Hivi mtu unapokuwa mgonjwa na hujaruhusiwa kutoka hospitalini au kuendelea na majukumu yako,kisheria unatakiwa kufanya jambo lolote la kiofisi?

Upinzani hapa tu ndio mnajivua nguo kabisa na hata mnapoteza credibility hivi Swala la lissu nalo ni lakukingia kifua kweli? Mtu ana mwaka na miezi tisa hayupo kazini bila hata taarifa bado mnataka aendelew kubebembelezwa kwanza amevumiliwa sana sana
 
Mahakamani mtakapoulizwa kuzunguka dunia ndio kupona kwa mgonjwa,sijui mtajibu nini!!

Mtakapoambiwa mutoe ushahidi wa daktari kuwa Lissu amepona au anaweza kuendelea na majukumu yake,sijui mtatoa ushahidi gani?!

Pia, mtakapoulizwa mahakamani kupata nafuu na kutoka hospitalini na kisha kutembea hapa na pale ndio uthibitisho wa kupona mgonjwa,sijui mtajibu nini juu ya hili?

Na pia mtakapoulizwa kazi ya kutamka kuwa mgonjwa huyu yuko fiti kuendelea na kazi ni yenu au ni ya daktari,sijui mtakuwa na jibu gani!!
Si jukumu la muajiri kuthibitisha kwamba mfanyakazi wake ana afya ya kutosha kufanya kazi; bali ni jukumu la mfanyakazi mwenyewe kuthibitisha kwamba afya yake haimruhusu kufanya kazi. Hivyo Spika yuko sawa kabisa kumsimamisha kazi Lissu mpaka atakapothibitisha mwenyewe kwa kuambatanisha maelezo ya daktari kwamba hakuweza kuhudhuria kazini.
 
Ndo shida yetu huwa inaanzia hapo! hivi upande wa pili umesha jibu hivyo vioja vya jamaa yetu dhaifu?

Vioja kwasababu hizi
A. Alipigwa risasi akiwa kazini akitekeleza majukum yake kikatiba. Na ilitakiwa mwajiri wake achukuwe majukum yote kuhakikisha anapona (yaani Bunge)

- spika alikuwepo

- wahudumu wa bunge walikuwemo

- wajumbe wa kamati za bunge walikuwepo

2. Makamu wa rais alifika kumjulia hali huko Kenya akisema alitumwa na rais

3. Ndugai aliahidi kumtembelea Mgonjwa

4. Bunge chini ya ndugai mwenyewe limeweza kumlipa mishahara na stahiki zingine zote kwa muda wote.

Maswali yakujiuliza

1. Wagonjwa wa akili au psychology disturbances wanasafiri? Au kunakifungu cha sheria kinasema wasisafiri......kivipi?

2.Kwanini mtu anapoapa anasema NIKIWA NA AKILI TIMAMU....je kupigwa lisasi zote hizo kunaweza kusababisha psychology problem kwa Lisu? Kama ndio lini kathibitishwa kupona?

3. Nani kuthibitisha utimamu au kupona kwa mgonjwa? wanasiasa au madakitari wa fani husika? Nani kathibitisha Lisu kapona? Kupitia ushahidi wa dakitari gani? Wapi? Lini?

4. Dakitari anaweza kukushauri ufanye nini kwa mazingira gani? Mfano mwaume ukifanyiwa operation kubwa unaambiwa usifanye ngono Miezi sita......nk nani kuthibitisha kwa tatizo la Lisu ni salama kurudi Tanzania

A. Miundombinu
-vitanda
-viti
-barabara
- vyombo vya usafiri

B. Uharaka wa kufikia matibabu halisi kutoka Dsm kwenda ulaya?

C. Waliomkosa/waliotaka kumuuwa mpaka Leo hawajakamatwa nini kinaendelea?

B. Kiakili kulingana na hofu ya mazingira je Lisu yupo teyari kukabiliana na mazingira halisi alipopigwa risasi?

Ukitafakali kwa jicho la tatu..... Ndugai kazua vioja na niviroja kwelikweli, hakuna hoja alizotoa zaid ya ujinga na Upumbavu.
 
Unajua maana ya kupewa discharge letter?

Kwa akili zenu,hata mgonjwa anaefanya mazoezi ya kutembea maeneo ya jirani na nyumbani kwake kwa maelekezo ya daktari au kuhudhuria mazoezi yanayosimamiwa na daktari ila hafiki kazini mtu huyo kwa akili zenu ni mtoro kazini na amepona kabisa!!!
kwa hyo kutoka ubelgiji mpaka uingereza ndo alikuwa anafanya mazoez ya jiran na kwake?

Mkuu hebu jikague kwanza kama uko sawa
 
Mahakamani mtakapoulizwa kuzunguka dunia ndio kupona kwa mgonjwa,sijui mtajibu nini!!

Mtakapoambiwa mutoe ushahidi wa daktari kuwa Lissu amepona au anaweza kuendelea na majukumu yake,sijui mtatoa ushahidi gani?!

Pia, mtakapoulizwa mahakamani kupata nafuu na kutoka hospitalini na kisha kutembea hapa na pale ndio uthibitisho wa kupona mgonjwa,sijui mtajibu nini juu ya hili?

Na pia mtakapoulizwa kazi ya kutamka kuwa mgonjwa huyu yuko fiti kuendelea na kazi ni yenu au ni ya daktari,sijui mtakuwa na jibu gani!!

kupona siyo hoja

je sheria inasemaje ikiwa unaumwa unatakiwa ufanye nini kulingana na sheria ya ajira??

Jibu :unajaza sick sheet unaituma officine kwa bosi wako!! Na kwenye sick sheet waweza kuandikiwa kuwa umelazwa au light duties au ED( exception of duties)!!
Swali ni je Lissu au ndugu zake au mwanasheria wake walifanya hivyo???
 
Najiuliza,hivi kwa sheria za nchi yetu hasa zinazohusu utumishi wa umma na kwa mujibu wa taratibu za kitabibu,mtumishi wa umma ambae yuko katika matibabu either akiwa amelazwa au anahudhuria matibabu huku akiwa anatokea nyumbani baada ya kulazwa na hana discharge letter kutoka kwa daktari,mtumishi wa aina hii anaweza kuadhibiwa kwa kutofika kazini au kutotimiza jukumu lolote la kiofisi kama kujaza form ya maadili?

Yaani kwa mfano leo hii mtumishi mwenye wadhifa unaomtaka ajaze form ya maadili na bahati mbaya akapata ajali na kulazwa Muhimbili na baada ya muda akaruhusiwa kwenda nyumbani huku akiendelea na matibabu kama mgonjwa wa nje,mtumishi huyu anaweza kuwajibishwa kwa kutokukamilisha majukumu fulani ya kiofisi ili hali bado yuko kwenye matibabu na bado afya yake haimruhusu kurudi kazini?

Kwa maneno mengine,ukiwa mgonjwa na afya yako haikurusu kurudi kazini au kurudi nchini kuendelea na majukumu yako,unaweza kutumiwa nyaraka yoyote ya kiofisi isohusiana na matibabu yako uifanyie kazi?

Na kwa anaetibiwa nje ya nchi sio ndio kabisa?

Alafu sijui walitaka Lissu aingie Bungeni na machuma miguuni!!!!
 
Mahakamani mtakapoulizwa kuzunguka dunia ndio kupona kwa mgonjwa,sijui mtajibu nini!!

Mtakapoambiwa mutoe ushahidi wa daktari kuwa Lissu amepona au anaweza kuendelea na majukumu yake,sijui mtatoa ushahidi gani?!

Pia, mtakapoulizwa mahakamani kupata nafuu na kutoka hospitalini na kisha kutembea hapa na pale ndio uthibitisho wa kupona mgonjwa,sijui mtajibu nini juu ya hili?

Na pia mtakapoulizwa kazi ya kutamka kuwa mgonjwa huyu yuko fiti kuendelea na kazi ni yenu au ni ya daktari,sijui mtakuwa na jibu gani!!
Mgonjwa ataambiwa awasilishe Barua ya kulazwa.
Itatolewa discharge form.
Mmesahau kuwa mlisema Kesha ruhusiwa kutoka hospitali.
 
Jokes aside, hutakiwi kujishughulisha na mambo ya ofisi wakati una leave ya hospitali
Sick leave with pay Ni miezi 6. Baada ya hapo unalipwa nusu mshahara.
Ikiisha jopo linaketi kujadili uwezo wako was kuendelea na kazi.
Kesi hii itaenda cma.
 
Najiuliza,hivi kwa sheria za nchi yetu hasa zinazohusu utumishi wa umma na kwa mujibu wa taratibu za kitabibu,mtumishi wa umma ambae yuko katika matibabu either akiwa amelazwa au anahudhuria matibabu huku akiwa anatokea nyumbani baada ya kulazwa na hana discharge letter kutoka kwa daktari,mtumishi wa aina hii anaweza kuadhibiwa kwa kutofika kazini au kutotimiza jukumu lolote la kiofisi kama kujaza form ya maadili?

Yaani kwa mfano leo hii mtumishi mwenye wadhifa unaomtaka ajaze form ya maadili na bahati mbaya akapata ajali na kulazwa Muhimbili na baada ya muda akaruhusiwa kwenda nyumbani huku akiendelea na matibabu kama mgonjwa wa nje,mtumishi huyu anaweza kuwajibishwa kwa kutokukamilisha majukumu fulani ya kiofisi ili hali bado yuko kwenye matibabu na bado afya yake haimruhusu kurudi kazini?

Kwa maneno mengine,ukiwa mgonjwa na afya yako haikurusu kurudi kazini au kurudi nchini kuendelea na majukumu yako,unaweza kutumiwa nyaraka yoyote ya kiofisi isohusiana na matibabu yako uifanyie kazi?

Na kwa anaetibiwa nje ya nchi sio ndio kabisa?

Alafu sijui walitaka Lissu aingie Bungeni na machuma miguuni!!!!
Umeandika maelezo marefu na mazuri nilidhani unazungumzia suala la kiutumishi wa Umma nikajiandaa kuelezea facts kwa mujibu wa utumishi wa Umma. Lakini mwishoni naona umemalizia na habari za Tundu Lissu nikaona nikae kimya maana masuala ya kibunge/siasa hayaendani na Utumishi wa Umma. Basi kwa hilo wataalamu ngoja waelezee.

KWA ISHU YA KIUTUMISHI WA UMMA
Kwa mfano ulioutumia wewe... mtumishi wa Umma anayetakiwa kujaza fomu hususani ipo Fomu ya Maadili ya Mtumishi wa Umma/ Kiongozi ni lazima ujaze na kuiwasilisha haijalishi uko wapi. Lakini ifahamike kwamba mara baada ya kuijaza na kusaini popote ulipo unao uwezo wa kuiwasilisha kwa njia yoyote iwe kwa mkono au kwa posta au EMS kadri itakavyofaa. Hivyo kwa mfano ulioutolea wewe hata kama uko nje ya nchi unao uwezo wa kujaza na kuituma kwa njia yoyote ile. Vivyo hivyo ipo pia Fomu ya Tamko la Mali na Madeni kwa viongozi pia ukishajaza na kusainiwa haikuzuii kuiwasilisha katika Mamlaka inayohusika kwa njia yoyote ile.

Kwa hiyo kwa hili hakuna kiteteo kwamba nilikua ninaumwa au nilikua na ruhusa ya kuumwa hivyo siwezi kujaza fomu hiyo inakuwa sio hoja ya msingi kwa sababu unao uwezo wa kujazia nyumbani na kisha kumwagiza mtu.

Kwa upande wa Kutakiwa kufanya kazi huku ukiwa na ruhusa ya ugonjwa sio sahihi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma. Lakini ni lazima ujiridhishe kwamba unavyo vielelezo vinavyothibitisha kwamba unaumwa kwa Mfano lazima kuwe na ripoti ya Daktari (seek sheet) inayothibitisha kwamba unaumwa na unaendelea na matibabu na kwa hali yako hutakiwi kuendelea na majukumu. Na taarifa hiyo ya Daktari lazima imfikie mwajiri ili ajue nini Dakatari ameshauri. Endapo baada ya muda ambao Daktari alishauri upumzike umeisha utatakiwa kurudi kazini na endapo Daktari ataona inafaa uongezewe muda atatakiwa kuandika ripoti hiyo tena na kisha utatakiwa kuiwasilisha kwa mwajiri hadi hapo utakapopona. Ukishindwa kuwasilisha uthibitisho wa Daktari juu ya mwenendo wa afya yako na kuamua kukaa nyumbani basi utahesabika mtoro kama watoro wengine hata kama uko hoi kitandani, kwa sababu hiyo ripoti ya Daktari ikishajazwa unao uwezo hata wa kumwagiza mtu endapo hali yako sio nzuri kuweza kufika kwa mwajiri.

Huu ni ufafanuzi ki Utumishi wa Umma.
 
Back
Top Bottom