Hivi hili jina Mwendazake wanalomuita Magufuli ni official?

Sambinyakwe kitololo

JF-Expert Member
Nov 15, 2022
2,420
2,880
Leo nimesikitika Sana watangazaji kutokuwa na weledi na kazi yao

Asubuhi ya leo nipo najiandaa kutoka radio ilikuwa inaongea (east Africa radio) kipindi wanakiita Mama Mia ,Rita chiwalo ndo mtangazaji alikuwa na mwezie Wakawa wanajadili maswala ya CAG Mara katika malumbano mmoja akasema mbona MWENDAZAKE magufuli aliwahi weka wazi mshahara wake?

Akatamka kabisa neno MWENDAZAKE mida ya sa 09:32

Sasa nauliza Hilo jina ni official Hadi mtangazaji amuite marehemu mwendazake?
 
Limekaa kikejeli sio official.. Mbona mkapa hakuitwa hivyo wala Nyerere??

Wauni walimtungia Hilo Jina likawa kama msimu Sasa watu washaanza kuzoea
Kaulize BAKITA. Neno mwendazake ni sahihi na wala sio kejeli sema kwa Magu linavuma sana kutokana na ukatili wake na tabia yake ya kuendesha nchi kibabe bila kufuata katiba na sheria za nchi. Lakini yule Dialo akaongezea tena neno eti nchi iliongozwa na kichaa.
 
Tunahitaji walimu watufundishe kiswahili humu JF!Kwani wakitamka hilo neno "MWENDAZAKE" unapata picha gani?Kwamba:
  • Aliondoka kwa kutoroka bila kuaga?
  • Aliamua aende zake tu bila mpango?
  • Alifukuzwa akajiondokea zake?
  • Alichukia tu akaamua aondoke zake?
NB: Ni neno la kiswahili lenye maana ya marehemu au mtu aliyefariki. Lakini, kama unaona haulipendi, unaweza kutumia lingine lifaalo.
 
Leo nimesikitika Sana watangazaji kutokuwa na weledi na kazi yao

Asubuhi ya leo nipo najiandaa kutoka radio ilikuwa inaongea (east Africa radio) kipindi wanakiita Mama Mia ,Rita chiwalo ndo mtangazaji alikuwa na mwezie Wakawa wanajadili maswala ya CAG Mara katika malumbano mmoja akasema mbona MWENDAZAKE magufuli aliwahi weka wazi mshahara wake?

Akatamka kabisa neno MWENDAZAKE mida ya sa 09:32

Sasa nauliza Hilo jina Ni official Hadi mtangazaji amuite marehemu mwendazake?
Mwendazake maana yake ni marehemu, ni neno rasmi la Kiswahili
 
Leo nimesikitika Sana watangazaji kutokuwa na weledi na kazi yao

Asubuhi ya leo nipo najiandaa kutoka radio ilikuwa inaongea (east Africa radio) kipindi wanakiita Mama Mia ,Rita chiwalo ndo mtangazaji alikuwa na mwezie Wakawa wanajadili maswala ya CAG Mara katika malumbano mmoja akasema mbona MWENDAZAKE magufuli aliwahi weka wazi mshahara wake?

Akatamka kabisa neno MWENDAZAKE mida ya sa 09:32

Sasa nauliza Hilo jina Ni official Hadi mtangazaji amuite marehemu mwendazake?
It's not fair
 
Katizame kwenye kamusi, au nenda Bakita waulize, mwendazake maana yake ni marehemu ni neno rasmi kabisa
Na akiwasikiliza watu wa Kenya,huwa wanalitamka kwa mbwembwe sana.Hasa wa kule Lamu,Malindi na Mombasa.Wamelizoea.Ni mfano tu wa maneno mengi yatumiwayo sehemu moja tofauti na kwingine.Itoshe kueleza kwamba,bado tuna kiswahili cha mazoea yetu au cha eneo tulilozoea.Tusijifungie.Tujifunze zaidi.
 
Mbona mkapa haiitwi?
Nyerere haitwii?
Why only JPM?
Inategemea tu na muitaji au mtamkaji.Mwingine ana msamiati mmoja tu wa marehemu.Mwingine anayo miwili tu.Marehemu na hayati.Halafu,kuna mwingine anayo misamiati zaidi ya miwili.Yaani marehemu, hayati, aliyetutoka, aliyetangulia, mwendazake, aliyependwa zaidi na BWANA nk.Huyo wa mwisho ana utajiri wa misamiati na anaamua atumie upi!Hata hivyo,hao wote tunaweza kuwaita kwa kutumia misamiati hiyo yote bila ubaguzi.Wigwa mwichane?
 
Inategemea tu na muitaji au mtamkaji.Mwingine ana msamiati mmoja tu wa marehemu.Mwingine anayo miwili tu.Marehemu na hayati. Halafu, kuna mwingine anayo misamiati zaidi ya miwili. Yaani marehemu, hayati, aliyetutoka, aliyetangulia, mwendazake, aliyependwa zaidi na BWANA nk. Huyo wa mwisho ana utajiri wa misamiati na anaamua atumie upi! Hata hivyo, hao wote tunaweza kuwaita kwa kutumia misamiati hiyo yote bila ubaguzi. Wigwa mwichane?
Wigwaga😂
 
Back
Top Bottom