Hitimisho kwenye kipimajoto itv jana usiku: Polisi wajitathmini kwanini wana vitambi?

GlorytoGod

Senior Member
Sep 8, 2012
158
50
Katika kuhitimisha mjadala uliokuwa unahusu maandamano katika kipindi cha kipimajoto ITV, Mdau mmoja alihitimisha kwa kuwaomba polisi wajitathmini ni kwanini wana vitambi? maana katika kila mauaji yanayotokea nchini yanahusishwa na polisi pale wanapotumiwa na wanasiasa haswa haswa hawa wa nyinyiem, je ni kweli vitambi vya polisi vinaletwa na hela isiyo safi? maana walitolea mfano cuf kipindi inavuma wanachama wake wengi walivyouwawa na polisi kule zanzibar, na sasa imeahamia chadema, je polisi ni kweli vitambi vya polisi ni vya hela chafu?
 
ITV nao wameshakua propaganda tool ya hawa wasaka ulaji a.k.a wanasiasa.
Haiwezekani kila siku wanastick kwenye hoja hizohizo hadi wanaboa.
 
Asilimia kubwa ya vitambi huwa ni diet tu, mtu anajioverfeed tu pasipokuwa na plani nzuri ya kula. Vitambi vya polisi wengi siyo kutokana na pesa chafu ni kwamba hawana mazoezi ya mara kwa mara na wamekosa ya ratiba ya kula na mwisho hawana cha kufanya kama kubrainstorm juu ya inteligenzia ya ulinzi wa ndani wa nchi na nini kifanyike kama wizi mkubwa, kupambana na majambazi, masuala ya mipakani-uhamiaji, wapo kwa ajiri ya kukabiliana na maandamano na mikutano ya vyama vya siasa tu!
 
Uozo ntupu. Kuna nchi rais wao alisema atawatimua mapolisi wote wenye vitambi. Uganda?
 
kuna uhusiano gani kati ya vitambi na kazi ya polisi mtu anaweza kuwa mnene na akawa mwepesi kutekeleza wajibu wake mbali na hilo hakuna sheria TANZANIA INAYOMKATAZA POLISI KUWA MNENE
 
Kwani wenye vitambi ni plice tu, au hela chafu ziko kwa police tu. Mbona kuna watu hap nchini wanakula hela chafu tena nyingi..............
 
Back
Top Bottom