hapa sikubaliani na wewe kwa sababu wote wanaopigwa/kuchomwa moto mpaka kuuwawa si vibaka...kuna mwanafunzi wa chuo alishawahi kupigwa mpaka akauwawa eti kwa sababu alipita karibu na nguo zilizoanikwa na mtu mmoja akapiga kelele za mwizi...ingekuwa ni mimi nipo kwenye mamlaka husika ningeiangalia vizuri ile footage na wote walioakuwa wanamwagia mafuta/kumpiga/kumuwekea majani ili moto ukolee wote wangekutana na mvua kali ya sheria...!Walifanya sahihi kuonyesha ili iwe fundisho kwa watu wengine wanao ishi kiujanja ujanja mjini.
Ni sahihi kwa kuwa hatuna askari nchi hii
waliopo ndo wanaowatuma.
kwa anaebisha ngoja yamkute utakuwa wa kwanza!!oa
Tunashukuru kwa kutupa taarifa ya habari mbali mbali zinazotokea katika kona ya Tanzania katika nyanja zote pamoja na vipindi vyenu vinavyoelimisha jamii, tena BURE bila malipo yoyote, mbarikiwe sana.
Sasa nijikite kwenye kilichotokea jana katika taarifa yenu ya HABARI, habari ya kijana kuchomwa moto ni habari iliyochukua nafasi kubwa kwenye habari ya jana, japo napingana na watu kuchukua sheria mkononi, LAKINI kitendo chenu cha kuonyesha kijana yule akiwa anapigwa mpaka kuzirai huku akiwa emetapakaa damu na baada ya hapo kuchomwa moto mpaka kufa SIYO SAHAHI HATA KIDOGO.
Mmefanikiwa kukata vipande vya filamu pindi watu wanapokuwa wanapigana mabusu hongereni kwa hilo lakini vipi kuonyesha picha za watu waliokufa au hata kukatwa mapanga bila hata kutaarifu watazamaji, kuna kipindi huwa mnakwenda mbali kiasi cha kuonyesha hadi kinyesi bila hata ya kutoa taarifa kwa watazamaji wenu.
Please jirekebisheni, mimi siyo mwandishi wa habari lakini sidhani kama ethics za uandishi wa habari zinaruhusu mambo kama hayo, keep in mind kids are watching ITV too.
ila kama hawakuweka tahadhari ndio kosa kama walikutahadharisha kuwa tu mpole sr magdalena..
Du ile habari niliependa sanaa kwani imeua ndege wawili kwa jiwe 1.
1-imepeleka msg kwa vibaka,wezi,matapeli na makanjanja wote wanaojifanya wajanja wa mjini wazee wa mishen town.
2-vyombo vyetu vya usalama vimepata sms ya aibu ya kubweteka mpaka watu wanagushi na kukaa kimya pindi wapewapo taarifa na kufika too late.
ni kweli...!hakukuwa na tahadhari yoyote Ndetichia.
Yaani kwa ujumla hawa ITV & Radio1 thinktank cabinet yao ni ya vilaza kweli kweli, almost wana kila aina za facilities muhimu kwa waandishi wa habari, lakini habari zao bado zinakosa mvuto! ila watangazaji wao wakihamia vituo vingine wana perform wonders! sijui tatizo ni operating procedures au managerial
Teeh x3 Bado niponipo jina lako na avatar yako imenifurahisha! BigUp...:juggle:Tuko hapa kukubaliana kutokukubaliana, regardless, the struggle continues!
hapa sikubaliani na wewe kwa sababu wote wanaopigwa/kuchomwa moto mpaka kuuwawa si vibaka...kuna mwanafunzi wa chuo alishawahi kupigwa mpaka akauwawa eti kwa sababu alipita karibu na nguo zilizoanikwa na mtu mmoja akapiga kelele za mwizi...ingekuwa ni mimi nipo kwenye mamlaka husika ningeiangalia vizuri ile footage na wote walioakuwa wanamwagia mafuta/kumpiga/kumuwekea majani ili moto ukolee wote wangekutana na mvua kali ya sheria...!
Haya yanaweza kuwa na mantiki maana mimi natumia dish mediacom nina kama wiki tatu hivi ITV siipati kabisa licha ya fundi kuhangaika bila mafanikio.Hivi ITV ni bure? Asee tangu haya madish ya kichina yaanze kuleta chenga chenga mi nalipia ITV bana nina kama nusu mwaka sasa! Bure yao kwenye antena au dish gani mkuu
Hapana mkuu, nimeshaibiwa mara nyingi sana lakini kwa kweli sina ujasiri na wala haiingii akilini mwangu kumpiga ,kumwagia mafuta na kuua binadamu mwenzangu hata kama ni kibaka. Wewe ukisikia siku ndugu yako wa karibu amefanyiwa hivyo hata kama kweli ni kibaka ndiyo utajua nina maanisha nini. Wewe unayeshiriki kumuua kibaka huoni unafanya kosa kubwa kushinda alilofanya kibaka mwenyewe na unastahili adhabu kubwa kupita hata atakayepata kibaka kama angepatikana na hatia? Nakushauri ukikuta kibaka anachomwa ufanye kama wale wasamalia wema waliokuwa wanayatoa yale majani yalikuwa yanamuwakia moto.Napata ufahamu hapa wewe hujawahi ibiwa kitu na hujakumbana na machungu ya kuibiwa wewe.