Hii sio usawa

Likasu

JF-Expert Member
Jan 18, 2011
843
405
Sheria ya ndoa 1971 ibara ya 129(1) " ni jukumu la mwanaume kutunza watoto wake" sasa ktk ulimwengu wa usawa bila kuangalia vipato vya wanandoa kwani pia mwanamke anaweza akawa na kipato zaidi ya mwanaume au mwanamke akawa ndo mwenye kipato mwanaume akawa hana kipato lakini jukumu la kutunza mtoto ni la mwanaume tu. Yaani mwanamke akimtunza mtoto ni kama anasaidia tu sio jukumu laje. Jee hii ni usawa wa kijinsia ?
 
Kaka ndiyo maana huwa tunasema watoto wangu. Japo kuwa akina mama huwa wanakuja juu lakini kwa sheria hii, ina maana mtoto ni wa baba. Ningewashauli wakiwa wanadai haki pia wadai na kubadilishwa kwa sheria hii iliyopitwa na wakati. Wizara ya wanawake, jinsia na watoto mpo wapi???
 
Hawawezi kudai sheria ibadilishwe kwa sababu inawaondolea jukumu la kutunza watoto. Wao wanakomaa na mirathi tu.
 
Ndio hapo unatakiwa uwaheshimu wanawake. They are potentially very powerful.

Wanaonekana wapole, wanyonge, wanahitaji kuhurumiwa.
Lakini:

Watoto, ni jukumu la mwanaume kuwatunza
Halafu watoto wenyewe wanaweza wasiwe na DNA yako.
 
Back
Top Bottom