Kijana Majaliwa hana tofauti na Babu wa Loliondo

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Naona yale yale ya BABU wa LOLIONDO yamejirudia tena.

BABU alitupiga kwa KIKOMBE na Sasa KIJANA MAJALIWA katupiga kwa KUFUNGUA MLANGO wa NDEGE kwa NJE.

Watanzania TUNAROGEKA kirahisi kabisa.

JamiiForums-1193006515.jpg
JamiiForums1439110294.jpg
 
Majaliwa aliandikiwa na Mungu mwenyewe, tusimuonee wivu, tusimsimange wala kumsema vibaya. Je angekuwa amelala ghetto kwake muda wa ajali, zali la mentali lingemwangukia? Majaliwa alikuwa kwenye mahali sahihi, na wakati sahihi wa kukutwa na bahati yake. Tumuombe Mungu wakati sahihi wa kukutana na bahati zetu tuwepo mahali sahihi.

Mhubiri 9:11
[11]Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.

I returned, and saw under the sun, that the race is not to the swift, nor the battle to the strong, neither yet bread to the wise, nor yet riches to men of understanding, nor yet favour to men of skill; but time and chance happeneth to them all.
 
Mbona nyuzi za kumpinga shujaa wetu zimekuwa nyingi sana. Serikali ishamtambua huyu dogo kuwa ni shujaa pamoja na jamii. Muacheni dogo atoke kimaisha huu ndo wakati aliyepangiwa na mungu.
 
ila kwenye hili la majaliwa wanaJF tumeonesha udhaifu mkubwa, kwanini kumuonea wivu kijana wa watu aliebahatika kupitia hili tukio? sasa kama hakuwepo pale mpaka akaumia na kuzimia hospital alifikaje au ndio kondakta wa ile ndege?.
 
Afu mkasahau msela ni wa ukanda ule ule wa wakulima wa misifa.

Possible muda anapiga mlango na kasia, ndio muda wale wahudumu pia wanafanya kufungua so ikatokea kwa pamoja.
 
ila kwenye hili la majaliwa wanaJF tumeonesha udhaifu mkubwa, kwanini kumuonea wivu kijana wa watu aliebahatika kupitia hili tukio? sasa kama hakuwepo pale mpaka akaumia na kuzimia hospital alifikaje au ndio kondakta wa ile ndege?.
Wanaomuonea gere ni wapotofu wa shukrani.Ukimsikiliza Majaliwa anaonekana ni kijana muadilifu halafu ni mzito katika kuongea.Ni bahati yake ile.Mambo ya wivu watu waache.Wivu ni wa shetani.
 
Wanaomuonea gere ni wapotofu wa shukrani.Ukimsikiliza Majaliwa anaonekana ni kijana muadilifu halafu ni mzito katika kuongea.Ni bahati yake ile.Mambo ya wivu watu waache.Wivu ni wa shetani.
hii ni tabia mbaya sana na ina akisi aina ya jamii tunayoishi nayo, husda wivu na chuki zisizo na msingi.Haya yote yanafanyika kwasababu wameona amefanikiwa.
 
hii ni tabia mbaya sana na ina akisi aina ya jamii tunayoishi nayo, husda wivu na chuki zisizo na msingi.Haya yote yanafanyika kwasababu wameona amefanikiwa.
Halafu,tu-assume,hakufungua mlango Ila ulijifungua.Sasa itakuwaje?Mama SSH afute kamisheni aliyompa Maja?Bahati ya mtu huja kwa njia hata za ajabuajabu.Watu waache roho mbaya!
 
Halafu,tu-assume,hakufungua mlango Ila ulijifungua.Sasa itakuwaje?Mama SSH afute kamisheni aliyompa Maja?Bahati ya mtu huja kwa njia hata za ajabuajabu.Watu waache roho mbaya!
kabisa mkuu, okay sawa tuassume hakufungua mlango je kule tu kuwa sehemu ya first responders na kule tu kuwa karibu na sehemu ya uokoaji haitoshi kumpa zawadi kwa wema wake na ujasiri?.
 
kabisa mkuu, okay sawa tuassume hakufungua mlango je kule tu kuwa sehemu ya first responders na kule tu kuwa karibu na sehemu ya uokoaji haitoshi kumpa zawadi kwa wema wake na ujasiri?.
Uchoyo na ubinafsi unaisumbua sehemu kubwa(siyo jamii yote)ya jamii yetu.Ingawa ni hulka ya binadamu kuwa mdadisi Ila tunapitiliza na kuonekana wachawi.
 
Uchoyo na ubinafsi unaisumbua sehemu kubwa(siyo jamii yote)ya jamii yetu.Ingawa ni hulka ya binadamu kuwa mdadisi Ila tunapitiliza na kuonekana wachawi.
Ila itavuma baadae itatulia tumtakie majaliwa kila la kheri kwenye mafanikio yake, kwa wivu huu nadhani kuna watu humu wanatamani wangekuwa kwenye ile ajali ili walipwe na bima.
 
Back
Top Bottom