Habibu B. Anga
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 6,557
- 25,671
- Thread starter
- #101
Huyu jamaa atakuwa alikuwa Jasusi sio bure, atakuwa alikuwa anatumika hata hizo taasisi kujipatia fedha maana CIA ndio mtindo wao. Elimu nzuri, mafunzo maalum jeshini, mafunzo ya mapigano. Mpaka hapo alikuwa tayari ameshatoka kimaisha, ilikuaje aka risk maisha kuvamia mabenki? Labda unishawishi kupitia muendelezo ujao, lakini mpaka sasa naamimi kulikuwa na watu/taasisi nyuma yake ikimtumia, na ndio imekuwa msaada kwake kutokamatwa na FBI miaka yote 30
Binadamu ni viumbe wa ajabu mkuu, Carl alihisi kuwa jambazi ndio destiny yake! Pia akiwa anahojiwa na FBI aliwaeleza kuwa ile rekodi yake ya kufungwa jela miezi 18 akiwa mtoto hakujua kuwa zile rekodi zinakuwa expunged baada ya muda fulani! Yeye aliamini hiyo rekodi ingekaa maisha yake yote na asingeweza kuajiriwa sehemu yoyote yenye staha..Kabisa! Kama ni kweli alikuwa mtu wa CIA asingekamatwa kamwe.. Ishu ingeishia juu kwa juu kusingekuwa na ulazima wa kumu-expose hivi..