Hivi sisi tukoje?

Sioni tatizo kwa ITV kuonyesha matukio kama hayo, hata kama kuna watoto. Wakiona mwizi anavyochomwa moto ni moja ya mafunzo kwao. Imefikia wakati ambapo watoto wanaweza kuangalia matukio kama hayo ambayo yatawafungua akili zaidi na kuelewa kuwa kuna vita, kuna ajali na kuna vitu vya kuvikwepa na kuvikimbilia.

Kwa fundisho sio tatizo. Ingekuwa picha za ngono na vitendo vya mapenzi ningewalaumu ITV.
 
Yaani kwa ujumla hawa ITV & Radio1 thinktank cabinet yao ni ya vilaza kweli kweli, almost wana kila aina za facilities muhimu kwa waandishi wa habari, lakini habari zao bado zinakosa mvuto! ila watangazaji wao wakihamia vituo vingine wana perform wonders! sijui tatizo ni operating procedures au managerial
 
Sikubaliani na wewe mkuu kulikuwa hakuna sababu ya msingi ya kuonyesha kijana akichomwa moto mpaka kifo kwenye Tv yao, na mbaya zaidi bila hata tahadhari, siyo sahihi kwa mtazamo wangu.
Kwani tupo hapa kukubaliana!!?? hata yeye hakubaliani na wewe!!
 
Ni sahihi kwa kuwa hatuna askari nchi hii
waliopo ndo wanaowatuma.
kwa anaebisha ngoja yamkute utakuwa wa kwanza!!:poa
 
Sioni tatizo kwa ITV kuonyesha matukio kama hayo, hata kama kuna watoto. Wakiona mwizi anavyochomwa moto ni moja ya mafunzo kwao. Imefikia wakati ambapo watoto wanaweza kuangalia matukio kama hayo ambayo yatawafungua akili zaidi na kuelewa kuwa kuna vita, kuna ajali na kuna vitu vya kuvikwepa na kuvikimbilia.

Kwa fundisho sio tatizo. Ingekuwa picha za ngono na vitendo vya mapenzi ningewalaumu ITV.

Kwa hiyo hata kuonyesha ngono ni poa tu, ili tuwafundishe watoto wetu kuwa ukifanya vile utapata mimba au magonjwa ya kuambukiza, somo kwa njia ya Television
 
Yaani kwa ujumla hawa ITV & Radio1 thinktank cabinet yao ni ya vilaza kweli kweli, almost wana kila aina za facilities muhimu kwa waandishi wa habari, lakini habari zao bado zinakosa mvuto! ila watangazaji wao wakihamia vituo vingine wana perform wonders! sijui tatizo ni operating procedures au managerial

Kuna habari zingine wanazipa coverage vizuri,zingine (mara nyingi) ni very poor,so low.
 
Sr. Magdalene.

Siyo ITV tu, hata jamaa wa clouds nao walionyesha kijana akiwa anafanywa bbq live on TV mbele ya watoto wetu, japo kuwa wao walitoa tahadhari kuhusu picha.
 
Ni sahihi kwa kuwa hatuna askari nchi hii
waliopo ndo wanaowatuma.
kwa anaebisha ngoja yamkute utakuwa wa kwanza!!:poa
hapa najiuliza kwanini watu huwa tunataka kuona habari za matukio kama yale yaliyotokea songea juzijuzi...na tena utasikia watu wananalalamika vyombo vyetu vya habari ni fake kwa sababu badala ya kuonyesha matukio kama hayo wanaonyesha vipindi vingine kama mziki...humu humu watu huwa wanalialia kila siku linapokea tukio lolote(hata liwe la umwagaji damu) "wekeni picha wekeni picha wekeni picha"...hayo matukio yanatofauti gani na hili la kijana kuchomwa moto? siungi mkono jamaa waliomchoma kijana moto ila jamii inatakiwa ione na vivile kukemewa kuhusu kujichukulia sheria mkononi...!
 
Sr. Magdalene.

Siyo ITV tu, hata jamaa wa clouds nao walionyesha kijana akiwa anafanywa bbq live on TV mbele ya watoto wetu, japo kuwa wao walitoa tahadhari kuhusu picha.

watoto wenyewe wenye kushinda wakiangalia movie za mauaji na kucheza games za kuuana? jaribu kumuasa mwanao kama fursa kama hiyo imejitokeza wakati mnaangalia naye tv...ni vitu vinavyotokea kwenye jamii yetu kwa hiyo ni busara kuvitolea maelezo hata kwa watoto wadogo...!
 
Du ile habari niliependa sanaa kwani imeua ndege wawili kwa jiwe 1.

1-imepeleka msg kwa vibaka,wezi,matapeli na makanjanja wote wanaojifanya wajanja wa mjini wazee wa mishen town.

2-vyombo vyetu vya usalama vimepata sms ya aibu ya kubweteka mpaka watu wanagushi na kukaa kimya pindi wapewapo taarifa na kufika too late.
 
Mie naungana na walichoonesha ITV ila walichokosea hawakutoa tahadhari kabla kwa watizamaji,
Kuwapa awereness ya kitakachoonekana kwenye hipo taarifa,otherwise ni fundisho tosha hata kwa watoto wajue kbs kuiba sio kitu kizuri.
 
Mimi sikubaliani na mtoa mada kuna mambo mengi sana yana kera hata yanadhalilisha utu na utamaduni wetu kuliko hata lililoonyeshwa jana na ITV.
 
wezi, vibaka majambazi siwasapoti hata kidogo. wamenirudisha sana nyuma kimaendeleo. yaani ntakapokuta wakimsulubu mwizi au mtu dizaini hiyo basi na mimi ntakuwa mshiriki. nna hasira nao sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom