Hivi ulipokuwa shule ya msingi,O-level na A-level ushawahi kuwa na cheo gani???

Teh me monitres la std1-3, unaletewa ubuyu,vishet,mahindi ya kukaanga, sukari kwenye vikopo vya Ayu, ili usiwaandike majina ya usumbufu,dah nlikuwa nabebewa ad mfuko wangu wa kitambaa wa daftar kama mfalme! Duh nkapandishwa cheo na kuwa prefect wa area, la5 nikavuliwa, kwa kupigana.
F1-2,monitres, fm3 nkahama shule,fm4 nikawa montres baada ya montres nliyemkuta kupata preg na kuacha shule.dah!
A levo mhasibu Ukwata chuo mwanachuo.
 
Nilipokuwa Primary nilipewa cheo cha kushusha bendera cha lazima na headmaster ambaye alinipenda sana. Nilipokuwa secondary nilikuwa na cheo cha kuchelewa kuingia darasani na utoro.
 
Nilikua mtunza funguo za stoo ya Shule.
Kuna wakati flani kwa masiku machache vyoo vya Skuli vilifanyiwa ukarabati, vikiwa havijakauka saruji vizuri vyoo vichache vikatengwa kwa matumizi na vikafungwa, hapo tena nikaongezewa cheo cha kua mtunza funguo za vyoo!
Mtu hany*, hakojoi hadi ameniona ! (vyeo adimu sana duniani hivi!)
 
dah,labda nilipokuwa mwenyekiti wa inglish klabu form two.hakikudumu sana though,nikapigwa chini wkasababu za kinidhamu.form four nikapewa u- time keeper,mahsusi kunisaidia nisitoroke na kuchelewa kufika(eti walimu waliona kijana mzuri 'anaharibika'....mbav zao!).niliteuliwa saa sita baada breki fupi,kesho yake saa saba kasoro nikavuliwa cheo kile kwa kugonga kengele ya kwenda assemble(kama vipindi vimeisha vile...kudadeki!).nikasogez tu saa yangu mbele afu nikamsubiri mwalimu wa nidhamu,alivouliza nikamwonyesha maamuzi yangu yalitokana na saa yangu maridadi!alikasirika hadi akatamani kulia na cheo kikaishia hapo!!
 
nlikuwa prefect wa mazingira ila nlikuwa mchelewaji mkuu akanivua gamba,nlijiskia vibaya sana
 
Nilikuwa bingwa wa kutegesha vioo chini ya madawati....ndio maana hata shule sikufika nayo mbali, nikaishia kuwa hapa nilipo..mvuvi wa sangara!. Chezeya Yego wewe!.
 
afu mie nilivyofika A-level, nikachaguliwa kuwa nakula chakula cha mchana na mwalimu bachala, ilikuwa raha.
 
Back
Top Bottom