwa style hii ngoja tu nifanye mchakato wa kwenda kufanya kaz nje ya nchi.

Nikifikisha 55yrs ntarud kuchukua vijisent vyangu!


Eti PAYE wamepunguza 5000 rubish
kweli mtu unaweza kujikuta umeongea na yasiyosemwa
 
Wavunje mkataba wa awali, watulipe chetu ndo watuombe tujiunge upya.

CDM watoe tamko wao wakiingia madarakani watatusaidiaje kwenye hili sheria dhalimu tuwape kura?
 
Nasikia sheria yenyewe imepitishwa mwezi april mwaka huu.Je wabunge wetu walipata nafasi ya kuijadili?
Kama ilipitia kwao tunatakiwa tuwa bane.Hii ni sheria kandamizi.

Umri wa kuishi wa mtanzania haufikii miaka 55-60
Ajira zenyewe ni za kubatatisha.
Kwa mfano kampuni imefungwa mfanyakazi una miaka let say 40.Unaambiwa usubiri mpaka miaka 55.Je watoto watosoma na nini? utakula nini? Huu ni wizi.Lengo la NSSF inatakiwa ikusaidie wakati huna kazi.

Kama issue ni uzeeni mbona wazee wengi wako mtaani hawana hiyo pensheni na wanaishi.mfano Wasfaafu wa EA.

Je kama ni kumsaidia mstaafu ni watanzania wangapi wameajiriwa?
Wale ambao hawana ajira mbona serikali iko kimya? Nanai anawasaidia wakizeeka?
Huu ni wizi wa mchana huwezi kukaa na pesa ya mtu bila ya ridhaa yake.

Wakati wa Sabasaba niwaliuliza maofisa wa NSSF kuhusu hii sheria, walichonijibu eti inatumika pote duniani.
USHAURI WANGU KWA SERIKALI
1.Sio kila kitu kinachofanywa na nchi za wenzetu kinatufaa na sisi lazima tuangalie na mazingira kama (UMRI WA KUISHO,UPATIKANAJI WA AJIRA,HUDUMA ZA JAMII KAMA ELIMU NA AFYA nk)

2.Tulipoambiwa tubinafisishe mashirika ya umma tukakubali hata yale muhimu leo tuna juta.

VYOMBA VYA HABARI VITUSAIDIE KUIPIGIA HII SHERIA KANDAMIZI YA WANYOGE.
KAMA WAMETUMIA OVYO MICHANGO YA WANACHAMA WAFILISIWE.
 
1. Wakulima wanahusikaje?
2. a)Mtaji wa biashara kivipi? ...huo si mtaji au savings account.
b)Mungu yupi? Kwani nani kasema mungu ndiye anayeua?

3)Tatizo ni retirment age au mfumo wa mfuko?
Acha kulalamika. Chacharika.

Hujaeleweka kabisa sijui umesimamia wapi?
 
serikali nyonyaji,inawaacha wageni wakiendelea kuneemeka huku ikiwanyonya wananchi wake kwa makusudi.
 
moderator unaweza kuziunganisha hizi threads maana maudhui yanafanana. Kuwa mtanzania sasa inakuwa ni kazi ya ziada!
Kuna tetesi kwamba serikali imetoa agizo leo mifuko yote ya hifadhi ya jamii kuacha kutoa mafao ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi wote watakao acha au kufukuzwa kazi kabla ya muda wa kustaafu kufika kuanzia leo.Taarifa hii imetolewa na meneja wa NSSF Mkoa wa Mara,Ndg MVUNGI pamoja na HR meneja wa barrick north mara leo wakati wanatoa ufafanuzi juu ya mambo yanayohusu sheria mpya ya mifuko ya hifadhi ya jamii.MWENYE TAARIFA KAMILI ATUJUZE
https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/295445-serikali-imetoa-agizo-leo-la-kusimamisha-withdraw-kwa-wanachama-wote-wa-hifadhi-za-jamii.html
 
Wafanyakazi Tanzania nzima tunatakiwa kufanya mgomo juu ya hili...
Kila sehemu wanatunyonya bado wanaona haitoshi
 
Ingekua Kenya, sa ivi tayari wangeshakua barabarani na matawi.

Sisi tunatishiwa eti tuitunze amani, hakuna maandamano.

Kuna kipindi cha kipumbavu TBC kinachoongelea amani cha kuwapumbaza watz.

Nchi ya kibwege sana hii.
 
DAWA NI KUCHAGUA CHAMA KINGINE CHA SIASA, chenye ahadi ya mtu kuchukua mafao muda wowote atakao yeye.


I agree with you 100%

Chama kitakachokuja na sera ya

1. Uhuru wa kuhama/kujitoa nakujiunga na mfuko ambao mwanachama anaminin ni bora kwake.

2. Kuchukua mafao yetu tunapoachishwa kazi iwe ni kwa maamuzi yetu kulingana na matatizo ya mtu.
 
Mnajua maana ya Social Security?

Mkuu nahisi wewe hujui bali unajifanya kujua. Si kila mfanyakazi anataka hayo mafao yako ya uzeeni. Kumbuka pia, shilingi moja ya leo haina thamani sawa na shilingi moja ya kesho! Jiulize, au fanya utafiti, nchi nyingine wame-approach vipi hii kitu. Sheria ya SSRA imekuja kwa sababu serikali dhaifu inategemea sana kukopa pesa kule na kurudisha inakuwa ngumu. Tafuta mtu wa Acturial akufanyie analysis ndo utajua kuwa hii itakuwa kama Desi tu wasipojipanga vizuri!
 
Wafanyakazi Tanzania nzima tunatakiwa kufanya mgomo juu ya hili...
Kila sehemu wanatunyonya bado wanaona haitoshi
Ninakuunga mkono kabisa my FirstLady1 wangu. Mgomo nchi nzima katika sekta zote, za umma na binafsi ndio suluhisho pekee. Ninashauri tu kuwe na minimum service, let's say 15-20% of the labour force of the sector concerned.
 
Last edited by a moderator:
Hao HLRC na nyie wooote mtakaoenda mahamakamani ndio mtakuwa mmefunga rasmi huu mjadala.( au mmesahau msamiati wa cku hzi?). Hahaah, joking.

Ukweli ULIO WAZI ni kwamba, kwenye hii kesi lazima HLRC waangukie pua. Hivi mnajua hilo fao la withdrawal halipo katika sheria yoyote ya PPF au NSSF?. Mlizoeshwa kulambishwa sukari,mkaona raha kumbe mnafadhiliwa!

Mtazoea tu..na hakuna maandamano hapo..NANI kakuambia mtanzania anayekaa ofisini au aliyeko kwa kazi ya Boss anaandamanaga?. Mtapiga kelele nyuma ya keyboard na maofisini kwenu kisha UPEPO utapita.lol!

I support fully operaationalizaon of Pension system in tz, SSRA Wamechelewa sana.

Lazima utakuwa ulikimbia bongo kwa kusosa ajira because shule ni ndogo na sasa upo UK au US unabeba box.
 
Hii mifuko inatoa mafao mbalimbali mojawapo likiwa fao la kujitoa ambalo ndilo linalolalamikiwa. katka hili, mwanachama anaruhusiwa kuchukua michango yake aliyochangia wakati wote wa uanachama wake. Hii dhana inatokana na dhana nzima ya hifadhi (social security) mfanya mtu aweze kumudu maisha kipindi ambacho anakuwa hana ajira au kipato; hivyo kufuta fao hili sio sahihi hata kidogo
 
Life expectancy at birth: total population: 52.85 years
male: 51.34 years
female: 54.42 years (2011 est.)
Definition: This entry contains the average number of years to be lived by a group of people born in the same year, if mortality at each age remains constant in the future. The entry includes total population as well as the male and female components. Life expectancy at birth is also a measure of overall quality of life in a country and summarizes the mortality at all ages. It can also be thought of as indicating the potential return on investment in human capital and is necessary for the calculation of various actuarial measures.
Source: CIA World Factbook - Unless otherwise noted, information in this page is accurate as of January 9, 2012
 
Mtoa tamko hilo ametukosea sana sisi wenye fedha zetu, hawezi kutupangia muda wa kuchukua kile ninachochanga eti mpaka miaka aliyoota usingizini.
Kama anataka yeye kuendelea kukopa hiyo hela sawa lakini ingekuwa VYEMA kutuhusisha sisi wanachama wa mifuko hii ya kijamii ili tukubaliane namna ya kutunza mapesa yetu huko.
Vinginevyo tutawaambia waajiri wetu wasitushe makato mpaka ufumbuzi upatikane. Nawashukuru LHRC kwa hatua yao hiyo mimi nipo tayari kwenda nao mahakamani ili wafute hiyo sheria kandamizi.
 
ukiwa 65yrs old, na umeshakula mafao yako unakuwa mzigo kwa private sector au jamii?

Due to theincreasing population of elderly there’s a need of designing long term pensionpolicy. Mostly these are the pension schemes that will cover both formal andinformal schemes. The pensionplan will be the largest scheme of insurance in Tanzania. Its primary role isto replace a portion of the earned income of contributors who cannot work atcertain age usually above 60 years. Reaching lowlevels of inactivity among older workers and promoting longer working lives arekey factors to alleviate the negative impact of population ageing on employmentand economic growth (European Commission-Tanzania 2009 Aging report). The 2001report stressed the importance of reforms encouraging higher employment andparticipation rates, especially among women and the elderly; it emphasized thatpension reforms are needed to ensure both the long-term financialsustainability and a certain degree of intergenerational fairness. Inresponse to pressures stemming from ageing populations and persisting lowparticipation rates, Tanzania have reformed its pension systems. These reformscomprise a number of different measures that are meant to keep the sustainabilityof public finances mainly by transferring part of the demographic risk from thestate to individuals and by giving strong incentives for working longer.
 
Jamani Mwenye number ya HLRC Tafadhali ninaomba anitumie, We need to support HLRC no mater what, Mimi nimepanga niache kazi next year then nichukue hela yangu ya NSSF nikalime, sasa mungu wangu mipango yangu yote imeishia kapuni.

Kwa kweli Kama Mbunge wako ame support this kweli hatakiwi kabisa kuwa mbunge wako.

Naomba mwenye ANSARD YA BUNGE ambayo imepitisha this tujue wabunge gani wamepitisha then tuanze kuwa andalia zengwe.
samahani kwa atakayekwazwa na hii picha bali mimi nimeitumia tu kama kielelezo kimojawapo cha bunge letu lilivyo katika enzi hii. Hawa watu wanaweza kuwa wamefikia hii hali sababu ya bunge letu linavyoendeshwa na matokeo yeke ndio haya ya kupitishwa sheria za kishetani kama hii ya mafao.
Picha hii iko kwenye gazeti la Mwananchi la leo.
mbunge.jpg
Katika nchi hii kuna mambo ya ajabu sana, na hili ni mojawapo. Wafanyakazi katika sheria hii mpya wana mambo muhimu ya kujiuliza:

Upitishwaji wa Sheria Hii Mpya
Sheria zote zinazopelekwa bungeni ikiwa pamoja na marekebisho yake, wadau hupewa na nafasi ya kuzijadili na kutoa maoni yao kabla ya kujadiliwa bungeni. Kwa nini mabadiliko ya sheria hayakujadiliwa, yakapitishwa kinyemela bila ya kupata maoni ya wenye mifuko yao? Wamiliki wa mifuko hii ni wafanyakazi, wala si serikali maana serikali haichangii chochote katika mifuko hii.
Je, wanajamvi hamuoni kuwa hii thread nyingine hapa chini ndio inaweza kuwa chanzo cha huu ushetani wote!!!???
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/296767-sheria-mpya-ya-mafao-haiwagusi-wabunge-na-viongozi-wengine-wakubwa.html
Wana JF,Nimedokezwa kuwa sheria mpya ya mafao ina kifungu cha 43 (6) ambacho kinasomeka kama ifuatavyo:
''This act shall apply to a person or employee employed in the formal or informal or self-employed in the mainland Tanzania and shall not apply to a person who has been insured or registered under any other law.''
Alichonieleza mdokezaji wangu ni kwamba kifungu hiki kinawaondoa wabunge na viongozi wengine wa juu katika ile kadhia ya kusubiri hadi miaka 55 au 60. Kwa maana hiyo, wabunge kwa mfano, wakishamaliza ile miaka 5 watachukua pesa zao kama kawaida.
Kuna mwenye kujua zaidi juu ya hili?
 
Back
Top Bottom