Hivi Jack Pemba ni tapeli?

Jack Pemba ageukia urembo

na Dina Zubeiry
KAMPUNI ya Global Scouting Bureau (GSB), imetoa tiketi nne kwa Kamati ya Miss Tanzania kwenda na kurudi Poland kumshangilia mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Miss World, Wema Sepetu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye Mgahawa wa Hadees, Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa GSB, Jack Pemba alisema kwamba tiketi moja kati ya hizo atapewa mwandaaji wa Kitongoji cha Dar Indian Ocean, Mange Kimambi.
Pemba alisema kwamba atagharamia safari ya Mange katika bajeti nyingine na akatoa dola 7,500 (sawa na sh 9,750,000) kwa wanakamati hao zilizopokelewa na Mkurugenzi wa kamati hiyo, Hashim Lundenga. Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Septemba 30.
Pemba alisema hatua hiyo inatokana na kuunga mkono wito uliotolewa na Mkurugenzi wa Kituo vha Uwekezaji Tanzania (TIC), Emmanuel ole Naiko, kuomba wadau mbalimbali kuchangia jitihada za kwenda kumuunga mkono Miss Tanzania.
"Pia ni uzalendo nilionao pamoja na kuthamini sanaa hii ya urembo ambayo inakua kwa kasi. Naomba watu na mashirika mengine wajitokeze kudhamini kwa namna moja ama nyingine," alisema.

source: freemedia.co.tz
Jack Pemba, wema, mange, connecting the dots...
 
Hii vita ya donhosnoop na Stanley Mitchell tamu sana wakuu. Macho yangu yapo hapa nataka kujua nani atachukuwa ubingwa.



Ndukiiiii
 
Back
Top Bottom