Mangungu apumzishwe, imetosha

Underwood

JF-Expert Member
Dec 25, 2020
1,909
3,104
Labda sikumbuki ni darasa gani hasa, au mada gani, lakini nakumbuka kwamba, kabla ya wakoloni wa kizungu kuja na kuweka misingi yao katika ardhi ya hapa kwetu Afrika Mashariki walitanguliwa na wapelelezi wao kama David Livingstone na Henry Morton Stanley.

Kati ya wapelelezi hao wote (kwangu binafsi) hakuna aliyeonekana kuwa katili, mwenye shauku na tamaa kama Mjerumani Carl Peters almaarufu “mkono wa damu”.

IMG_8234.jpg

Carl Peters (kulia).

Mwaka 1884, ndani ya kipindi cha muda wa wiki sita, akipitia mto Wami, kwa niaba ya kampuni yake ya GEACO, Carl Peters aliwasainisha mikataba ya kilaghai Machifu wengi wa maeneo ya pwani ambao walitakiwa kusaini huku wakiwa na uelewa hafifu kuhusiana na vipengele vya mikataba husika iliyokabidhi maeneo ya himaya zao kwa Carl Peters aliyekuwa akiiwakilisha kampuni ya GEACO.

Miongoni mwa mikataba hiyo, mkataba kati ya Chifu Mangungu wa Msovero na Peters huko Usagara ndio mkataba maarufu zaidi ambapo Chifu Mangungu (kwa kujua au kutokujua) alikabidhi eneo lake lote la himaya yake kwa Carl Peters na GEACO milele, bila kuwepo kwa kipengele chochote cha kuvunja mkataba, ndiyo, MILELE.

IMG_8233.png

Ramani kuonyesha eneo lote la GEACO lililopatikana baada ya mikataba ya kilaghai.

Katika elimu ya hapa kwetu Tanzania, mkataba wa Chifu Mangungu umekuwa ukitumika kuonyesha ni kwa namna gani ujinga na ukosefu wa elimu kwa ujumla unavyoweza kumuangamiza mtu na jamii kwa ujumla huku Chifu Mangungu akiwekwa kwenye kundi la machifu wa hovyo, waoga na wajinga tofauti na wenzake kama Mirambo, Mkwawa na Meli kwa sababu alisaini mkataba wa kilaghai na Wajerumani.

Lakini sote tunafahamu, bila shaka, Chifu Mangungu hakuwa amepata elimu ya shuleni, au alijua hata kusoma kiingereza au kijerumani wakati wa kutia saini nyaraka za mkataba. Pengine wakati wa kutia saini mikataba, Chifu Mangungu alilazimika kufanya hivyo mbele ya mtutu wa bunduki.

Kwa kuusoma mkataba wa makubaliano ya uendeshaji wa bandari kati ya serikali yetu na kampuni ya Dubai, DP world, kwa kutazama nguvu inayotumika kuuhalalisha licha ya viashiria vyote vya mkataba kutufunga zaidi sisi kama taifa, huku kukiwa umilele kwenye mkataba wenyewe, naiomba serikali imuondolee Chifu Mangungu kivuli cha aibu yote anayopatiwa kwenye mitaala yetu ya elimu.

Naamini, kwa Chifu Mangungu upo utetezi wenye nguvu juu ya mkataba wake na kampuni ya GEACO kuliko utetezi wa serikali juu ya mkataba wake na DP World!

Kama Yuda Iskarioti alivyogeuka kuwa picha wakilishi ya usaliti ulimwenguni pote, baada ya kumsaliti Yesu wa Nazareti, elimu yetu pia imemfanya Chifu Mangungu kama picha wakilishi ya mikataba yote ya kilaghai ambayo mtu anaweza kujiingiza.

Nadhani kwa sasa tuna picha wakilishi halisia zaidi kuliko Chifu Mangungu. Kwa heshima ya muhenga wetu huyu, ambaye hatujui alitia saini kwenye mkataba kati yake na GEACO katika mazingira gani, tumuondolee taswira hii ya aibu na tuiweke serikali yetu yenye wasomi wa kada ngazu mbalimbali katika madaraja tofauti tofaut, inastahili.

.
 
View attachment 2676010

View attachment 2676012

Ok
 
"Blacks are born with a sense of a half-mad mindset and self esteem".
By Jan Smuts
 
Kama mkataba ulikuwa wa milele, je kampuni ya Carl Peters bado inamiliki hiyo Ardhi? na kama jibu ni hapana ni kwa nini?
 
Vizazi vijavyo vitamsoma Chifu Hangaya Kwa kusaini mkataba wa kilaghai na DP World.
 
Kama mkataba ulikuwa wa milele, je kampuni ya Carl Peters bado inamiliki hiyo Ardhi? na kama jibu ni hapana ni kwa nini?
Ujeruman iliposhindwa vita kuu ya kwanza ya dunia 1918,Tanganyika ikawekwa chini ya Uingereza kwa udhamini wa Jumuiya ya mataifa .Mikataba yote na Wajerumani ikawa invalid.Tulipopata uhuru wa bendera 1961 na Kisha kuwa Jamuhuri 1964 mikataba yote ya kikoloni ilikoma kuwa na nguvu Tena.Mahusiano yaliyobaki hadi ni yale aliyoyaita Nkrumah ,Neo colonialism na Nyerere akayaita Ukoloni Mamboleo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom