Prof. Mkenda anafuata nyayo za Mungai ktk kuchezea elimu

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Nimefuatilia maelezo ya waziri na maafisa wengine wa wizara kuhusu mabadiliko ya mitaala ya elimu sijaona jipya zaidi ya ubabaishaji tu na kupiga posho kupitia semina uchwara.

Hakuna changamoto yoyote inayowakabili wahitimu wetu itakayotatuliwa na mitaala mipya.

Hoja kubwa inayosemwa kuwa ni sababu ya wizara kuja na mabadiliko ya mitaala ni wahitimu kukosa ujuzi na kushindwa kujiajiri baada ya kuhitimu.

Kuna mabadiliko gani makubwa ktk mitaala hii mipya? Kwenye kila badiliko nimeweka swali fikirishi.

1. Kuondoa mitihani ya darasa la saba. (Kwani mitihani ya darasa la 7 ndiyo inawakosesha wanafunzi ujuzi na maarifa ya kujiajiri?)
2. Kupunguza miaka ya elimu ya msingi kutoka 7 hadi 6. ( Miaka ya shule ya msingi ikiwa michache ndiyo wanafunzi wataweza kujiajiri?)
3. Kuunganisha elimu ya msingi na sekondari. Kwamba mtoto ataanza darasa la kwanza mpk kidato cha 4. (Nini lengo la kuunganisha? Kwani wasioweza kujiajiri ni wale wa shule za msingi tu? Mbona kuanzia form 4 mpk wahitimu wa vyuo vikuu wanahangaika mitaani?)
4. Mafunzo ya veta yatatolewa sekondari. (Vifaa vya kutolea mafunzo ya veta kila sekondari zote serikali itaweza kuvinunua? Ikiwa veta halisi ipo moja tu kila wilaya lkn bado vifaa vya kufundishia havitoshi vipi kila sekondari?? Huko sekondari hata madawati ni shida kompyuta, vyerehani na randa itakuwaje?)
5. Kupunguza baadhi ya masomo na kuyafanya kuwa ya kuchagua (optional/elective subjects). (Haina uhusiano wowote na kumpa ujuzi mwanafunzi).
6. Historia kuwa ya kiswahili na inayowajadili viongozi wetu, mfano Nyerere, Bibi Titi, Ndugai , Magufuli, n.k. (Hakuna cha maana ktk hili. Kujua maisha ya Bibi Titi kutamsaidia nn mtoto?)

Tatizo la wahitimu kutokujiajiri linasababishwa na nn hasa?

Kinacholeta shida siyo elimu peke yake. Mfano kuna wahitimu wa SUA wanaosomea kilimo wanazalishwa kila mwaka lakini hatuwaoni huku uraiani wakishiriki ktk kilimo. Kwann?

Wahitimu hawa wamepewa mafunzo ya kilimo na ufugaji kwa vitendo na ardhi imejaa tele hapa nchini. Sasa kwann hawaitumii elimu yao kujiajiri kwenye kilimo?

Halafu tujiulize hivi ni chuo gani kinachotoa mafunzo ya bodaboda, machinga na mama lishe?

Tatizo kubwa la nchi hii ni sera na mipango ya kiuchumi isiyo tabirika. Hiki ndiyo kikwazo cha wahitimu kushindwa kujiajiri. Serikali yetu haina focus. Haijawekeza ktk jambo lolote linalochagiza ama kuchochea uchumi. Mfano Marekani waliamua kuitambua sekta ya sanaa kama chanzo kikubwa cha mapato. Nchi ikatengeza sera na sheria nzuri za kukuza vipaji, kukuza muziki na kulinda haki za wasanii. Wakaanzisha vyuo vya fufundisha muziki na makampuni mengi yamewekeza kwenye Muziki. Muziki ukipigwa hata kwenye baa msanii analipwa.

Hapa kwetu Sasa. Kila kukicha mtazamo wa nchi unabadilika, mara utasikia "kilimo kwanza" baada ya muda "Tanzania ya viwanda" hujakaa sawa "Royal tour". Full madrama.

Huu mtaala mpya hautafanya chochote. Prof. Mkenda anafuata nyayo za waziri mwenzake aliyetangulia ambaye naye alikuja na vurugu kama hizi lkn hakufanikiwa.
 
Mpaka Sasa ilitakiwa wawewameshaanza kusambaza vifaa na kujenga miundombinu kwenye shule hizo nchi Zima Ili kuendana na mabadiriko ya mtaala.
 
Shida kubwa la taifa letu ni kufanya vitu kwa mihemko bila kufanya Research ilikupata kiini Cha tatizo Kiko wapi.Mfano ni kuanzishwa kwa Historia ya Tanzania lilikuwa wazo la mtu mmoja na sio maamuzi ya umma,lakini limefanywa kuwa suala la umma( maamuzi ya kisiasa zaidi).

Mwisho kama taifa Tunashindwa kufaham nini tunataka,ndio maana taifa lipo lipo tu.Hakuna muunganiko wa kisera toka awamu ya kwanza mpaka sasa ya Sita,Kichwa cha Rais na mawazo yake binafsi hubadili mwelekeo wa taifa.

Prof.Mkenda ni hopeless kabisa.
 
Nimefuatilia maelezo ya waziri na maafisa wengine wa wizara kuhusu mabadiliko ya mitaala ya elimu sijaona jipya zaidi ya ubabaishaji tu na kupiga posho kupitia semina uchwara.

Hakuna changamoto yoyote inayowakabili wahitimu wetu itakayotatuliwa na mitaala mipya.

Hoja kubwa inayosemwa kuwa ni sababu ya wizara kuja na mabadiliko ya mitaala ni wahitimu kukosa ujuzi na kushindwa kujiajiri baada ya kuhitimu.

Kuna mabadiliko gani makubwa ktk mitaala hii mipya? Kwenye kila badiliko nimeweka swali fikirishi.

1. Kuondoa mitihani ya darasa la saba. (Kwani mitihani ya darasa la 7 ndiyo inawakosesha wanafunzi ujuzi na maarifa ya kujiajiri?)
2. Kupunguza miaka ya elimu ya msingi kutoka 7 hadi 6. ( Miaka ya shule ya msingi ikiwa michache ndiyo wanafunzi wataweza kujiajiri?)
3. Kuunganisha elimu ya msingi na sekondari. Kwamba mtoto ataanza darasa la kwanza mpk kidato cha 4. (Nini lengo la kuunganisha? Kwani wasioweza kujiajiri ni wale wa shule za msingi tu? Mbona kuanzia form 4 mpk wahitimu wa vyuo vikuu wanahangaika mitaani?)
4. Mafunzo ya veta yatatolewa sekondari. (Vifaa vya kutolea mafunzo ya veta kila sekondari zote serikali itaweza kuvinunua? Ikiwa veta halisi ipo moja tu kila wilaya lkn bado vifaa vya kufundishia havitoshi vipi kila sekondari?? Huko sekondari hata madawati ni shida kompyuta, vyerehani na randa itakuwaje?)
5. Kupunguza baadhi ya masomo na kuyafanya kuwa ya kuchagua (optional/elective subjects). (Haina uhusiano wowote na kumpa ujuzi mwanafunzi).
6. Historia kuwa ya kiswahili na inayowajadili viongozi wetu, mfano Nyerere, Bibi Titi, Ndugai , Magufuli, n.k. (Hakuna cha maana ktk hili. Kujua maisha ya Bibi Titi kutamsaidia nn mtoto?)

Tatizo la wahitimu kutokujiajiri linasababishwa na nn hasa?

Kinacholeta shida siyo elimu peke yake. Mfano kuna wahitimu wa SUA wanaosomea kilimo wanazalishwa kila mwaka lakini hatuwaoni huku uraiani wakishiriki ktk kilimo. Kwann?

Wahitimu hawa wamepewa mafunzo ya kilimo na ufugaji kwa vitendo na ardhi imejaa tele hapa nchini. Sasa kwann hawaitumii elimu yao kujiajiri kwenye kilimo?

Halafu tujiulize hivi ni chuo gani kinachotoa mafunzo ya bodaboda, machinga na mama lishe?

Tatizo kubwa la nchi hii ni sera na mipango ya kiuchumi isiyo tabirika. Hiki ndiyo kikwazo cha wahitimu kushindwa kujiajiri. Serikali yetu haina focus. Haijawekeza ktk jambo lolote linalochagiza ama kuchochea uchumi. Mfano Marekani waliamua kuitambua sekta ya sanaa kama chanzo kikubwa cha mapato. Nchi ikatengeza sera na sheria nzuri za kukuza vipaji, kukuza muziki na kulinda haki za wasanii. Wakaanzisha vyuo vya fufundisha muziki na makampuni mengi yamewekeza kwenye Muziki. Muziki ukipigwa hata kwenye baa msanii analipwa.

Hapa kwetu Sasa. Kila kukicha mtazamo wa nchi unabadilika, mara utasikia "kilimo kwanza" baada ya muda ",Tanzania ya viwanda" hujakaa sawa "Royal tour". Full madrama.

Huu mtaala mpya hautafanya chochote. Prof. Mkenda anafuata nyayo za waziri mwenzake aliyetangulia ambaye naye alikuja na vurugu kama hizi lkn hakufanikiwa.
Katafute nchi ya kuishi we kenge. Nachukia vilalamishi km ww
 
Tatizo la nchi hii ni kukosa watu wanaoweza,kufikiri,kuamua na kutenda kwa ueledi unaoendana na mazingira husika.kukosekana kwa watu hao kumesababisha kila kitu kuwa drama na vituko.Elimu inayohitajika sasa ni ile itakayomfanya alieipata kuweza kutumia akili yake vizuri katika kuyatazama mazingira na kuamua kufanya kitendo chenye manufaa kwa faida yake na jamii husika, hayo mengine ni kuhamisha tatizo kutoka ubongo wa kulia na kulipeleka ubongo wa kushoto.
 
Nadhani Kuna hoja katika kupenyeza elimu ya ufundi shuleni. Lakini pia kufanya elimu ya msingi iishie sekondari ni kuwatesa walimu wa sekondari Bure. Maana watawajazia wanafunzi wasiona vigezo. Idadi kubwa ya wanafunzi nichanzo Cha kufeli. Mtaala wa amali uanzie msingi. Pia Sanaa irasimiswe, watu wajiajiri.
 
Back
Top Bottom