Hivi ndivyo Mbowe anaadhimisha miaka 50 ya Uhuru na Kuzaliwa kwake!

Chief Isike

JF-Expert Member
Jan 17, 2010
445
462
Baada ya maandalizi ya muda mrefu kidogo, vikao kadhaa, huku akilazimika kukatisha ili akabiliane na majukumu muhimu ya kitaifa kama vile vikao vya bunge na suala nyeti la Katiba Mpya, hatimaye Mheshimiwa Freeman Mbowe baada ya kuwa amejumuika na Wananchi wenzake pale Uwanja wa Uhuru, kesho Jumamosi, Desemba 10, 2011, ataanza shughuli kadhaa kwa siku mbili mfululizo za kusherehekea miaka 50 ya uhuru na kuzaliwa kwake.

Kamanda alizaliwa Septemba, 1961 lakini akabatizwa siku yenyewe ya uhuru, Desemba 9, 1961. Na kuitwa Freeman. Siku ya Jumamosi, Desemba 10 kutakuwa na shughuli kadhaa, itakayojumuisha harambee na uzinduzi wa miradi kadhaa;

1. Kutakuwa na harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya Msikiti wa Lambo, uliopo eneo la kijiji alichozaliwa cha Nshara, huko Machame. Shughuli hii mgeni rasmi alipaswa kuwa Mzee Sabodo, lakini kutokana na sababu nje ya uwezo sasa atakuwa Shehe Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Shughuli ya Harambee itatanguliwa na ibada itakayoongozwa na Alhaji Sheikh Yusuf Lyasenga.

2. Kutakuwa na uzinduzi wa Kampeni ya "Make Kilimanjaro Beautiful". Hii ni matokeo ya ziara zake za kuzungukia maeneo ya jimbo na Wilaya ya Hai na kuwasikiliza wananchi, ambapo amejionea athari za ukataji miti hovyo, hali inayokaribisha jangwa kwa kasi na kukausha vyanzo vya maji, kuweka maisha ya watu na mifugo yao hatarini na kisha kuharibu mandhari nzuri ya wilaya na mkoa. Hivyo project inalenga kupanda miti milioni 3 ndani ya miaka 4. Phase one itazinduliwa Desemba 10, Lengo ni ku-cover 40 kms. Cost of 1 km per annum is 9 mil.

3. Itazinduliwa Project Keep Boma Clean; hii italenga kuhamasisha kuwa suala la utunzaji mazingira na usafi wa makao makuu ya Hai, Bomalang'ombe kuwa suala endelevu. Mheshimiwa Mbowe na viongozi wengine wa serikali, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro (ndiye mgeni rasmi katika shughuli zote za uzinduzi wa miradi mbalimbali ya Desemba 10), mkuu wa wilaya, watendaji wa halmashauri, watafanya usafi mitaa yote, kisha atatoa vifaa vya kufanyia usafi na kuzolea taka. Pia kutakuwa na shughuli ya kuyatambua maeneo ya kupumzikia na viwanja vya wazi kwa ajili ya kuchezea watoto.

4. Kutakuwa na uzinduzi wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali, isiyokuwa ya kisiasa wala isiyotengeneza faida, iitwayo HAI Kilimanjaro Development Initiative (HAKIDI). Hii itahusika katika "coordinating, mobilizing resources and carrying out different projects in Hai District with the ultimate objective of creating employment, conducting empirical researches, studies and appraisals that will form the basis for different social economic interventions. It 'll also carry out other social responsibilities like improving environment and any other that adds to the wellbeing of Hai Residents.

5. Lastly, but not least is the Project of "Jobs 5000". Its ultimate goal is to create 5000 salaried jobs in Hai District by 2015, specifically in Agriculture and Tourism. How; under HAKIDI, training of appropriate skills will be provided to youths, establishing and registration of Machame route porters society, work out modalities to sustain the project with Hai District authorities, etc. Mpaka sasa vijana wapato 450 wameshapata mafunzo na zaidi ya nusu yao wameajiriwa tayari, katika sekta ya utalii.

Baadae jioni kutakuwa na mkutano wa hadhara, Bomang'ombe. Tutawajuza kitakachozungumzwa kwa wananchi.

7. On Sunday, December, 2011, Mheshimiwa Mbowe atakuwa na harambee ya uchangiaji fedha kwa ajili ya upanuzi na ujenzi wa Kanisa la KKKT hapo Kijijini Nshara, ambapo Alex Malasusa, Thomas Leizer, Martin Shao wataongoza ibada (kwa kusaidiana), huku Mgeni Rasmi akiwa ni Reginald Mengi. Viongozi waandamizi wa serikali, wastaafu, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wa vyama mbalimbali wamealikwa.

Karibuni.
 
yule muislam aliyempiga kofi wakati wa uchaguzi atakuwepo?nadhani itakuwa nafasi nzuri amuombe Radhi.mbowe amefikiria vizuri badala ya kuhangaika na uch
ochezi na maandamano yaSiyo na tija.
 
Hongera Mh wazo zuri sana tunahitaji watu kama nyie,Mungu akuzidishie na akuongoze katka harakati zako.
 
Ni aina ya viongozi ambao ratiba zao zimejaa shughuli zenye tija kwa Taifa na ni shughuli za wazi, sio wale wanaojaza ratiba zao kwa mapango-mkakati ya kimtandao..Tunahitaji viongozi wabunifu, wachapa kazi,wamisionary..ambao kulala na kuamka kwao, wanawaza na kuwazua njia na mbinu mbalimbali za kumkwamua masikini na kumpa hadhi ya utu wenye heshima mama mjamzito,Kijana mjasiriamali,Mtoto yatima, ndugu mlemavu, binti msomi, mtumishi wa umma,baba,bibi na babu wastaafu..Kama yalivyo dhahiri mafuta kwenye maji,vivyo hivyo kwa viongozi Bora; Mawazo, maneno na matendo yao huwatenga mbali na kuwapambanua bayana dhidi ya viongozi wachovu!..Hongera mbowe,Mengi,Sabodo na wengine...Don't u ever get tired of doing the right thing; coz in the end thats what pays off...
 
yule muislam aliyempiga kofi wakati wa uchaguzi atakuwepo?nadhani itakuwa nafasi nzuri amuombe Radhi.mbowe amefikiria vizuri badala ya kuhangaika na uch
ochezi na maandamano yaSiyo na tija.

acha ujrnpa wanaume tu kazin
 
Kama amezaliwa september inakuaje asherehekee Disemba?. Au ni kutafuta sifa?.

Hizi ni sifa za uraisi, hana lolote.

Raisi hawezi kutoka KASKAZINI. Atausikia kwenye bomba.
 
Ni aina ya viongozi ambao ratiba zao zimejaa shughuli zenye tija kwa Taifa na ni shughuli za wazi, sio wale wanaojaza ratiba zao kwa mapango-mkakati ya kimtandao..Tunahitaji viongozi wabunifu, wachapa kazi,wamisionary..ambao kulala na kuamka kwao, wanawaza na kuwazua njia na mbinu mbalimbali za kumkwamua masikini na kumpa hadhi ya utu wenye heshima mama mjamzito,Kijana mjasiriamali,Mtoto yatima, ndugu mlemavu, binti msomi, mtumishi wa umma,baba,bibi na babu wastaafu..Kama yalivyo dhahiri mafuta kwenye maji,vivyo hivyo kwa viongozi Bora; Mawazo, maneno na matendo yao huwatenga mbali na kuwapambanua bayana dhidi ya viongozi wachovu!..Hongera mbowe,Mengi,Sabodo na wengine...Don't u ever get tired of doing the right thing; coz in the end thats what pays off...

Mbowe anafanya kwa ajili ya kutafuta sifa. Mengi nae pia hajitambui, hauwezi utoe misaada wakati unashindwa kuwalipa wafanyakazi wako.

Tunahitaji viongozi wanaofanya kwa ajili ya watanzania. Ila sio wanaotafuta popularty kwa kupitia shida zetu. Huu ni uhuni.
 
Kama amezaliwa september inakuaje asherehekee Disemba?. Au ni kutafuta sifa?.

Hizi ni sifa za uraisi, hana lolote.

Raisi hawezi kutoka KASKAZINI. Atausikia kwenye bomba.

Endelea kumeza hivyo hivyo, ila mziki utakuja uuone 1 day
 
Mbowe anafanya kwa ajili ya kutafuta sifa. Mengi nae pia hajitambui, hauwezi utoe misaada wakati unashindwa kuwalipa wafanyakazi wako.

Tunahitaji viongozi wanaofanya kwa ajili ya watanzania. Ila sio wanaotafuta popularty kwa kupitia shida zetu. Huu ni uhuni.

Nani hajalipwa?? acha umamluki wewe
 
We
quote_icon.png
Mzee inaoneka umepewa traki suti 1 na CCM ukahisi umepewa kabati la suti eeeeeeeeeehhhh!!! CDM hakuna huo upuuzi
 
Raisi hawezi kutoka KASKAZINI. Atausikia kwenye bomba.

Huu ndio upuuzi na propapanda zinazoenezwa na ccm huku wakihubiri kuwa cdm ni chama chenye ukanda

Tafakari, chukua hatua.
 
Kama amezaliwa september inakuaje asherehekee Disemba?. Au ni kutafuta sifa?.

Hizi ni sifa za uraisi, hana lolote.

Raisi hawezi kutoka KASKAZINI. Atausikia kwenye bomba.

Masaburi at work. Kwa hiyo tuongozwe na vichwa vibovu kila wakati? Tuongozwe kila siku na wapiga story? Siku yaja na sasa ipo wakati nchi yetu itakapokombolewa rasmi
 
Mbowe anafanya kwa ajili ya kutafuta sifa. Mengi nae pia hajitambui, hauwezi utoe misaada wakati unashindwa kuwalipa wafanyakazi wako.

Tunahitaji viongozi wanaofanya kwa ajili ya watanzania. Ila sio wanaotafuta popularty kwa kupitia shida zetu. Huu ni uhuni.

Acha fikra zako za kimagamba hapa,
Pendelea sana kushughulisha ubongo badala ya masaburi.
Kama mtu anatafuta sifa katika swala la maendeleo wewe kinakuuma nini?
Anaesheherekea miaka 50 kwa kuwachezesha watu juani mchana ili tu ku-utilize bajeti ya 50Billion na yule anaesheherekea kwa kupanga mikakati endelevu ya maendeleo nana anafaa kuigwa.
Watu wengine mnaishi mpaka sasa kwa sababu tu hatuwajui kwa sura!!!
 
Back
Top Bottom