Hivi inawezekanaje mtu huna kazi bado unasoma Master's Degree?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,465
17,307
Wakuu habari za Jumapili,

Niseme, mwaka huu 2023 nimehitimu Shahada ya Umahiri ama Master's Degree kwenye fani ya uchawi na ushirikina chuo kikuu.

Kwenye kuisoma hiyo fani, kilichonishangaza sana na bado nazidi kushangaa ni kuona vijana wakisoma Shahada za Umahiri huku hawana kazi.

Najiuliza, kwa hapa Tanzania kazi zinazotangazwa zinazotaka mtu awe mahiri ni kazi ambazo lazima uwe na uzoefu usiopungua miaka 8 na kuendelea na mara nyingi kama sio zote hua ni managerial positions.

Sasa kama Shahada ya awali haijakupa kazi, haijakusaidia kupata kazi, unawezaje kwenda kusoma Shahada nyingine ya juu zaidi huku huna kazi?

Kwa mtazamo wangu, wazazi wanapoteza pesa nyingi sana kusomesha watoto wao Master's Degree ambazo wangezitumia kuwafungulia miradi ya ujasiliamali na wakapata pesa.

Leo kukuta kijana yuko mtaani na anaendesha bodaboda na ana Master's Degree ni kitu cha kawaida, unajiuliza hiyo pesa ya Master's Degree zaidi ya 10m na 2+years za kusoma, angeanza kua bodaboda si angekua mbali sana, kwanza angekua na bodaboda 5 ambazo zinamuingizia wastani wa 1.2m kwa mwezi, miaka 2 angekua na 25m+ na bado bodaboda zake ziko pale pale.

Juzi nimeenda na girlfriend wangu mahala kwa tailor, nikakuta tailor katika mazungumzo anasema ana Master's Degree ya Accountancy halafu ni fundi nguo, yeye mwenyewe anajilaumu kusoma Master's Degree bora angeaza ushonaji mapema angekuwa mbali.

Master's Degree bongo zinasomwa kwa kujifurahisha?
 
Kama kuna kosa tunalifanya ni kuendelea kuidharau elimu. Someni kama kuna fursa ya kufanya hivyo...ili hata msipoajiliwa muweze kuweka ubora kwenye shughuli zingine mnazozifanya.
Tumekuwa tukidharau kazi za mikono kuwa ni za watu wasio na elimu lakini ukweli ni kwamba ajira nyingi zitapungua hivyo tegemeeni kazi za suluba kuwa kimbilio la wasomi wengi.
Sijui mnautazamaje ujio wa robots and AI technology nyie wasomi.
 
Back
Top Bottom