Hivi ndivyo Mbowe anaadhimisha miaka 50 ya Uhuru na Kuzaliwa kwake!

big up kamanda wa anga hakuna kulala mpaka kieleweke wakati wanapiga kelele kuhusu kaskazini sisi tujadili na kuimarisha kaskazini yetu generate ajira,hifadhi mazingira hamasisha usafi, kaskazini salama inawezekana, my take hii kasi ijumuishe na Arusha.
 
Vizuri saana! This is how MP's are supposed to be. Plan and Work for your constituency. Although 5000 chances of employment are not enough, but not bad to start with. Bravo Freeman bravo!
 
naomba kama kuna member yupo karibu na january makamba ampe asome hii,mambo yanafanywa kitaalam na kiutu uzima zaidi,mambo ya kukurupuka bila kuhesabu gharama na matokeo hayalipi wakuu,thank you mbowe
 
nimesoma vizuri, thats why nimeuliza inakuaje asherehekee besidei yake disemba wakati yeye ni wa septemba?. Hapo atakuwa anasherehekea siku ya ubatizo na wala si siku ya kuzaliwa. Siku ya kuzaliwa imeshapita, pengine alisherehekea kimya kimya na familia yake then leo anakuja kujitafutia sifa wakati tunasherehekea siku ya kuzaliwa taifa letu pendwa.
Siku ya kuzaliwa siyo lazima uisherekee tarehe hiyo hiyo inaweza kufanyika kabla au baada ya tarehe husika. Ni kumbukumbu tu wala si jambo la kisheria. Lakini haya ni mambo ya kuiga tusitegemee kila mtu awe na uwelewa nayo wa kutosha.
 
what kind of charty is this!? Hapo anafanya siasa, cheap popularty.
Busara za Chimwaga zinaniacha hoi. Kwa hiyo kila anayefanya siasa anatafuta cheap popularity? Anayetafuta 'real popularity' anapaswa afanye nini? Ufisadi?
 
Siku yake ya 'kuzaliwa kiroho' (ubatizo) atafanya harambee ya kujenga Msikiti. Na mgeni rasmi ni Sheikh wa Mkoa. Kweli siasa ni mchezo mchafu.

bora hilo la kujenga msikiti na kanisa kama atakavyofanya leo na kesho vipi sherehe za jana za kutumia pesa badala ya kutuonesha tulipo na tunakwenda wapi 50 yrs to kam
safi sana mbowe onesha mfano tuko pomoja achana na hao wanajisifu wakti kila kitu kinatoka china tunafurahia kwa kuwa soko la watu wengine leo hata kiwanda cha tanbond ,dabaga hakipo tunategemea blue band toka kenya tena hii ni kwa sisi wenye nafuu ukimuuliza mtu wa kijijini hajui tuna zungumza nini

 
Hapa tunajadiri birthday za watu au shughuli za maendeleo anazotarajia kuzifanya? Mbona hilo mnalokomalia halina tija yoyote. Watu makini hujadiri vitu vya msingi na si upuuzi, mtu akiamua kusherehekea birthday kila siku inatuhusu nini sisi. Acheni utoto kama si ujinga na ujuha bana...mna bore sana ninyi watu to mention few " Mzee na Ritz"

kwani si typo ile?! Ama... Kwani typo inajadiliwaga??!
 
Kuhusu gharama usiwe na shaka, kwa kuwa mwykt katuonyesha mfano wa harambeee! Siasa za kenya za tangu enzi hizooo za hayati Mzee Jomo Kenyata na Mama Ngina eeenh?
Nazikubali sana siasa za harambee za Mzee Jomo Kenyatta. Kutokana na harambee hizo vijana wengi wa Kenya walikwenda shule na vyuoni (siyo kuingia madarsani tu) na matokeo yake tunayaona yanavyotutia kiwewe tunapofikiria kuendeleza mchakato wa EAC. MWENYEKITI SONGA MBELE NA HARAMBEE.
 
Kama amezaliwa september inakuaje asherehekee Disemba?. Au ni kutafuta sifa?.

Hizi ni sifa za uraisi, hana lolote.

Raisi hawezi kutoka KASKAZINI. Atausikia kwenye bomba.

sijawahi kuwaza kama unaweza kuandika upuuzi kama huu hapa jf!acha ubaguzi.
 
Nazikubali sana siasa za harambee za Mzee Jomo Kenyatta. Kutokana na harambee hizo vijana wengi wa Kenya walikwenda shule na vyuoni (siyo kuingia madarsani tu) na matokeo yake tunayaona yanavyotutia kiwewe tunapofikiria kuendeleza mchakato wa EAC. MWENYEKITI SONGA MBELE NA HARAMBEE.
Mara nyingi Watz tumekuwa tukishabikia siasa bila kuzielewa. Nakupa mfano wa azimio la Arusha. Tulitembea kwa miguu kuunga mkona mpaka wengine walikufa. Tukidhani kuwa sasa, matajiri wananyang'anywa mali zao kwa nguvu ili tufaidi sote. Pilika zilikuwa kubwa 'hakuna kulala'. Matajiri wengi walichukizwa sana (hata mimi na wewe, leo tukifanyiwa vile, hatutofurahi) wengine walikufa kwa kihoro, wengine waliihama nchi kwa kuona siasa kigeugeu, leo hivi, kesho je itakuwaje? Hao tuwaache kwanza turudi kwetu sie tuliodhania kuwa sasa Majumba, Mashamba,Viwanda, Magari nk. Wamenyang'anywa wanyonyaji wale, sasa ni mali ya umma, yaani sasa ukikuta shamba unaingia unalima tu, au gari 'su' unachukuwa tu unaende unakotaka kisha unalirudisha anachukuwa mwingine. Kumbe loooh! Sivyo kabisaaa! Tumekuja elewa wakati mambo yameshaharibika. Kumbe zoezi lile tulilolishabikia kwa nguvu zote ni kuwanyang'anya wamiliki halali wa mali zile na kuwapa 'Waswahili' wachache watumbue na kugawana mali kama zao vile! Sie tulioshangilia hakuna tulichoambulia zaidi ya kuambiwa 'jamani kazeni mikanda' hali ngumu! Huo ni mfano mmoja tu. Tafakari, chukua hatua.
 
Kamanda soma basi kwa utulivu, mbona unasoma kama unakimbizwa. If u cant listen u cant understand, that is philosopy of understanding ili uwe katia nafasi nzuri ya kujenga hoja ya kupinga ama kuunga mkono. Amezaliwa Septemba 1961 ndiyo, akabatizwa Desemba 9, 1961, mbona imeandikwa kwenye thread vizuri tu. Soma vyema, si kusoma headline halafu unafikiri umeelewa bro.
Kikristo kubatizwa pia ni kuzaliwa upya. Mweleze huyu mwenye kutaka petty arguments.
Watanzania utadhani tumelaaniwa toka matumboni mwa mama zetu! Kutafuta vijikosa vidogovidogo na kuacha kutafuta makosa makubwa yenye athari kubwa ndio jadi ya wengi.Sijui tutafika wapi.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hapa naanza kufarijika atlast my party is starting to walk the talk wengine wakiiga itakuwa plus lakini kwajinsi walivyo mafisadi wakiiga badala ya kujenga watazidi kubomoa....I am really impressed by these good intiatives..Kudos my honorable chairperson Freeman Aikael Mbowe Mungu akuongezee miaka mingine 50 ya bila uzee kwakurejesha ujana wako kama tai!
 
Kama amezaliwa september inakuaje asherehekee Disemba?. Au ni kutafuta sifa?.

Hizi ni sifa za uraisi, hana lolote.

Raisi hawezi kutoka KASKAZINI. Atausikia kwenye bomba.

ukiwashwa jikune, ukitafuta wa kukukuna unaweza kukunwa na dudu.
 
Laiti watu wengi zaidi wangetaka sifa kama hizi taifa letu lisingetia aibu kama sasa.

Long live Freeman Mbowe!

wos, tatizo la watanzania sisi,, na hasa wanaojisikia kwamba wana hisa kwenyeuongozi wa nchi hii, ni viziwi na vipofu. Hawaoni jema wala hawasikii jema.
Kazi yao ni kuona wanataka kunyang'anywa uongozi wa ncho.
Inashamgaza kama kuna mtu anaona initiatives za mbowe kwenye jimbo lake ni kutafuta sifa.
Hawahawa ndo wanaanzisha threads zinazosema cdm wamefanya nini majimboni mwao.
Huu ni upumbavu kwa viwango vya iso
 
Back
Top Bottom