Serikali kuwabana zaidi waagizaji Magari yaliyotumika ili kulinda uzalishaji wa ndani

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,798
12,240
Watanzania wajiandae kuanza kununua magari mapya baada ya serikali kukamilisha kuandaa sera mpya ambayo itapiga marufuku Watanzania kununua magari yaliyotumika.

Sera hii mpya inaungwa mkono na wawekezaji ambao watakuwa na jukumu la kuingiza magari mapya na pia kushirikiana na makampuni ya kigeni yanayounda magari kujenga viwanda hapa nchini.

Maoni yangu: Wale wote walinaojiandaa kununua magari yaliyotumika kwa bei nafuu wafanye haraka kabla sera mpya haijaanza kutumika.
---
Wakati Kiwanda cha Magari cha Mahindra cha India, kikikusudia kuwekeza zaidi Sh10 bilioni nchini, Serikali inakusudia kufanya mapitio ya sheria ya uagizaji magari nje kwa lengo la kubana zaidi uingizaji wa magari yenye muda mrefu ili kulinda wawekezaji wa ndani.

Ujio wa kampuni hiyo umekuja zikiwa zimepita siku 25 baada ya Rais Samia kufanya ziara nchini India Oktoba, mwaka huu na kuwashawishi wawekezaji waje kuwekeza nchini.

Mahindra wanakuja nchini kufanya uwekezaji wa uunganishaji wa magari madogo kwa kushirikiana na Kampuni ya Tanzania ya Gf Automobile inayofanyia shughuli hizo Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi ya ushirikiano huo, iliyofanyika jijini Da es Salaam leo, Jumanne Desemba 5, 2023, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema katika ziara ya Rais Samia nchini India, kampuni ya Mahindra iliahidi kuwa ya kwanza kuleta shughuli zao nchini.

Amesema kampuni hiyo imekuja kwa ajili ya hatua za awali na kwamba ndani ya miezi sita itaanza uzalishaji wa magari hayo nchini.

“Uwekezaji huu maana yake ni kazi kwa vijana wetu, kodi kwa Serikali na kuongeza uchumi kwa Watanzania na Taifa kwa ujumla,” amesema Profesa Kitila alipokuwa akifafanua nini maana ya uwekezaji huo katika uchumi wa nchi.

Amesema uwekezaji huo unaenda sambamba na malengo ya Serikali katika kuvutia wawekezaji katika sekta ya magari magari nchini, hasa yanayotumia umeme, kwa kuzingatia Tanzania ina madini ya Lithium yenye uwezo wa kutengeneza betri za umeme.

“Ili kukamilisha hili, Serikali itaangalia upya sera yake ya uagizaji magari kutoka nje, kwa sasa unaruhusiwa kuingiza gari lolote hata kama limeshatumika miaka 100 unaruhusiwa kuingiza,” amesema na kuongeza;

“Lakini ili kulinda viwanda vya kuzalisha magari hapa nchini, huko mbele lazima tuangalie sheria zetu upya ili kuzuia baadhi ya magari ambayo yamechakaa na hivyo kulinda soko la magari la hapa Tanzania na yale yatakayokwenda kwenda nchi nyingine.”

Hata hivyo, licha ya kuruhusu magari yenye umri wowote kuingia nchini, kiwango cha tozo ya uchakavu kinatofautiana kutokana na mwaka ambao gari ilitengenezwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Januari 2021 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), utozaji ushuru kwa magari yaliyotumika, hutokana na umri wa gari kwa kufuata mwaka wa kalenda.

Kwa upande wa magari madogo yenye umri wa miaka minane hadi tisa tangu kutengezwa, pamoja na kodi nyingine, hutozwa ushuru wa bidhaa kwa asilimia 15 huku yale yenye umri zaidi ya huo, hutozwa asilimia 30.

Ushuru mkubwa zaidi umewekwa kwa magari yaliyotengenezwa muda mrefu kama njia ya kuvunja moyo uagizaji wa magari yaliyotengenezwa muda mrefu.

Naye Mkurugenzi wa GF Group, Imran Karmali amesema uunganishwaji wa magari hayo madogo nchini utasaidia kushusha gharama za uagizaji na kuwawezesha Watanzania kumudu gharama.

“Pia magari haya yatakuwa mapya. Hivyo kama malengo ya Serikali ni kusaidia viwanda vya magari viongezeke, ni vyema kuweka mazingira magumu kwa magari yaliyo na miaka mingi kuingia nchini,” amesema Karmali.

Amesema waliona fursa ya kushirikiana na Mahindra baada ya Rais Samia kutembelea India ndipo waliamua kutafuta kampuni kutoka nchini humo ili waweze kushirikiana nao.

Kampuni ya GF imekuwa moja ya kampuni zinazounganisha magari makubwa nchini kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo za kubebea mizigo na kwa mwaka huu pekee hadi Oktoba wamezalisha zaidi ya magari 1000.

“Tunapokwenda kuanza uzalishaji wa magari madogo, tutaongeza pia idadi ya ajira zitakazozalishwa, kwa sasa watu 250 wameajiriwa huku 700 wakiwa ajira zisizokuwa rasmi,” amesema Karmali.

Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri amesema ujio wa kampuni hiyo unaakisi ongezeko la uwekezaji lililoshuhudiwa kati ya Julai hadi Septemba mwaka huu ambapo mtaji wa zaidi ya Sh2.505 trilioni umewekezwa sekta mbalimbali.

Amesema uwekezaji huo ni mara mbili ya kile kilichokuwapo kipindi kama hicho mwaka 2022, Pia ni nusu ya uwekezaji ambao Tanzania iliupata kwa mwaka 2019 na 2020.

Aliwataka Watanzania kushiriki katika mageuzi ya kiuchumi kwa kutumia vivutio mbalimbali vilivyowekwa na Serikali kwa ajili yao ili waweze kuwekeza kwa urahisi zaidi na kupata ushirikiano.

“Watanzania wenye shule, kiwanja, jengo wanaotafuta wabia wa kuwekeza nao, sisi TIC tunapokwenda nje ya nchi kuhamasisha uwekezaji hatutamani kuona wawekezaji wanakuja kusimama kwa asilimia 100 tungependa kuona kilichotokea kwa Gf Automobile na Mahindra kinatokea kwa Watanzania wengi,” amesema Teri.
 
Watanzania wajiandae kuanza kununua magari mapya baada ya serikali kukamilisha kuandaa sera mpya ambayo itapiga marufuku Watanzania kununua magari yaliyotumika...
Hii nchi bwana. Asilimia kubwa ya wafanyakazi wa serikali ni waalim ambao imeshindwa kuwalipa pesa ambayo inawawezesha kununua gari mpya.

Hata viinua mgongo vyao wengi wakipewa haviwezi nunua brand new car.

Halafu wanatunga sera ya kuzuia magari used.

Unajiuliza lengo ni kwamba watu wasimiliki magari au
 
Ningemuona Waziri ni kichwa kama angeanza kwanza na mchakato wa kuyashawishi makampuni makubwa ya kutengeneza magari kama Toyota, Isuzu, Suzuki, Mitsubishi, nk kuja kujenga viwanda vya kua assemble magari! Kabla ya kukurupuka kama ilivyo desturi yao.

Maana wanatambua fika Watanzania walio wengi hawana uwezo wa kununua magari mapya kutokana na vipato vyao vidogo. Ila kwa makusudi tu wanajitoa ufahamu.

Viwanda vya nguo tu vinawashinda!! Mpaka leo bado tunavaa mitumba na nguo kutoka China!! Halafu wanapata kabisa ujasiri wa kutaka kupiga marufuku used cars from Japan, etc!!!

Halafu nilitaka kusahau!! Hivi yale mabehewa na vichwa vya treni ya mwendokasi ni vipyw, au used!!!!
 
Watanzania wajiandae kuanza kununua magari mapya baada ya serikali kukamilisha kuandaa sera mpya ambayo itapiga marufuku Watanzania kununua magari yaliyotumika...
Wenzenu South africa walijenga kwanza Viwanda vya kutosha, vya karibia aina zote za Magari maarufu, ndo baadaye wakapiga marufuku magari ya Mtumba!

Sasa Viongozi wetu wanadanganywa na Wafanyabiashara huku kukiwa hakuna kiwanda hata kimoja....!

Hii ni akili ama Matope.
 
Hii ni akili ama Matope.hi

Back
Top Bottom