Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,086
- 144,523
- Thread starter
- #21
Mpaka hapa ujue tu Lissu ameshawashinda.Sheria ya utumishi wa umma iko wazi kabisa kwamba kama ukikosekana kazini kwa siku tatu mfululizo bila taarifa unakuwa umejifukuza kazi. Kama ulilazwa hospitali na baadaye ukaruhusiwa lakini daktari anaona bado huwezi kurudi kazini, atakupa barua ya kusema ulilazwa kuanzia siku fulani hadi siku fulani na sasa umetoka hospitali lakini unahitaji kupumzika nyumbani kwa siku kadhaa kabla ya kurudi kazini. Bila barua kama hiyo utakuwa umejifukuzaa kazi na wala si jukumu la muajiri kutafuta barua hiyo kutoka kwa daktari. Ni juu yako wewe mwenyewe kupeleka barua hiyo.