Historia itakukumbuka Mbowe kwa kuyasaliti Mageuzi

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015, CCM ilikuwa imevurugika kwa mgogoro wa ndani kwa ndani na kulikuwa na tishio la kugawanyika pande mbili na moja ya mambo yaliyowashangaza wengi ni uamuzi wa CHADEMA chini ya Mwenyekiti Mbowe kumpokea Edward Lowassa na kumfanya mgombea uraisi. Hapo hapo muungano wa vyama vya upinzani ukafa rasmi huku kiongozi muhimu wa CHADEMA Wilbroad Slaa akijitenga na chama.

Lowassa hakuhama na wimbi la vigogo wa CCM. Badala yake uamuzi ule ulirudisha amani ndani ya CCM na kuwarudisha kuwa kitu kimoja na ilipelekea ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu.

Wengi wanaweza kuongelea kura nyingi na wabunge wengi ambao CHADEMA ilipata kuliko kipindi kingine chochote ila faida hiyo haikudumu hata miaka 5 maana kuna wengi, ikiwemo Lowassa mwenyewe waliamua kuunga mkono juhudi na kurudi CCM. Unaweza kusema "in the long term", CHADEMA walipoteza zaidi ya kupata kwa uamuzi ule wa 2015.

Madhara yake CHADEMA kilionekana ni chama ambacho hakina misimamo, kilionekana ni chama cha walaghai, chama kinachoweza kununulika. Lebo hii itaendelea kukiandama chama siku zote za maisha yake.

Baada ya kifo cha Rais John Magufuli, CCM ilikuwa kwenye hali mbaya sana kisiasa. Mazingira ya kifo chake yalichagiza uwezekano wa mtifuano mkubwa ndani ya chama. CHADEMA walipata ahueni kutokana na kuondoka kwa mtesi wao ila wakati huo huo Rais Magufuli bado alikuwa na wafuasi wengi ndani ya CCM. Wale vigogo ambao Magufuli alionekana wazi kuwapinga ndani ya chama walionekana kurudi kwa kasi na mgawanyiko mkubwa ulikuwa unajongea ndani ya CCM. Mwenyekiti Mbowe kwa mara nyingine akawa mfariji na mwokozi wa CCM. Mbowe kupitia maridhiano akakiongoza CHADEMA kufanya maamuzi ya kuituliza CCM na mpaka leo CHADEMA inatumika kama nyenzo ya kuangamiza maadui ya wale wanaoiongoza CCM kwa sasa.

Naelewa CHADEMA iliumizwa sana kipindi cha 2015-2021. Wanachama wake ikiwemo viongozi walikuwa na madai mengi ikiwemo madai binafsi ya kudhulumiwa na kuharibiwa biashara zao. Bila kuonyesha ni jinsi gani wale waliotenda ubaya na kuvunja katiba na sheria za nchi wamewajibishwa (au kujitokeza rasmi na kukiri makosa yao na hatimaye kujiuzulu nyadhfa zao), maridhiano yoyote yanayoendelea ni ulaghai tu.

Siasa za kukikumbatia chama tawala hazijawahi kuwa njema katika mustakabali wa kutetea demokrasia na utawala bora. Siasa za namna hii siku zote zimekuwa siasa zinazofanywa na mapandikizi, walaghai na wale wasio na nia njema ya kutetea haki na uwajibikaji.

Bila mashinikizo ya kisiasa, CCM haiwezi kamwe kuleta mabadiliko ya msingi ya kisiasa na kiutawala katika nchi. Inapotokea nafasi za kipekee za kufanya mashinikizo hayo halafu mtu anakuja kukimbilia "maridhiano" badala ya kutake advantage ya hali mbaya ya kisiasa ndani ya chama tawala, wanamageuzi wengi tunaanza kutilia mashaka uadilifu wa baadhi ya viongozi wa CHADEMA tukianzia na Mwenyekiti Mbowe.

Ahadi za katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na mabadiliko ya kweli ya kisiasa, kiutawala na nyanja nyingine kama elimu na uchumi haziwezi kamwe kutimizwa kwa njia hizi tunazoahidiwa.

Mwenyekiti Mbowe, kwa maamuzi uliyoyasimamia kipindi hiki cha miaka 8 iliyopita, historia itakuhukumu vibaya kama msaliti wa mageuzi ya nchi hii.
 
Sukuma Gang bana ,si muanzishe chama chenu ?kwani nini tu mbowe ?
 
Haya yote ni kutokana na wananchi kutojitambua wewe mchango wako ni upi? Aliandamana kinondoni Hadi kufungwa wewe ulikuwepo, kakamatwa Mwanza issue ya katiba wapi kakaa gerezani siku kibao. Siasa zinabadilika kutokana na utawala uliopo
 
Maridhiano maana yake Ni compromise..yaani mnakubaliana Kila mtu kukubali kupoteza au kupunguza baadhi ya misimamo au vitu au misingi ili mkutane katikati..

Na Mimi Nina wasiwasi na matokeo ya compromise.. lakini naona tuwaache CDM wapate angalau nusu na wapoteze nusu kuliko kupoteza kilakitu Kama kipindi Cha magufuli..
Lakini Ni kweli kabisa Lowassa alileta matatizo makubwa ndani ya CDM na ngumu kuyaondoa..
 
IMG-20230308-WA0102.jpg
 
Back
Top Bottom