Hizi msg za Valentine za kufowadiana . . . .

Yaani sijui watu hawazisomagi vizuri au hawajui maana yake???!!!

Namshangaa kweli, katumiwa msg ya u-valentine na jibaba lake usiku wa kuamkia leo halafu anai-fowadi kwangu saa hizi saa tatu na nusu asubuhi, eti "am the first to wish you happy valentine this night, sleep well my sweet"
Sipiyu alokutumia ni wifi au? nimeguswa na hapo aliposema yeye ni wa kwanza!!
 
Bahati mbaya mtu mwenyewe yupo Morogoro mimi Dar. Sasa anadai ananipenda since alipoanza kunifahamu Jan, yaani nilihisi tu tangu mwanzo nadanganywa
Hahahahhahahhhhhh kumbe imetokea Moro !! Asa we ulitegemea uipate saa ngapi?? Loh imechelewea barabarani bana.....alituma saa sita za usiku si ndo mwanzo wa siku? hahahahaaaaaa
 
hujamuelewa Vizuri Michelle.Msg inasema i am the first to wish u this night....then sleep well na hiyo msg katumiwa saa tatu asubuhi. By ze way mzima wewe akin..happy Valentine day.:clap2:
mmmhhhh humpendi tu,lazima ikupe kichefuchefu......
Huyo jibaba ni mwanaume kama wewe na anastahili kupendwa,haihusu nani kamtumia,yeye kaona uzuri kukutumia wewe...na sijaona ubaya wa hayo maneno!!!
 
hujamuelewa Vizuri Michelle.Msg inasema i am the first to wish u this night....then sleep well na hiyo msg katumiwa saa tatu asubuhi. By ze way mzima wewe akin..happy Valentine day.:clap2:

Happy Valentine Vince :clap2::clap2:

asante kunielewesha!!!!
 
Penda penjda tu mimi aaaahaaa nasubiri matukio miye na siku hii ya valentino ya kuigiza
 
Mkuu
Its the Thought That Counts....,

Kuwa au Kutokuwa Mshairi au Mwandishi Mzuri haipunguzi pendo lake Kwako....
 
Sms huwa haina maana iwapo mtumaji hajaiandika mwenyewe hasa kuhusu suala la upendo.
Kwa nini usiandike sms wewe mwenyewe ili ueleze hisia zako badala ya ku send sms aliyoiandika mwenzako???

Yaani mkuu upendo wa watu wa siku hizi, bora dunia ifike mwisho wake mapema
 
Siku ukiwa karibu nae jaribu kuijepa simu yake JIDIPU uone amekusevu vipi, kama unatumatuma vocha usije ukashangaa kukuta umeseviwa vocha dar

Daaah
Aiseee hii itakuwa kali kuliko
Yaani nimeshakuwa vocha, kweli mabinti wa siku hizi balaa
 
Mitambo wakati wa siku kama hizi inalemewa, inawezekana ilitumwa usiku lakini ikafika hiyo saa 3:30 abh.

Mmmmmmmh bibie, unaongea na mtu anaedai anakupenda kwa dhati saa 3 asubuhi anasema "mpenzi, nimekumiss kweli ngoja nikutumie msg ya valentine niliyoandika kwa ajiri yako" halafu ndo unapata kama hiyo niliyoandika hapo juu, hiyo traffic jam ilianzia wapi?
 
Sipiyu alokutumia ni wifi au? nimeguswa na hapo aliposema yeye ni wa kwanza!!

My dia, wa kwanza ni huyo jibaba aliyemtumia, mi nimetumiwa kiporo cha jibaba lake. Angekuwa wifi mbona angejidai, ni binti tu ambaye nilikutana nae wakati nipo Moro kikazi, akadai amevutiwa na mimi huku akidai anamuogopa mwanamke mwenzake (yaani alidhani nina mke au mpenzi), nikamwambia asijali kwani sina mke wala mpenzi tuendelee kuwasiliana tu kama friends
 
Hahahahhahahhhhhh kumbe imetokea Moro !! Asa we ulitegemea uipate saa ngapi?? Loh imechelewea barabarani bana.....alituma saa sita za usiku si ndo mwanzo wa siku? hahahahaaaaaa

Jam gani ananiambia anatuma msg saa 3 asubuhi halafu iko hivyo??!!!!
Mi ndo kwanza nimecheka mpaka basi
 
Mkuu
Its the Thought That Counts....,

Kuwa au Kutokuwa Mshairi au Mwandishi Mzuri haipunguzi pendo lake Kwako....

Kaka, hayo mapendo ya namna hiyo hata siyawezi, kwanza unajuaje kama ana mawazo chanya juu yangu?
 
Back
Top Bottom