Elections 2010 Hizi ni dalili za kifo cha CCM

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,780
3,227
Na mwandishi Absalom Kibanda wa Tanzania Daima 6/10/2010

Wadau nawaletea kipande cha habari ndefu ya mwandishi huyu ila mimi nimependa tujadili hiki kipande karibuni;

"Ili kufanikisha hilo, kina Dk. Slaa, Mbowe na wenzao wengine wa ndani ya CHADEMA walipaswa na kimsingi wanachopaswa kuendelea kukifanya sasa ni kuwashawishi wananchi sababu za kuwachagua wao na kuwaweka kando kina Kikwete na wagombea wa CCM badala ya kuendelea kuzozana na majenerali ambao kwao siasa si eneo lao la kujidai.
Ni wazi kwamba iwapo vyama vya CUF (Zanzibar) na CHADEMA (Tanzania Bara) vitakuwa na mikakati imara na endelevu ya kisera, kifedha, kimtandao na kioganaizesheni basi safari ya CCM kuendelea kubakia madarakani inaweza ikawa imeanza kukoma mwaka huu kwa upande mmoja wa Muungano au kwa pande zote mbili. Ingawa hilo linaweza likaonekana kuwa ni ndoto ya alinacha kwa baadhi ya watu, hususan wale walio na maslahi ndani ya CCM, ukweli wa kimazingira umeanza kuonyesha kwamba silaha pekee ambazo chama hicho tawala kimebakiza na ambazo sasa inazitumia kama turufu yake ya ushindi ni nguvu ya fedha (si sera), mtandao na historia yake ambayo inawafanya hata wale ambao walipaswa kuwa wameshakihama chama hicho waendelee kubakia humo humo. Hizi ni dalili za mwanzo za kifo cha CCM".
 
bilioni 50 kwa kampain jumlisha 1.7 trilion tuliodanganywa ya kufufua uchumi, I AM GOING TO DYE SOON......!!!
 
Kwa billion 50 Kwa kampeni za miezi 2 manake daily inabidi watumie 1.6 billion.
Alafu mnasema elimu bure na afya bure haviwezekani
 
vote_for_me_plzzz_by_shuqing.jpg
 
Ili kufanikisha hilo, kina Dk. Slaa, Mbowe na wenzao wengine wa ndani ya CHADEMA walipaswa na kimsingi wanachopaswa kuendelea kukifanya sasa ni kuwashawishi wananchi sababu za kuwachagua wao na kuwaweka kando kina Kikwete na wagombea wa CCM badala ya kuendelea kuzozana na majenerali ambao kwao siasa si eneo lao la kujidai.

Hivi huelewi ya kuwa hao majenerali wametajwa katika sehemu ndogo sana ya kampeni za Chadema hivyo picha ya kuwa wanazozana nao siyo sahihi hata kidogo.

Vile vile ieleweke kuwa majeshi ni sehemu ya mtandao wa CCM katika kuendelea kukamata dola na hivyo yangelikuwa ni makosa ya kijinai kwa maana ya kisiasa kama Chadema wangeliwapuuza njemba hizi za majeshini na hadaa zao za vitisho ili tuogope kujitendea haki tarehe 31st October
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom