Hii ni habari njema, sasa tunaongea kuhusu elimu nchini

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Next....

(1) Futa kidato cha Tano na Sita. Vyuo Vikuu vyote viwe na mwaka mmoja wa kufundisha Foundation courses mbili (i) Foundation course for Natural Sciences na (ii) Foundation course for Social sciences.
.
Tupunguze kabisa muda wa kukaa shuleni kabla haja fuzu fani fulani. Imagine Sasa hivi ukianza chekechea utatumia miaka 17 (yaani 1+7+4+2) ndiyo uingie Chuo Kikuu really? Angalao tupunguze iwe 11 (yaani 1+6+4) tu.

(2) Futa Advance Diploma. Huyu aongezewe masomo kidogo kisha apewe degree tu..

(3) Ngazi ya cheti (certificate) ibaki kwa wanaotafuta ujuzi maalum wa nyongeza au ambao hawakufaulu vizuri Form IV waitumie kama njia ya kuelekea kwenye Diploma. Mfano mimi nina shahada ya Afya ya wanyama, halafu nataka kupata ujuzi kuhusu uvuvi. Naweza kwenda kutafuta cheti cha uvuvi.
.
Au sikufaulu vizuri Form IV natafuta ujuzi ili kuelekea kupata diploma au kujiajiri. Vyuo vya VETA sasa vitoe National High Certificates na Diploma. Udereva, ufundi, etc. Cha msingi njia (pathways) za kila mtu kufuzu baada ya kidato cha nne ziwe nyingi.

(4) Imarisha vyuo vya elimu ya kati. Wakimaliza Form IV, wote wapate pa kwenda kupata ujuzi rasmi. Wengine waaende chuo kikuu, na wengine waende kwenye vyuo vya Diploma... za kilimo, nyuki, mifugo, uvuvi, afya, ualimu, maabara, utalii, IT, ufundi, n.k!. Wengine wapite njia ndefu ya Cheti.. Alimradi hakuna anaekosa option.

(5) Ongeza bajeti ya Elimu
(a) Hakikisha shule za sekondari zipo za kutosha.. Idadi ikaribie ile ya shule za msingi, kwasababu idadi inayomaliza darasa la sita sasa ndiyo hiyo hiyo itakwenda sekondari.. Au zilizopo ziwe na uwezo wa kuchukua wanafunzi wengi.. Streams... Mradi madarasa yasijae kupita kiasi

(b) Shule ziwe na vifaa na walimu wa kutosha. Tujenge uwezo wa walimu na mishahara yao isiwe na kwikwi.. Vifaa vya kufundishia viwepo vya kutosha.

(6) Tengeneza mitaala inayozingatia mahitaji ya uchumi wa nchi yetu na kukua kwa teknolojia duniani..

(7) Tukae chini tuje na mipango kabambe na endelevu ya kutoa mikopo ya elimu kwa ngazi zote. Kila mtu aweze kulipa ada!

(8) Nursery school iwe mwaka mmoja. Mtoto akiingia darasa la kwanza awe tayari anajua kusoma na kuandika. Tumepunguza muda wa kukaa shule ya msingi.. hivyo tusitumie mwaka mzima kufundisha aeiou.

Watoto chini ya miaka mitano wacheze tu na kujifunza kusocialize na basic life skills!

Mwaka wa tano waanze kuhesabu na kusoma. Akifika miaka 6 mbio za zianze 'tairi liwe kwenye lami!' siyo tena ba be bi bo bu.

Na Nursery iwe sehemu ya shule ya msingi. mtoto aunganishe tu.

Mambo ya Day Care ni idara tofauti kabisa.. Tena wanaofanya kazi huko wala wasiwe wamesomea ualimu. Wawe wataalamu wa mambo ya "BABY SKILLS AND EARLY CHILDHOOD DEVELOPMENT" Hii ni kozi maalum... watu waisome wapewe vyeti ndiyo waajiriwe kwenye Day Cares... Tena wapimwe akili na emotional intelligence kabisa Siyo kila mtu apewe kundi la watoto wa umri huu alee..
 
Mipango sio matumizi

Hizo shule za dumu fagio Ni uchafu mtupu wastage of time and resources

Elimu inahitaji Formation za kupunguza number of enrollment kwanza Kuna watu shule sio Sehemu yao Kabisa ..

Mfano for the time being wtoto wengi wanawaza ngono tupu kichwani so ao wanabidi wakacheze x than send them to school .

Elimu inabidi ibaki na watu wachache cream na sio kila Mtu .
 
Back
Top Bottom