Hivi ndivyo Mbowe anaadhimisha miaka 50 ya Uhuru na Kuzaliwa kwake!

hizo sifa zote sababu ya urais

Pure Bandwagon fallacy. Look at the issues. Nway...pia si dhambi. Lakini haina uhusiano wowote na hicho unachokifikiria wewe sasa hivi. Jimbo la Hai, linapaswa kuwa jimbo la mfano. Sina haja ya kusema sababu gani eeh!
 
Wabongo sijui mpaka mfanyiwe nini ndo mridhike. Mtu akiwa fisadi kama Kikwete mnalalamika; mtu akijihusisha kwenye shughuli za maendeleo kama hizi anazoanzisha Mbowe mnalalamika pia; Mtu akiamua kukaa tu bila kufanya lolote mnamwita *****! Hivi mnataka mtu afanye nini ndo mrizike?

Kweli kamanda. Wakati mwingine we are too much negative of ourselves. Pole pole watu wataelewa labda. Actuaaly haitarajiwi tukubaliane kwa kila kitu, lakini mtu mwenye akili anapaswa kutazama mantiki na authentic katika kila jambo analoliona, kulisoma au kulisikia au kulisoma.
 
Nimeipenda sana hii Mwekiti Mbowe nafikiri kila mwanachadema akifanya hivi kwa nafasi yake tutajitofautisha sana na hao mafisadi na makupe.
 
Kama amezaliwa september inakuaje asherehekee Disemba?. Au ni kutafuta sifa?.

Hizi ni sifa za uraisi, hana lolote. Raisi hawezi kutoka KASKAZINI. Atausikia kwenye bomba.

Kamanda soma basi kwa utulivu, mbona unasoma kama unakimbizwa. If u cant listen u cant understand, that is philosopy of understanding ili uwe katia nafasi nzuri ya kujenga hoja ya kupinga ama kuunga mkono. Amezaliwa Septemba 1961 ndiyo, akabatizwa Desemba 9, 1961, mbona imeandikwa kwenye thread vizuri tu. Soma vyema, si kusoma headline halafu unafikiri umeelewa bro.
 
safi sana kama anajituma kufanya kazi ili apate sifa Mungu mwenyewe anapenda sifa sembuse wanadamu tulio umbwa kwa mfano wake

Achani kejeli mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
 
Atakua alishamsamehe kitambo sana wala hakumbuki tena!
Big up baba, kuliko uende clouds kuongelea wimbo uupendao!
yule muislam aliyempiga kofi wakati wa uchaguzi atakuwepo?nadhani itakuwa nafasi nzuri amuombe Radhi.mbowe amefikiria vizuri badala ya kuhangaika na uch
ochezi na maandamano yaSiyo na tija.
 
Kama amezaliwa september inakuaje asherehekee Disemba?. Au ni kutafuta sifa?.

Hizi ni sifa za uraisi, hana lolote.

Raisi hawezi kutoka KASKAZINI. Atausikia kwenye bomba.

soma vizuri sio unakurupuka kama mende chooni..
 
Mbowe anafanya kwa ajili ya kutafuta sifa. Mengi nae pia hajitambui, hauwezi utoe misaada wakati unashindwa kuwalipa wafanyakazi wako.

Tunahitaji viongozi wanaofanya kwa ajili ya watanzania. Ila sio wanaotafuta popularty kwa kupitia shida zetu. Huu ni uhuni.
kwan anayelipa mishahara ni Mengi au ni kampuni? Na anayetoa misaada ni Mengi au ni kampuni? Tukiweza kulijua hili itasaidia sana!
 
Baada ya maandalizi ya muda mrefu kidogo, vikao kadhaa, huku akilazimika kukatisha ili akabiliane na majukumu muhimu ya kitaifa kama vile vikao vya bunge na suala nyeti la Katiba Mpya, hatimaye Mheshimiwa Freeman Mbowe baada ya kuwa amejumuika na Wananchi wenzake pale Uwanja wa Uhuru, kesho Jumamosi, Desemba 10, 2011, ataanza shughuli kadhaa kwa siku mbili mfululizo za kusherehekea miaka 50 ya uhuru na kuzaliwa kwake.

Kamanda alizaliwa Septemba, 1961 lakini akabatizwa siku yenyewe ya uhuru, Desemba 9, 1961. Na kuitwa Freeman. Siku ya Jumamosi, Desemba 10 kutakuwa na shughuli kadhaa, itakayojumuisha harambee na uzinduzi wa miradi kadhaa;

1. Kutakuwa na harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya Msikiti wa Lambo, uliopo eneo la kijiji alichozaliwa cha Nshara, huko Machame. Shughuli hii mgeni rasmi alipaswa kuwa Mzee Sabodo, lakini kutokana na sababu nje ya uwezo sasa atakuwa Shehe Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Shughuli ya Harambee itatanguliwa na ibada itakayoongozwa na Alhaji Sheikh Yusuf Lyasenga.

2. Kutakuwa na uzinduzi wa Kampeni ya "Make Kilimanjaro Beautiful". Hii ni matokeo ya ziara zake za kuzungukia maeneo ya jimbo na Wilaya ya Hai na kuwasikiliza wananchi, ambapo amejionea athari za ukataji miti hovyo, hali inayokaribisha jangwa kwa kasi na kukausha vyanzo vya maji, kuweka maisha ya watu na mifugo yao hatarini na kisha kuharibu mandhari nzuri ya wilaya na mkoa. Hivyo project inalenga kupanda miti milioni 3 ndani ya miaka 4. Phase one itazinduliwa Desemba 10, Lengo ni ku-cover 40 kms. Cost of 1 km per annum is 9 mil.

3. Itazinduliwa Project Keep Boma Clean; hii italenga kuhamasisha kuwa suala la utunzaji mazingira na usafi wa makao makuu ya Hai, Bomalang'ombe kuwa suala endelevu. Mheshimiwa Mbowe na viongozi wengine wa serikali, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro (ndiye mgeni rasmi katika shughuli zote za uzinduzi wa miradi mbalimbali ya Desemba 10), mkuu wa wilaya, watendaji wa halmashauri, watafanya usafi mitaa yote, kisha atatoa vifaa vya kufanyia usafi na kuzolea taka. Pia kutakuwa na shughuli ya kuyatambua maeneo ya kupumzikia na viwanja vya wazi kwa ajili ya kuchezea watoto.

4. Kutakuwa na uzinduzi wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali, isiyokuwa ya kisiasa wala isiyotengeneza faida, iitwayo HAI Kilimanjaro Development Initiative (HAKIDI). Hii itahusika katika "coordinating, mobilizing resources and carrying out different projects in Hai District with the ultimate objective of creating employment, conducting empirical researches, studies and appraisals that will form the basis for different social economic interventions. It 'll also carry out other social responsibilities like improving environment and any other that adds to the wellbeing of Hai Residents.

5. Lastly, but not least is the Project of "Jobs 5000". Its ultimate goal is to create 5000 salaried jobs in Hai District by 2015, specifically in Agriculture and Tourism. How; under HAKIDI, training of appropriate skills will be provided to youths, establishing and registration of Machame route porters society, work out modalities to sustain the project with Hai District authorities, etc. Mpaka sasa vijana wapato 450 wameshapata mafunzo na zaidi ya nusu yao wameajiriwa tayari, katika sekta ya utalii.

Baadae jioni kutakuwa na mkutano wa hadhara, Bomang'ombe. Tutawajuza kitakachozungumzwa kwa wananchi.


7. On Sunday, December, 2011, Mheshimiwa Mbowe atakuwa na harambee ya uchangiaji fedha kwa ajili ya upanuzi na ujenzi wa Kanisa la KKKT hapo Kijijini Nshara, ambapo Alex Malasusa, Thomas Leizer, Martin Shao wataongoza ibada (kwa kusaidiana), huku Mgeni Rasmi akiwa ni Reginald Mengi. Viongozi waandamizi wa serikali, wastaafu, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wa vyama mbalimbali wamealikwa.

Karibuni.
Mbona shughuli zooote hizo zilizo orodheshwa zimeilenga Hai tu? Kulikoni?
 
kwan anayelipa mishahara ni Mengi au ni kampuni? Na anayetoa misaada ni Mengi au ni kampuni? Tukiweza kulijua hili itasaidia sana!



Nail On The Coffin...

Huyu "Mzee" anajifanyaga kasoma sana na mwerevu sana lakini alishindwa kutofautisha kitu kidogo tu kama hicho?
Kama nakumbuka vizuri inaitwa "separate entity".
 
Big up Mh

Safi sana kamanda kweli hayo ni maono anayoyapata kiongozi yeyote alietulia na kuwatanguliza watu anaowaongoza. Daima Mungu hushuka na kumpa hekima. Mungu akubariki kakaangu. Nyie chapeni mwendo Mungu amewaona mpk huku vijijini tumewaelewa niko Makete. Kila siku lazima nikutane na raia mmoja niuze sera ya cdm.
 
Kamanda soma basi kwa utulivu, mbona unasoma kama unakimbizwa. If u cant listen u cant understand, that is philosopy of understanding ili uwe katia nafasi nzuri ya kujenga hoja ya kupinga ama kuunga mkono. Amezaliwa Septemba 1961 ndiyo, akabatizwa Desemba 9, 1961, mbona imeandikwa kwenye thread vizuri tu. Soma vyema, si kusoma headline halafu unafikiri umeelewa bro.

nimesoma vizuri, thats why nimeuliza inakuaje asherehekee besidei yake disemba wakati yeye ni wa septemba?. Hapo atakuwa anasherehekea siku ya ubatizo na wala si siku ya kuzaliwa. Siku ya kuzaliwa imeshapita, pengine alisherehekea kimya kimya na familia yake then leo anakuja kujitafutia sifa wakati tunasherehekea siku ya kuzaliwa taifa letu pendwa.
 
soma vizuri sio unakurupuka kama mende chooni..

nimesoma vizuri. Nina uhakika na ninachosema.

Nauliza, kama amezaliwa septemba 61 then disemba 61 akabatizwa. Sasa anachosherekea ni siku ya kuzaliwa kwake au siku ya ubatizo?.

Sherehe yake imekaa kisiasa siasa. Ni vigumu kuwaruhusu wachaga watawale nchi hii. Mungu atuepushie mbali..
 
Hapo Boma mbowe inabidi pawe Clean kweli tushindane na moshi mjini, hasa maeneo ya soko la zamani na hapa stendi mpya! Hiyo movement ya Keep boma clean nimeipenda! HONGERA JEMBE MBOWE MUNGU AKULINDE .
 
Back
Top Bottom