Hivi inakuaje

NATA

JF-Expert Member
May 10, 2007
4,492
1,311
Na unajisikiaje kutupa taka hovyo

Jana nimeshuhudia MJbaba mmoja yuko kwenye gari moja bomba kafungua dirisha karusha uchafu nje tena katikati ya barabara ya kinondoni

Hivi hatuwezi kubadilika?
Naomba serikali ikajifunze Moshi jamani hii ni kero kubwa.
Inaniuma sana nikiona mtu anatupa hovyo uchafu tubadilike
 
Kwa kweli siku zinavyozidi kwenda ndivyo Dar inavyozidi kuwa chafu.
Ustarabu ni kitu cha bure acha kutupa taka hovyo ufurahie mazingira masafi.
 
inabidi sheria kali ziwekwe,KAMA KWETU MOSHIII,kwakweli nikienda huko heshima inaongezeka
yani wakikuona unadalili za kutupa taka , wagambo wanakufwata nyumanyuma kama fisi ameona mfupa
ukutupa tu haaaaa uwe na kitambi hammer au una makalio manene ,utakiona cha mtema kuni,
nadhani wagambo wa dar badala ya kuwadhulumu wamachinga na akina mama ntilie wangeongeza
nguvu zao kwenye kuwasaka wachafuzi wa mazingira<wakitandikwa hata viboko v3 makalioni watatia akili
,manake moshi tumeshawahi kushushwa kwenye bus wooote tukafagia barabara ndo tukaendelea na safari
kila mtu anamlinda mwenzie atiiii :pound:!!!!!!!!!!!
 
Nimeipenda sana hii, fagio mlipata wapi?
 
Inabidi wanunue mini-dustbins ziwe kwenye gari, ukiona hivyo ujue hana ustaarabu hata wakwake binafsi.
 
Yaani hapo umenikumbusha jana niliweka uchafu wa karatasi kwenye gari nikawa natafuta mahali pa kutupa kila ninapotaka kutupa najisikia vibaya hadi nimeacha mpaka leo sijatoa! yaani watu wengine sijui wakoje wanatupa uchafu popote, wengine wanatema mate popote yaani hadi kinyaa. Kwani ustaarabu wa Moshi hauwezi kuwekwa kila mkoa?
 
Hivi si kuna kipindi nilisikia watu kutoka manispaa wamepelekwa MOSHI kwenda kujifunza usafi?

hawakujifunza kitu au ndio ilikua dili la kujipatia per diem?
 
Yaani hapo umenikumbusha jana niliweka uchafu wa karatasi kwenye gari nikawa natafuta mahali pa kutupa kila ninapotaka kutupa najisikia vibaya hadi nimeacha mpaka leo sijatoa! yaani watu wengine sijui wakoje wanatupa uchafu popote, wengine wanatema mate popote yaani hadi kinyaa. Kwani ustaarabu wa Moshi hauwezi kuwekwa kila mkoa?

Hata mimi najiuliza hili, ingekuwa bora kabisa
 
Back
Top Bottom