Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,232
- 113,610
Miaka takribani arubatashara iliyopita tukakutana pale uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ivato, jijini Antananarivo kisiwani Malagasi.
Wote bado tulikuwa washababi na watanashati wenye nyuso zilizojaa furaha na bashasha.
Wewe hukuwa na shaka na usharafu wangu nami vivyo hivyo sikuwa na shaka na wa kwako.
Tumepitia mengi, njia tambarare, milima, pamoja na mabonde.
Nini kilichokusibu ghafla umebadilika? Wewe hutaki kuambiwa. Hutaki kusemwa.
Unashawishika na mambo madogo. Unashawishika na vitu vidogo.
Hivi kwa nini? Kwa nini watu hubadilika na kuwa kama siyo wao tena?