Hivi TBC inafundisha au inapotosha?

Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,323
18,793
Nipo natazama kipindi cha Zamadamu, kinachorushwa na TBC1 wametembelea makumbusho mjini Arusha, kilichonishangaza ni huyu muhusika wa makumbusho anavyotoa maelezo ya uongo, kuna huyu mnyama anaitwa Eland jamaa kasema anaitwa Kudu na kuna mwingine anaitwa Heeterbeast amesema ni Impala, jamani ni elimu finyu au bora liende? au ndio zile ajira za kupewa na mjomba?...kaziii kweli
 
Na mie naangalie huyu jamaa naona ana nyodo kweli au ndo fani ya utangazaji?? Nimeamua kuangalia sehemu nyingien, nadhani kuna umuhimu wa TBC kuangalia watu wa kuwahoji na sio bora kipindi
 
Kuna yule mtangazaji wa kipindi cha nyimbo za dini jumapili- huwa nashindwa kuelewa sijui anafanya vizuri au ananiboa na ile staili yake ya utangazaji. Nadhani ananiboa, hebu ajirekebishe aache kutangaza kama anataka mchumba
 
Preta.hiyo ndo tabia ya watanzania tulio wengi.hatujari ubora.hatuko makini ktk kazi.tumesoma lakini hatujaelimika.
 
Preta.hiyo ndo tabia ya watanzania tulio wengi.hatujari ubora.hatuko makini ktk kazi.tumesoma lakini hatujaelimika.

sasa hapo nimejiuliza...wale ambao hawajui si ndio wamepotoshwa kabisa, na msururu wa kujazana ujinga ndio unazidi kushika kasi
 
sasa hapo nimejiuliza...wale ambao hawajui si ndio wamepotoshwa kabisa, na msururu wa kujazana ujinga ndio unazidi kushika kasi

Mbaya zaidi Preta ni kwamba kile kipindi kilikuwa Recorded, waka ki Edit kabla ya kurushwa!!. Sasa unapoonekana Uozo wa namna hii ambao una Misleed public Sijui tunatengeneza watanzania wa aina gani, kama kituo chao cha taifa kinarusha Sumu.
 
Preta.hiyo ndo tabia ya watanzania tulio wengi.hatujari ubora.hatuko makini ktk kazi.tumesoma lakini hatujaelimika.
Miundombinu tunaweza tusimlaumu sana yule kijana wa pale kwenye jumba la kmbkmb!!! Tatizo kubwa ni kwa hawa wanahabari wa hiki kituo walioruhusu habari yenye upotoshaji kwenda hewani!!
 
Kuna yule mtangazaji wa kipindi cha nyimbo za dini jumapili- huwa nashindwa kuelewa sijui anafanya vizuri au ananiboa na ile staili yake ya utangazaji. Nadhani ananiboa, hebu ajirekebishe aache kutangaza kama anataka mchumba
Tayari mmekwisha anza! :croc::croc:anaitwa Festus makerubi na ndiye huyo wakati mwingine hutangaza Zamadamu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom