Hii ni nini, kumuwaza mtu na baadaye akakutafuta?

MENEMENE TEKERI NA PERESI

JF-Expert Member
Mar 11, 2022
2,539
6,295
Ndugu zanguni hamjambo?

Eti mnisaidie mimi ndugu yenu nikimuwaza mtu au kumfikilia kwa siku nzima basi lazima atapiga simu kwangu au kama hana namba yangu ni lazima ataitafuta kunijulia hali.

Yaani leo nikiwa niko katika harakati zangu nikamuwaza yeyote lazima kuna muda hii hali itajirudia tena akilini basi lazima nikae karibu na simu yangu maana lazima mlengwa atanitafuta.

Je, hii ni nini?
Nawakaribisha wajuzi mbalimbali wa mambo kutoka kada ya uchawi, unajimu na fikira mnyambuliko wa dunia ya kiza.

Ahsanteni.
 
Niliwahi kusikia mahali ni kama Miayo ukipiga na anaekuangalia nae atapiga Miayo ((sidhani kama nimeandika sahihi))... na kumbukumbu ipo hivyo hivyo ukiwa unamkumbuka kumbuka Mtu basi na yeye anakukumbuka.... ila wewe unakaza kumtafuta yeye kujizuia hawezi anajikuta anakutafuta
 
Ndugu zanguni hamjambo ?

Eti mnisaidie mimi ndugu yenu nikimuwaza mtu au kumfikilia kwa siku nzima basi lazima atapiga simu kwangu au kama hana namba yangu ni lazima ataitafuta kunijulia hali .

Yaani leo nikiwa niko katika harakati zangu nikamuwaza yeyote lazima kuna muda hii hali itajirudia tena akilini basi lazima nikae karibu na simu yangu maana lazima mlengwa atanitafuta .

Je hii ni nini ?
Nawakaribisha wajuzi mbalimbali wa mambo kutoka kada ya uchawi , unajimu na fikira mnyambuliko wa dunia ya kiza .

Ahsanteni .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
CC Mshana Jr
 
Niliwahi kusikia mahali ni kama Miayo ukipiga na anaekuangalia nae atapiga Miayo ((sidhani kama nimeandika sahihi))... na kumbukumbu ipo hivyo hivyo ukiwa unamkumbuka kumbuka Mtu basi na yeye anakukumbuka.... ila wewe unakaza kumtafuta yeye kujizuia hawezi anajikuta anakutafuta
Basi itakuwa hivyo , maana nikiwawaza hata siwapigii ila lazima watapiga tu .

Ni leo nimemkumbuka ex wangu , hasa ile style yake aliyonipa ya kafie mbali basi nimekaa kidogo mara simu inaita kusikia sauti ni yeye basi full shangwe .

Lawama zake za hapa na pale ila nikamueleza walau wikiendi tumeet anipe tena ile style

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo inaitwa TELEPATH Ni ule uwezo wa kusoma au kuwasiliana moja kwa moja na mawazo ya mtu mwingine bila kutumia njia za kawaida za mawasiliano kama lugha au ishara.

Japo sayansi bado haijathibitisha ila aina hii ya mawasiliano ipo na mtu akiwa ana meditate kwa bidii huu uwezo anaupata . DR Mambo Jambo
Dah basi unadhani nameditate basi ? Nipo zangu tu na ingia toka bar za wanakijiji hata msikiti na kanisa sijui viliko .

Ila kama ni uwezo mzuri nijuzwe naweza labda kuwa hata sangoma nipate hela za wanakijiji .

Chief DR Mambo Jambo nakuomba bana kuna namna umetajwa unaweza nieleza chochote aisee

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
• Kiongozi MENEMENE TEKERI NA PERESI, siyo michepuko kweli hiyo, ndo inatikisa ubongo wako. .

• Wanasemaje hapo Green City mkuu..
Yaani kiukweli wengi ni michepuko .
Hapa Green city pako safi kabisa na mvua ya hapa na pale .

Ila zaidi tuko tunajiandaa na maandamano ya Chadema japo kwetu sisi wanakijiji hayana mashiko mno maana kwasasa sukari imefika 2300 hapa kijijini ila umeme hatuna shida nao maana walituunganishia mawaya hawajawi kuuwasha hivyo hatuujui .

Kuhusu maisha kuwa magumu , huku jembe lako ndiyo litaamua familia yako iishi kwa neema mwaka mzima au yakukute magumu .

Hivyo napata kazi sana kuwaambia wanakijiji twende mjini kuandamana maana walipita wawakilishi wa Tulia Ackson wakawapa wanakijiji mkopo wa elfu sabini mpaka laki hivyo huwaaambii kitu .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Dah basi unadhani nameditate basi ? Nipo zangu tu na ingia toka bar za wanakijiji hata msikiti na kanisa sijui viliko .

Ila kama ni uwezo mzuri nijuzwe naweza labda kuwa hata sangoma nipate hela za wanakijiji .

Chief DR Mambo Jambo nakuomba bana kuna namna umetajwa unaweza nieleza chochote aisee

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Dr atakueleza ila huwa inatokea tu na inafaida, unaweza mshawishi mtu ata kabla ya kuzungumza nae na kujua hadi mwisho wake utakuaje ni jambo ambalo lipo. Manabii matapeli wajanja wanaitumia sna hii kuwasoma kondooo.
 
Kuna namna naanza kukuelewa ndugu .
Kuna hali nakuwa nayo ikiwa ninahitaji kufanya mazungumzo seriuos na mtu serious uwa ni kama nabahatika kuhisi kabla kuwa ataongea hiki au kile .

Mfano , nikiwa na watu wengi maahali pamoja najikuta nakuwa wa kwanza kuhisi ujio wa mtu tulipo au kuhisi kugongwa kwa mlango hivyo nikisema kuna mtu anakuja au anagonga mlango wengu husema hapana umesikia vibaya ila ghafla kweli mtu hubisha tena

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Psychology Fact: when you can't get a person out of your head it means that the other person is also thinking about you.
Dada Hannah nimeingia google nimeelewa ulichosema nashukuru sana ila naomba uzi wangu uende kwa kiswahili maana kuna waswahili wenzangu wasije wakaupita kisa hii lugha maana wameshanifuata PM kunishukuru kwa mimi leo kupandisha uzi .

Kwako Dr Faustine Ndugulile

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom