Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,967
- 11,212
Tatizo lao wao ni kodi kwanza, reinforcement second na mazingira ya soko ndio kitu cha mwisho akilini mwao.Hawajaangalia pia backward na foward linkages ya kuleta magari mengi bongo
Kuna watu wataathirika sana kibiashara wanapolimit haya mambo mf, wauza mafuta, spares, garage
Na mbaya zaidi hakuna kiwanda hata kimoja bongo cha magari useme tutakimbilia huko
Ajali kwa kweli zimezidi especially za mabasi na malori na mengi ukiyaangalia yakiwa katika mazingira ya ajali sanasana malori unakuta wheel axles chali zimegeuka upande mwengine kabisa. Lakini hii aina maana wote wenye malori ya miaka hiyo yapo katika hali sawa.
Ndio maana ukaguzi wa ubora wa gari kuwa barabarani ni kitu muhimu sana kushinda sera ya kukazania magari mapya, kwanza kukaguliwa unalipa hela serikarini (ongezeko la pato, considering wingi wa magari hili linaweza wapa nafasi ya kushusha ushuru wa uagizaji magari makubwa na mazuri kama kila gari ndani ya tanzania litakaguliwa kwa helfu ishirini tu kwa mwaka au mengine kupata ukaguzi kila baada ya miezi sita kutoakana na umri ulioenda sana) na hivyo kuwa na annual income allocated to road infrastructure.
Iwapo gari likifeli linanyimwa kibali cha kutembea mpaka marekebisho kadhaa yafanyike the idea behind this ni kulinda umuhimu wa watu kumiliki magari kwa matumizi yao muhimu ya kikazi ama kifamilia na kumiliki kulingana na uwezo wao.
Halikadhalika itapanua service sector ya magari both repairing and parts replacement, in the long run wale wenye magari ambayo spare zake hata ulaya azipatikani au ni tabu kuzipata wenyewe watabadilisha tabia ya kuagiza magari hayo au kuendelea kuyatumia yakisha fail test kutokana na ugumua wa parts replacement na sheria za ukaguzi zinavyotaka ndio mwanzo wa kuwa na scrap yard zetu za magari maana parts zingine ambazo bado imara zinaweza kwenda kwenye magari mengine.
Kwakuwa serikari inakusanya mapato mapya ya ukaguzi, wafanya biashara wa repair wanalipa kodi, hawana sababu ya kuwekea vat kubwa kwenye import parts hila mfanya biashara wa parts alipe kodi za kibiashara therefore kukuza na kulea repair industry.
Wakiongeza na kushusha ushuru wa magari kama hayo ma X5 et al baada ya miaka michache yataingia kwawingi kitasawazisha kipato ambacho ni sawa na sasa kama si zaidi (ukiongezea na kodi zilizojitokeza za ushuru wa makampuni yaliyotokana na sera na charge za ukaguzi) faida zingine ni kuwa barabara zitajaza magari yenye ubora zaidi.
Vitu hivi vinahitaji majadiliano na wadau wa sehemu husika, wachumi na asasi za kiraia sisi waafrika bado kuelewa kama chanzo cha policy endelevu ni kushirikiana na wadau ili serikari isi loose kipato, sector ikuwe na kutoa ajira na jamii ipate inachotaka.
Mwisho wa siku kupunguza ajali licha ya hizo sheria ni road regulation, imagine umeendesha masaa kadhaa kwenye giza out of the blue jamaa anakuja na full light na wewe huko speed halafu labda umechoka that situation adds up to driving error, ni hivi regulations za barabarani pia ni tatizo.