Hivi sisi tukoje?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,232
113,610
Hata kama huyo mtu alikuwa tapeli au mwizi, ndiyo afanyiwe unyama kiasi hicho?

Yaani kweli hayo makosa aliyotuhumiwa yanastahili hiyo adhabu aliyoipata?

Tena mbele ya chombo cha habari mtu anachomwa moto na wao wanaendelea tu kurekodi na hatimaye kuirusha hiyo footage kwenye taarifa yao ya habari bila ilani yoyote ile.

Have we become that desensitized to images of violence and awful cruelty like this one in the video below that we don't get bothered by it anymore?

Last edited by a moderator:
huyo mwandishi/reporter anavyo ripoti utafikiri mtu kuchomwa moto ni sheria ya nchi lol!!
 
Sisi sijui tuna mioyo ya namna gani tu!?

NN usilaumu waa kushangaa mioyo ya hao jamaa , mazingira yamewafanya wa change..angalia mmoja kaibiwa bajaji na askari unaona anavyojibu? eti alikuwa kaenda kukagua kagereza ....wtf....? yaani hajali na ndio maana wananchi wanaona wajichukulie sheria mkononi
 
Sisi sijui tuna mioyo ya namna gani tu!?
Sio sisi tu. Binadamu mkuu.. We can be cruel and sadic...
Kumbuka wakati hapakua na serikali ya nguvu
hata Europe/US na Asia yalitokea. Saa zingine hata zaidi...
When people don't trust the formal justice system wataazibu wenyewe
na matokeo yake ndio hayo. the mob doesn't think.
 
Inatisha kwa kweli!
 
Inatisha kwa kweli!
Inatisha sana, hasa ukikumbuka kua kila mtu ana haki ya kujitetea ashtakiwapo.
hapo ukute kesi ingeenda mahakamani maybe angekua sio tapeli by law
au wangepata namna ya kumlipa yule alie tapeliwa, na huyu akafungwa miaka kadhaa
Now it can't be undone, na mali yake hapati. Mmoja katapeli, wengi wameua... so sad.
 
Sasa tuseme imetokea case ya mistaken identity...si mtu asiye hata na hatia anaweza akapoteza maisha yake hivi hivi...

Huu mtindo ni mbaya sana.
 
Sasa tuseme imetokea case ya mistaken identity...si mtu asiye hata na hatia anaweza akapoteza maisha yake hivi hivi...

Huu mtindo ni mbaya sana.
Kwanza kuna hayo: unajuaje huyu mtu yuko guilty?
Pili kuna kosa la proportion: Hata akiwa guily ndio hivi jamani?
Tatu kuna ile complicity wa watu. They are all criminals
Huyo alie recodi, na hao walio mchoma, na waliokuwepo
Kwa nini hawakujaribu kumuokoa huyo victim?
Na kama hakuna atakae wajibika hapo basi makosa yanaendelea tu.
 
This is wrong in so many levels

Nawahurumia hao watoto wanaoshuhudia unyama huo unaofanywa na watu wazima they look up to.
 
Tatu kuna ile complicity wa watu. They are all criminals
Huyo alie recodi, na hao walio mchoma, na waliokuwepo

Oh yeah...I'd charge those damn onlookers as well for failing to take action against the burning that someone/anyone of ordinary prudence would have done under the same circumstances!

And just for good measure, I'd add another charge of 'relishing the misery of a dying person'

"Stupids"
 
NN, kwanza nakuomba na wewe uweke viewer discretion advice:poa.
sijaiangalia hiyo video, i am a sensitive viewer:A S embarassed:.
lakini tatizo ni pana zaidi, wananchi wamechoka na hakuna system ya kuhakikisha haki inatendeka. huko polisi hakufai, kama mwakyembe alingejewa apeleke ushahidi kuwa kuna tishio dhidi yake na akapeleka na polisi bado waka-mute, unategemea nini kwa hao wa chini. we need an overhaul of the system, and there after tuanze psychological treatment.
 
Tunashukuru kwa kutupa taarifa ya habari mbali mbali zinazotokea katika kona ya Tanzania katika nyanja zote pamoja na vipindi vyenu vinavyoelimisha jamii, tena BURE bila malipo yoyote, mbarikiwe sana.

Sasa nijikite kwenye kilichotokea jana katika taarifa yenu ya HABARI, habari ya kijana kuchomwa moto ni habari iliyochukua nafasi kubwa kwenye habari ya jana, japo napingana na watu kuchukua sheria mkononi, LAKINI kitendo chenu cha kuonyesha kijana yule akiwa anapigwa mpaka kuzirai huku akiwa emetapakaa damu na baada ya hapo kuchomwa moto mpaka kufa SIYO SAHAHI HATA KIDOGO.

Mmefanikiwa kukata vipande vya filamu pindi watu wanapokuwa wanapigana mabusu hongereni kwa hilo lakini vipi kuonyesha picha za watu waliokufa au hata kukatwa mapanga bila hata kutaarifu watazamaji, kuna kipindi huwa mnakwenda mbali kiasi cha kuonyesha hadi kinyesi bila hata ya kutoa taarifa kwa watazamaji wenu.

Please jirekebisheni, mimi siyo mwandishi wa habari lakini sidhani kama ethics za uandishi wa habari zinaruhusu mambo kama hayo, keep in mind kids are watching ITV too.
 
meseji senti,inabidi wajirekebishe!warning ni muhimu ili watoto wakimbizwe vyumbani
 
Naunga mkono, ni taswira mbaya kuonekana machoni mwa watoto.

La pili ambalo limeniudhi jana ni kutoonesha Tamthilia ya Great Queen Sendeok kwa sababu zisizo za msingi.
 
Wako sahihi.......tabia mbaya lazima zionyeshwe zikiwa na matokeo mabaya.....ifuate waonyeshe ulevi ni mbaya kuanzia mwanzo hadi mtu anapokosa fahamu kabisa

Sikubaliani na wewe mkuu kulikuwa hakuna sababu ya msingi ya kuonyesha kijana akichomwa moto mpaka kifo kwenye Tv yao, na mbaya zaidi bila hata tahadhari, siyo sahihi kwa mtazamo wangu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom