HLRC kuiburuza serikali mahakamani kuhusu NSSF

kumbe we kobello una mtindio....huwezi kuwa sawa...
Mkuu huo ndiyo ukweli wenyewe, sounds crazy but kila government funds kama hizi ndiyo moja ya mchango wa wafanyakazi kwenye bajeti zao. Real talk wala sina nia ya kumuudhi mtu.
 
For sure nichanganyikiwa kwanza ndio nina miaka 26 nilikuwa nategemea NSSF yangu inisaidie nirudi shule sasa ndoto zangu zote zimevulugika nafuu kuingia vitani kuliko kuvumilia manyanyaso haya.
Sheria hii ni ya kinyama na ni ugaidi wa wazi kwa wafanyakazi wa Tanzania.
 
Wafanyakazi wajue maana ya Social Security au wasijue is irrelevant. Jambo la muhimu ni kuwa hela hiyo ni michango ya wafanyakazi. Namna gani itawasaidia, wao ndiyo wanaojua, na serikali haina haki yeyote kuifanya hela ya wafanyakazi kuwa mfuko wa kutekelezea miradi ya maendeleo. No way. Nadhani serikalini bado kuna watu ambao wapo kwenye usingizi mnono wa kukosa fikra, wakifanya kazi ya ku-copy mambo machache kutoka mataifa mengine bila ya kujifunza na kutambua mambo hayo yatafanya kazi vipi katika mazingira yao.

Wewe katika nchi yako, watu wenye ajira rasmi hawafikii hata 10% halafu unasema mfanyakazi asipate mafao mpaka afikishe umri wa miaka 60, wewe una akili au tahira? Nchi ambayo mfumko wa bei ni zaidi ya 20% halafu umwambie mfanyakazi aliyeachishwa kazi akiwa na umri 30, halafu eti asubiri kwenda kuchukua mafao yake mpaka baada ya miaka 30, kweli anayefikiria hivyo ana akili au ni kichaa?

Hapa umesema mkuu. Social security ni bomu linalosubiri kupasuka. Katika mazingira haya mifuko hii haimweki mwanachama mbele hata kidogo. Fikiria umechangia kwa miaka 10 baada tu ya kumaliza chuo ukiwa na miaka 24 baadae ukaamua kuacha kazi ili ufanye kazi zako zingine, je ni akili kweli kusubiri pesa yako miaka 26 baadae. Huu ni uporaji wa mchana. Ni muhimu watu tufanye utafiti wa kutosha juu ya ufanisi wa mifuko hii katika nchi zingine na kulinganisha na hali halisi ya maisha na mfumo wa jamii ya Kitanzania. Vinginevyo copy and paste itatuletea majanga mengi siku za usoni.
 
Mzigo kivipi? Inaonekana wewe ni moja ya wale wanaokuwa fedha zetu. Kuna wazee wangapi ambao serikali haijihusishi kwa sasa? Unataka kuniambia miaka hiyo ndo mtaanza kuwasaidia siyo? Nimekuona uchangiaji wako. Unakera, na kama unafaidika kwa wizi huu unaofanywa na mafisadi au wewe ni fisadi basi nyamaza. Unaringia pumzi ambayo umepewa na Mungu na naweza kumwomba Mungu akufunge pumzi wakati wowote.
 
Nijuavyo mimi huwezi ku retire kazi ukataka kuchukua fedha yako NSSF unapopenda. Kuna mashatri ya Umri wako na miaka ulolitumikia..Kama mfanyakazi haja qualify ktk makundi haya tuseme unaaxcha kazi ukiwa na umri wa miaka 45 na hujalitumikia taifa kwa miaka inayotakiwa - Huwezi kuchukua hata kama ukienda mahakama gani. Muhimu sana tuelewe vifungu vya sheria za NSSF kabla hatujaunga mkono maana unapojaza makaratasi na kujiunga kuna vipengele ambavyo watu wengi sana huwa hawavisomi..
Ebu pitieni site hii muone mfano.. Bofya
Hiyo link sio sahihi. Ni ya watumishi wa serikali ambao kwa hapa Tanzania wapo chini ya GEPF. Kuna tofauti kubwa sana kati ya Pension fund and provident fund. Kwa wenzetu hata watumishi wa serikali hawapeleki michango provident kwa vile mafao ni madogo wanapeleka pension scheme maalum ndio maana ina hizo sheria. Kama hufahamu serikali huwa haipeleki michango kwenye pension scheme licha ya makato ila wanalipa kwa fungu la bajeti wakishajua idadi ya watu wanaostaafu mwaka huo.
 
Hebu tujiulize...

Kinachoua hii mifuko ya jamii ni wanachama kuchukua pesa zao kabla ya kustaafu au mifuko hii imegeuzwa shamba la bibi na serikali pamoja na kuwekeza kwenye miradi ya pwagu pwaguzi??
Ripoti ya CAG inajibu vizuri sana swali hili...

Mwanachama anapoajiriwa hapewi nafasi ya kuchagua ajiunge na mfuko gani...Waajiri wengi wameingia makubaliano
exclusive na mfuko mmoja na kulazimisha wafanyakazi kujiunga na mfuko huo mmoja. Ni wachache sana wanatoa option kwa mfanyakazi kuchagua anataka kujiunga wapi. Unapojiunga na mfuko mmoja huruhusiwi kuhama kwenda mfuko mwingine.

Mwanachama hana sauti juu ya pesa yake inawekezwa wapi na yeye kama mwanachama atanufaika vipi. Katika nchi za wenzetu walioendelea mwanachama anapewa nafasi ya kuamua pesa zake ziwekezwe wapi. Hii inasaidia kumpa moyo mwanachama kuona pesa yake anayowekeza inazaa faida na hivyo hatapenda kuiondoa mapema.

Huku kwetu mifuko ya jamii imejiingiza katika miradi mingi isiyo na tija bila kushirikisha wanachama wake wala kuwa na udhibiti wa aina yoyote kutoka SSRA. Mbaya zaidi Serikali yetu nayo imeigeuza mifuko hii kuwa shamba la bibi kwa kujichotea pesa kiholela bila ya kuwa na mpango wa kuzirejesha. Sasa hali imekuwa mbaya wanatafuta kwa kutokea kwa kusingizia mifuko inafilisika sababu ya wanachama wanaochukua mafao yao mapema...Wizi mtupu!! Serikali ina sauti zaidi juu ya pesa hizi kuliko wanachama wenyewe!

Hii hoja wanayotoa kuwa pension za wanachama zitatumika kama dhamana kuwakopesha nyumba haina mshiko kabisa; Kwanza hiyo mikopo ya nyumba lazima itakuwa na masharti...sitegemei mwanachama mwenye akiba ya milioni 1 akopeshwe nyumba ya milioni 10, isitoshe nyumba sio priority ya kila mtu.

Mwisho kabisa Average Life Expectancy ya Mtanzania sasa ni miaka 53 kama sikosei...Hii ina maana kwamba asilimia kubwa ya wanachama watafariki kabla ya kuchukua hayo mafao yao ya uzeeni hivyo kuacha mzigo mkubwa kwa wajane na watoto kufuatilia hayo mafao!!
 
Social security funds si kwa ajili yako, ni kwa ajili ya serikali.... Once you have that in your head, utaona haya malalamiko hayana nguvu kimataifa.

Kwa hiyo Social security kwa maneno mengine ni goverment security? mbona unatuchanganya. Ila inahisu mifuko yote na si NSSF peke pake kama mtoa mada alivyoanzisha
 
Katika hili, vyama vya wafanyakazi viko wapi? Paazeni sauti zenu, ikishindikana itisheni migomo ambayo haitabagua sekta binafsi wala serikali. Ikumbukwe kuwa ufanisi katika sekta binafsi una mchango mkubwa katika mustakabali wa mafanikio serikalini.

TLP (Tanzania Labour Party), hii ni ngazi ya kupandia, tumieni fursa vizuri.
 
Mnajua maana ya Social Security?

Binafsi naijua vizuri na wala haipo Tanzania.....ile ya NSSF ni pension

Social Security is a concept enshrined in Article 22 of the Universal Declaration of Human Rights which states that Everyone, as a member of society, has the right to social security and is entitled to realization, through national effort and international co-operation and in accordance with the organization and resources of each State, of the economic, social and cultural rights indispensable for his dignity and the free development of his personality. In simple term, this means that the signatories agree that society in which a person lives should help them to develop and to make the most of all the advantages (culture, work, social welfare) which are offered to them in the country.


Social Security may also refer to the action programs of government intended to promote the welfare of the population through assistance measures guaranteeing access to sufficient resources for food and shelter and to promote health and wellbeing for the population at large and potentially vulnerable segments such as children, the elderly, the sick and the unemployed.

Source: Webster's Dictionary
 
Katika nchi ya wenzetu kule Kenya wana NSSF lakini utaratibu wao sio huu wa TZ, kwani wao wanakatwa Kshs 200=Tsha 3,600/= na Mwajiri anakatwa the same amount ambayo it is like nothing na huchukui mpaka umri huo wa kustaafu yaani 55 au 60. Kwa hili unaweza ukaangalia amount nyingine yote unalipwa kama mshahara wako.
Inaonekana TZ tumeamua kufuata mfumo ambao hatuujui na huu utaleta matatizo makubwa mie nimejipanga kuacha kazi mwezi ujao na NSSF inanitosha kujiajiri badala ya kuendelea kuwa mtumwa Patachimbika.

Pili hii mifuko ndugu zangu ina ujanja mwingi hebu fikiria kiasi unachoweka 20% kwa miaka yote hiyo na hakuna riba na mafao wanayotangaza ni uongo mtupu, usisahau kuangalia miradi mikubwa waliyonayo where is our dividends??? Wanatumia hela zetu kuekeza halafu we are getting nothing?? Nasema Patachimbika.
 
Kituo cha kutetea haki za binadamu nchini Tanzania kimesema kinaandaa taratibu za kuiburuza serikali mahakamani kwani kumkatalia mwanachama kuchukua hela zake kwa vile hajafikisha miaka 60 ni ukiukwaji wa haki za binadamu.Hii ni kwa sababu hakuna makubaliano yaliyofanyika kati ya mifuko husika na wanachama ili kuleta sheria hii ambayo ni mbaya na haramu hasa kwa wafanyakazi wa sekta binafsi.
HLRC imeomba ushirikano wa wafanyakazi wote kufanikisha azma hii.

Source:Habari BBC Jioni.

My take:
Sheria hii ya NSSF ni kitanzi kwa wafanyakazi kote nchini hasa wa sekta binafsi kutokana na ukweli kwamba makampuni mengi binafsi yamekuwa yakiwaachisha mara kwa mara wafanyakazi wake huku kukiwa hakuna utetezi wowote wa serikali.Ni vigumu sana wafanyakazi kuunga mkono sheria hii kutokana na ukweli kwamba mtu akiacha kazi akiwa na miaka 30 itampasa kusubiri miaka 25 ili apate mafao yake.Huo ni uendawazimu.
Safi sana LHRC, maana mimi nafikiria kuacha kazi kabla hata ya kufukisha hiyo miaka 55 ili nifanye mambo yangu sasa kwanini PPF wasinipe fedha yangu. Mimi nafanye shirika la umma kwa hiyo mfuko wangu ni PPF, ila mifuko yote kwa sasa inasimamiwa na mamlaka ya SSRA
 
Kwenye hili, mama Hellen Kijo Bisimba, weka mawasiliano tu, tutatuma mchango wowote uutakao, hata ikibidi kwenda mahakama ya dunia, tutawasafirisha, hii serikali, yaani full wizi tu, imeshindwa kukusanya kodi kotoka kwa wafanya biashara inawaza wizi tu, sasa imefikia kuja hadi kwenye viakiba vyetu, wazee wa africa mashariki wameshindwa kuwalipa hadi leo, inafikia hatua hadi hadi wanawamwagia pilipili sembuse sisi, si ndio watatupiga mabomu kabisa?

Kwa wapenda dini, hivi jamani mbona utawala wa Mwinyi na Kikwete migogoro yake ya kipesa inafanana sana, enzi ya mzee ruksa pia serikali ilikuaga haina pesa lakini wafanya biashara hasa wa kihindi walikuwa nazo nyingi tu, eti ni kwaninni? ni swali tu la kizushi!
 
ingefaa zaidi iwepo sheria ya wanchama kuweza kutumia michango yao kama dhamana ya kupata mikopo hasaa ya nyumba
 
Tatizo la Serikali huwa inatunga sheria kama inafanya jando.Sheria zinatungwa kwa siri mno bila kuwahusisha na kuwashirikisha kwa karibu wadau wote.
 
Hao HLRC na nyie wooote mtakaoenda mahamakamani ndio mtakuwa mmefunga rasmi huu mjadala.( au mmesahau msamiati wa cku hzi?). Hahaah, joking.

Ukweli ULIO WAZI ni kwamba, kwenye hii kesi lazima HLRC waangukie pua. Hivi mnajua hilo fao la withdrawal halipo katika sheria yoyote ya PPF au NSSF?. Mlizoeshwa kulambishwa sukari,mkaona raha kumbe mnafadhiliwa!

Mtazoea tu..na hakuna maandamano hapo..NANI kakuambia mtanzania anayekaa ofisini au aliyeko kwa kazi ya Boss anaandamanaga?. Mtapiga kelele nyuma ya keyboard na maofisini kwenu kisha UPEPO utapita.lol!

I support fully operaationalizaon of Pension system in tz, SSRA Wamechelewa sana.
 
ukiwa 65yrs old, na umeshakula mafao yako unakuwa mzigo kwa private sector au jamii?
unafikiria kwa kutumia masaburi! ninakuwa wa private coz jamii haitahusihwa we mbwiga! ni mimi na familia yangu! kwani kikwete anajua babu yangu anaishi vipi? peleka umajinuni wako baharini!
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom