Hii ni kwa wana-CHADEMA tu

Acha kudanganya watu, wewe mwenyewe unapata support kutoka CDM , vipi ww ukisupport tena?
 
Naunga mkono hoja, umesahau kitu kimoja. Kususa kama kawa, mpaka kieleweke!
 
Hivi kwanini tusifungue tawi hapa kwenye jf?

Aisee naunga mkono hoja; sio tu tawi lkn tuwe na utaratibu wa kuchangia pia! Nina imani kwa id hizi wengi watachangia bila kucompromise ajira zao hasa walio kwenye sector nyeti za kiserikali!
 
ndugu zangu wana cdm( nasisitiza ni chadema tu) matokeo ya igunga yamenifanya nije na wazo.Huu si wakati wa sie kutulia na kuacha hili jambo linapita bila kulifanyia kazi.Kifupi ushauri wangu harakati za chama ziendelee chini ya viongozi hapo wilayani kwa kuimarish chama kama walivyoshauri watu wengi mikutano mijini na vijijini watu wapewe elimu ya uraia .kukubalika kwa cdm kumenistua sana na hili jambo lisiachwe hivi hivi.mwalimu aendelee na mikutano ya kushukuru wananchi na kuendelea kuwapa taarifa wale 22000 na zaidi ambao hawaitaki ccm.wana cdm tuwe tayari kusapport juhudi kama hizi. Maeneo mengine wameweza kwa kutumia michango toka kwa wanachama na changizo mbalimbali. Hili linawezekana wana cdm tujitoe hata kwa mali ili ukombozi upatikane naomba kuwasilisha

Mama kubwa hiyo inaweza kuwa moja ya mikakati mnayoweza kuitumia kuongeza uungwaji mkono wa chama chenu na inaweza kuwasaidia KIDOGO kwenye uchaguzi ujao. Inabidi muelekeze nguvu zenu kwenye kudai katiba mpya itakayoandaa mazingira yanayotoa fursa sawa kwa vyama vyote. Kwa sasa hamuwezi kuishinda CCM ambayo inatumia dola kubaki madarakani.

CCM wana tume ya uchaguzi, wana wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wakurugenzi wa halmashauri za miji na wako chini ya ofisi ya waziri mkuu, wana polisi, wana usalama wa taifa, na wana uhakika wa kuwatumia mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ambao wote ni makada wa CCM lakini wanagharimiwa na serikali kuwakampenia CCM. kumkukeni kuwa wakuu wa mikoa na wilaya, ambao ni makada wa CCM, ndio wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama wa maeneo yao. Kwa kutumia kofia hiyo wanaweza kabisa kutoa maelekezo kwa maofisa wa polisi, usalama wa taifa na jeshi kuhusu kuwasaidia kweye uchaguzi.

Mfumo wa sasa wa kikatiba na kisheria uliandaliwa na Hayati Nyerere kuhakikisha kuwa CCM Inatawala milele. Msipofanikiwa kuubadilisha mfumo huo ili kuwapa fursa sawa na CCM, kamwe hamuwezi kushinda uchaguzi nchi hii. Mtapata majimbo machache ambayo wananchi wake wameamka kisiasa na wanauwezo wa kudai na kusimamia haki zao. Huku kwingine mtaishia kuyasikia kwenye redio tu.
 
Kweli kabisa nakuunga mkono isitoshe na mimi magamba wameniuzi sana kwa vituko na mbinu walizofanya ingunga..ila zitawaishia tu siku mbinu zao zoteeee
 
  • mipango yote ni bora iambatane na vitendo itasaidia sana pia huu uzi ukae agalau week moja first pg wengine wauone nadhani wataunga mkono hoja
  • tatizo ni nani atakaye kuwa msimamizi mwadilifu, anaye aminika NA kukuballika na CHADEMA JAMII FORUMS

Mkuu mimi napendekeza Dr. Slaa ndo asimamie huu mfuko wa kuelimisha vijijini na kujenga network ya chama. Tunamwamini na anaaminika pia.
 
.... (1) katiba MPYA, (2) Operation Vijijini, Mashina mapya na Elimu ya Uraia kwa wapiga kura watarajiwa, (3) kuundwa upya Tume ya Uchguzi; sheria na kanuni zake,

(4) kuelekeza Tume kutumia Mtandao wa Kitaifa wa Kompyuta ulio wazi kwa washiriki wote kuendeshea hatua zote z uchaguzi, (uhakiki wa daftari la wapiga kura kila baada ya miezi 24 na pale kila kunapotokea uchaguzi mdogo.

tuanzie hapa na kuendeleza moto mkubwa zaidi kupiga vita UFISADI na ugumu wa maisha kwa wananchi kwa ujumla wetu.

Mpaka hapa naomba kila nayesoma taarifa hii hapa ukajiambie mwenyewe kwamba 'VITA VYA UKOMBOZI WA NCHI TOKA KWA WAKOLONI WEUSI UNAANZA NA KUFUNGA NA MIMI NIKIWA NI MPAMBANAJI WA AHUENI YA BAADAYE'.

Haya twende sasa Machalii wote nchini!!!!!!!!!!!!!!
 
naunga mkono hoja mana kama igunga tumeshinda mjini kazi ianze vijijini huko ndo magamba wanakoringia simply because wananchi huko hawana ufahamu wanachojua wao ni chama cha nyerere, na ndo kuna maisha mabovu zaidi, slaa, mbowe, zitto tafadhalini zingatieni hili
 
naunga mikono na miguu!! tena ingetakiwa CDM waanzishe ka mfuko fulani wa kuimarisha chama!! ili watu wenye mapenzi mema na cdm wakiwezeshe ili kiweze kuwafikia watu wa kijijini ili wapate elimu ya uraia.au unaonaje.
hayo yanawezekana kama harusi tunaweza kuchangia je chama chetu tutashindwa kuchangia? pia tisheti, skafu hata begi zinaweza kutengenezwa tukanunua vitu hivyo kwa mnada ili kuimairisha chama kifedha .nina mawazo mengi lakini sina ukaribu na viongozi wa cdm hivyo wenye kuongea nao tafadhali wapeni mawazo. Hii nchi itakombolewa na wenye uchungu.
 
Naunga mikono na miguu yote, kwanza hoja yako nimeipa kipaumbele kuliko zote zilizotangulia, pili nimekugongea like, na tatu mimi naanza kwa mfano kwa kuwaelimisha watakao elewa na wale wasio waelewa nitaweka utaratibu wa kununua shahada zao siku chache kabla ya uchaguzi wowote na kuzichoma moto, namshauri Dr aungurumishe chopa tena igunga awaite wananchi wote kwenye mkutano mkubwa zaidi ya ambayo imeshawahi kufanyika ili kuwashukuru wanaigunga na pia kuwatia moyo pamoja na mgombea wao ili wajue kuwa cdm haikuwa kwao kwa ajili ya madaraka au ubunge bali kwa mapenzi ya cdm kwao...kama bajeti ya chopa hamna wana cdm tuko wengi huku jf tunaweza kujichanga na kufanikisha hilo ni mtazamo wangu tuu....nawasilisha
Asante leo nimegongelewa like nyingi nashukuru kama na yako ipo.Maeneo ya kuyapa kipaumbele ni yale matokeo ya 2010 yalionyesha tulifanya vizuri tukashindwa kwa kura chache au kwa kuchakachuliwa, huko tupeleke nguvu hadi vijijini.Maeneo korofi yashughulikiwe kwa namna yake yote yanawezekana watu wamechoka na wako tayari kwa mabadiliko
 
Nakubaliana nawe, nawaomba viongozi wa CDM wasichelewe kuchukua hutua,vuguvugu hili lisiachwe kupoa,kama alivyosema Dr. Slaa,UMOJA WETU NDIYO NGUVU YETU. Chadema itakwenda ikulu kwa nguvu ya umoja wa wapenda mabadiliko,haitaji michango ya mafisadi, Mh Silinde alishinda Ubunge kwa michango ya watanzania maskini.PAMOJA TWAWEZA(sio ya RAJESH).
Imani ya watanzania kwa CHADEMA ni kubwa sana.
Time for action makamanda.tuko pamoja
Viva Chadema
Tanzania ni yetu sote


Hivi hatuwezi kumwajiri Mwalimu Kashindye kufanya hii kazi kwa mkoa mzima wa Tabora? Nadhani si ngumu kumlipa japo allowance sawa na ule mshahara na malupulupu aliyokuwa anapata wakati akiwa afisa elimu.

Tujiulizeni jamani mchango wetu ni upi katika ukombozi wa nchi hii? Wenzetu wanatumia matajiri kufadhiri chama lakini cdm haina matajiri hivyo ni sisi walalahoi tutawafadhiri cdm mpaka kieleweke.

Tunaomba viongozi wa cdm watupatie ile namba ya kutuma neno 'CHADEMA' kwenda kwenye short code ya wasp ili tuchangie kwa airtime. Ni pesa ndogo sana lakini kama kila mtu atafanya hivyo mara kwa mara anapo recharge simu yake itasaidia sana kupata kiasi fulani kikatumika kwa ajili ya Elimu ya uraia vijijini.
 
ndugu zangu wana cdm( nasisitiza ni chadema tu) matokeo ya igunga yamenifanya nije na wazo.Huu si wakati wa sie kutulia na kuacha hili jambo linapita bila kulifanyia kazi.Kifupi ushauri wangu harakati za chama ziendelee chini ya viongozi hapo wilayani kwa kuimarish chama kama walivyoshauri watu wengi mikutano mijini na vijijini watu wapewe elimu ya uraia .kukubalika kwa cdm kumenistua sana na hili jambo lisiachwe hivi hivi.mwalimu aendelee na mikutano ya kushukuru wananchi na kuendelea kuwapa taarifa wale 22000 na zaidi ambao hawaitaki ccm.wana cdm tuwe tayari kusapport juhudi kama hizi. Maeneo mengine wameweza kwa kutumia michango toka kwa wanachama na changizo mbalimbali. Hili linawezekana wana cdm tujitoe hata kwa mali ili ukombozi upatikane naomba kuwasilisha
Hayo mawazo ni mazuri sana, wala hakuna haja ya kuwa na wasiwasi bora kuna watu wameipenda CDM fedha si tatizo Obama wa USA alichukua nchi kwa one dollar campaign. Tunaweza kuanza kuchanga kuanzia sasa tukilenga 2015 bora good accountability and transparency!!!!!!!!!!!
 
  • mipango yote ni bora iambatane na vitendo itasaidia sana pia huu uzi ukae agalau week moja first pg wengine wauone nadhani wataunga mkono hoja
  • tatizo ni nani atakaye kuwa msimamizi mwadilifu, anaye aminika NA kukuballika na CHADEMA JAMII FORUMS
CHADEMA wenyewe makao makuu wa introduce mtu atakaye coordinate hii mipango ya one dollar campaign kukomboa Tanzania yetu!!!!!!!!!!
 
Kwa kweli watu wa vijijini wanahitaji sana kupewa elimu ya uraia na haki ya kushiriki katika chaguzi mbalimbali!
 
Naunga mkono hoja. Tuanze sasa na sio baadae. Inabidi tuende mbali kidogo. Inatakiwa katika uchaguzi wa 2015, kila jimbo la uchaguzi, kata kwa maana ya diwani, jimbo kwa maana ya Mbunge wa jimbo na Raisi anyekubalika. Maadalizi inabidi yaanze sasa, kwa kuwa na ofisi za vijiji na mtaa. Ni kwa msingi huu tunaweza kuwa na wagombea katika ngazi zote. Wagombea wa chama ndio wanaoteua mawakala wa kusimamia kura zao nao watalinda kura za mbuge na rais.
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom