Hirizi ni mzigo mzito sana

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,640
697,940
Unajiuliza nini dhima ya hirizi maungoni? Unakuja kugundua mvaaji kapewa ili IMLINDE!
Imlinde na uchawi
Imlinde na wanga
Imlinde na chuma ulete
Imkinge na mambo yote mabaya
Impe mvuto
Impe ngekewa nknk

Unatafakari vile ilivyo.. Je ina uwezo wa kufanya yote haya? Ni kweli kabisa hirizi ni kubwa na ina nguvu kushinda roho yako?
Mbona sasa badala ya kukulinda wewe ndio unailinda?
Mbona sasa badala ya kukuficha usionekane na wabaya wewe ndio unaificha isionwe na wengine?

Mbona sasa inageuka mzigo mzito kwako kwa masharti?
Hakikisha haishiki maji(hata kama ina majasho yako)
Hakikisha huogi nayo
Hakikisha ukitaka kufanya mapenzi unaivua
Hakikisha huishiki mpaka ukoge
Hakikisha haigusani na msalaba nk nk

Mwisho wa siku badala ya yenyewe kukutumikia wewe ndio unaitumikia na kuijengea madhabahu bila kujua...!! Hata mapete ya bahati nayo ni aina mojawapo ya hirizi maana nayo yana masharti kama yote!
Kama unalo moja au kadha maungoni mwako tambua umebeba uchafu usio na maana yoyote na limekugeuza mtumwa bila ridhaa yako! LIVUE ULITUPILIE MBALI KULE
1270845_hirizi_2.jpg
 
Shukrani Mkuu kwa Elimu.

Kumbe watu huwa wanajilinda kupitia hayo madude nasikia pia + yale mapete makubwa...sasa ikitokea amelisahau kwa bahati mbaya then akakutana na wajamaa..

Ndio basi tena?..au?

Yote kwa yote watu tuache uvivu wa maombi.
 
Back
Top Bottom