hii picha inatufundisha nini

Tulen tu raha huku mjini ila tusimsahau mama kule kijijn kwan hatujui alipitia mishe mishe gani mpaka leo tunajidai na kula mabaga huku mjini,
Eee mungu mpe mama yangu maisha marefu aendelee kuenjoy kile kidogo ulichonijali mwanae,
Nampenda sana mama yangu.
 
unatufundisha kuwa usingizi ni popote hata chini ya kibanda za nyanya unaweza kumlaza mtoto akapata usingizi pia
 
Mama mtoto mjasirimali na touch screen phone isiyobanduka kujivisha shingoni, dunia inabadilika na wanadunia wako radhi kuendena na wakati.
 
Raisi wa kesho TZ, hii picha inafaa ihifadhiwe kwani kuna uwezekano huyo mtoto akaja akawa Maarufu sana!!!!!
 
nakubaliana na wote mliochangia

Hofu yangu..kama patatokea cha kutokea mf..Vurugu za mgambo?..au vurugu za watu kupigana
pili kama inatokea mvua kubwa ya ghafla...je ...Bi mkubwa atamkumbuka mtoto hapo chini au Biashara kwanza?
 
haya ndiyo maisha ya watanzania walio wengi, wanajitahidi kadri ya uwezo wao, ili kukabiliana na maisha haya magumu, wanapodai watanzania ni wavivu, wakati hakuna uwekezaji nchini, nashindwa kuelewa, huyu mama hana aridhi, ameona njia pekee ya yeye kuweza kuendesha maisha yake ni kufanya uchuuzi, ili apate fedha za kujikimu yeye na familia yake, viongozi wetu ni kweli wanalitambua hili kuwa wananchi wanajitahidi kadri ya uwezo wao?
 
Inatufundisha kwamba haki sawa kwa wote mama baba wote wanatakiwa kuchakarika kutafuta ngawila si kwasababu anamtoto mdogo ndiyo akae nyumbani lahasha!
 
Imenifundisha hiyo nchi alokuwa mwenye hii picha ni masikini na ajira hakuna na bila juhudi binafsi mkono hautaenda kinywani
 
Kweli hakuna kama mama. Namtakia mama yangu afya na maisha marefu ya furaha katika siku hii ya wapendanao. NAKUPENDA MAMA
 
Inatufundisha tuwe tunawalaza watoto wetu chini ya meza za biashara wanaposikia usingizi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom