Hii nguvu si mchezo: Kitenge, Zembwela na Hando wapewa escort ya ving'ora Dubai

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
5,950
23,265
photo_2023-06-23_09-24-58.jpg


Nani amefatilia Wasafi media leo asubuhi? Hawa watangazaji watatu tangu juzi wapo Dubai na wanajinasibu Kama ni wageni rasmi wa DP world kutoka Tanzania. Na wanapata escort ya ving'ora Kama wageni wa heshima.

Leo walikuwa wanawahoji watanzania ambao wanafanya kazi hapo bandari ya Dubai. Kiuhalisia wote waliohojiwa ni kutoka kwa ndugu zetu unguja na pemba (Zanzibar).

Mambo mengi mazuri Sana ya DP world yameongelewa,ikiwa pamoja na bandari kupokea meli 30 kwa wakati mmoja na kuhudumia meli sita zenye magari 3k kwa siku mbili tu. Mambo ni mengi.

Lakini Hawa jamaa ni wanajizima data au hawajui kilio Cha wanaowapinga hao DP world kuwa siyo ufanisi wao Bali ni MKATABA mbovu na wa kinyonyaji na wakivhief Mangungo baina yao na Tanzania?

Hata dada yetu wa Jf bi Faiza Fox nae aliandikw uzi wenye mtazamo huu huu wa kina Zembwela kuwa "DP world wapo hadi Uingereza iweje nyie walala hoi watanganyika mnawakataa". Akapigwa maswali haya haya,umeuona mkataba wa Uingereza? Au mkataba wa Uingereza na huu wa kwetu unafanana?

Alafu kingine; hivi ni nani amawafadhili Hawa jamaa watatu? Huko Dubai? Maana wanajimwayamwaya kama wafalme. Na Wana ego balaa,full kujisifu.

Hii nguvu ya DP world kwenye media za bongo siyo mchezo.

Lakini Hawajui kuwa ukimsisitiza Sana Mtu kuwa kitu chako ni ni kizuri ndivyo unavyomfanya astuke kwamba kwa nini jamaa ananilazimisha Sana nione hiki kitu chake kipo sawa? Jamaa wanafosi mpaka kila mtu Sasa anajua kwamba wanalazimisha!!

Hii tabia tunayo Sana sisi mawinga/ wazee wa kulenga hapa kariakoo. Nikiona hiki kiatu ni 'mdosho',nguvu ninayotumia kukuaminisha kwamba ni kiatu genuine ili uingie mkenge siyo ya nchi hii. Ukifungua wallet tu tukamalizana napita hivi,utajijua mbele ya safari. Ukikivaa ukapiga hatua zako 20,mguu unanyanyuka,soli inabaki chini.

Nikimwangalia Gerald Hando ni Kama Mtu mwenye kujistukia tofauti na wenzie. Hawa jamaa wawili wanaupepeta mdomo si mchezo. Hawana breki.
 
Nani amefatilia Wasafi media leo asubuhi? Hawa watangazaji watatu tangu juzi wapo Dubai na wanajinasibu Kama ni o. Nikiona hiki kiatu ni 'mdosho',nguvu ninayotumia kukuaminisha kwamba ni kiatu genuine ili uingie mkenge siyo ya nchi hii. Ukifungua wallet tu tukamalizana napita hivi,utajijua mbele ya safari. Ukikivaa ukapiga hatua zako 20,mguu unanyanyuka,soli inabaki chini.

Nikimwangalia Gerald Hando ni Kama Mtu mwenye kujistukia tofauti na wenzie. Hawa jamaa wawili wanaupepeta mdomo si mchezo. Hawana breki.
Kama hayo mambo mazuri wayapeleke kwao pemba
 
Nani amefatilia Wasafi media leo asubuhi? Hawa watangazaji watatu tangu juzi wapo Dubai na wanajinasibu Kama ni
Tatizo hawajibu hoja, na raia wenye asili ya Tanganyika hawamkatai DP World, wanachokikataa ni vifungu ovu, tatanishi, visivyoeleweka na ikitokea vikarekebishwa haina shida, mwekezaji apewe kazi.
Yaani wamekomaa kuelezea ufanisi wa DP World na siyo mapungufu ya mkataba sijuwi maana yake nin.
 
Back
Top Bottom