lukindo
JF-Expert Member
- Mar 20, 2010
- 8,466
- 9,028
Naomba pia kujulishwa juu ya hili:Hapa umesema mkuu. Social security ni bomu linalosubiri kupasuka. Katika mazingira haya mifuko hii haimweki mwanachama mbele hata kidogo. Fikiria umechangia kwa miaka 10 baada tu ya kumaliza chuo ukiwa na miaka 24 baadae ukaamua kuacha kazi ili ufanye kazi zako zingine, je ni akili kweli kusubiri pesa yako miaka 26 baadae. Huu ni uporaji wa mchana. Ni muhimu watu tufanye utafiti wa kutosha juu ya ufanisi wa mifuko hii katika nchi zingine na kulinganisha na hali halisi ya maisha na mfumo wa jamii ya Kitanzania. Vinginevyo copy and paste itatuletea majanga mengi siku za usoni.
Hivi hizi pesa zinawekwa kwenye basis of interest earning au unazoweka ndizo hizo hizo unazorudishiwa baada ya hiyo miaka 60???
Hapa namaanisha kuwa ukinunua shares Presisionair, CRDB, Twiga Cement, TOL nk, wakipata faida kunakuwa na gawio lakini nasikia kila siku hii mifuko ina-inflate faida ila sijawahi kusikia wanachama wakipewa japo 10% ya faida hiyo!