Hii kesi unge shauri nini???

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,111
115,905
Kuna jamaa alipata kazi kwenye moja ya taasisi kubwa
serikalini.....
Akiwa hana ndugu wa godfather hapo ofisini ,mambo
mengi yalikuwa yanampita......
Vipromosheni vidogovidogo,visemina,warsha n.k..

Kama bahati akampata dada mmoja hapo ofisini ambaye
ametangulia kufanya kazi hapo miaka michache kabla yake
so wakapendana baada ya mda wakafunga ndoa..
Baada ya ndoa....mambo yakaanza kumnyookea...
Mara semina,mara kozi ndogo ,mara warsha nje ya nchi
n.k n.k
miaka michache ikapita jamaa akapanda ngazi kadhaa
kimasilahi na kwa vyeo......
Yeye na mkewe wakajenga nyumba kadhaa,magari n.k
well....hata hivyo kulikuwa na habari kuwa
mke anamsaidia mumewe kupata hizo promoshen kwa
ku lala na mabosi mbalimbali wa taasisi hiyo.....
Haijulikani ni vipi mume hakujua kabisa au vipi but kadri
habari zinapoenea mwisho habari zikamfikia mume
na mgogoro ukaanza.....
Siku moja mume na mke wamegombana.....ugomvi unahusu
mke alikuwa anahisi mume anatoka nje....
Katika kutupiana maneno.....mwisho mke akasema...
We unafikiri bila mimi we ungefika hapo???unafikiri hizo
promosheni umezipata bure tu??
Kasheshe likaibuka na baadhi ya ndugu ilibidi
waitwe kutuliza huo ugomvi,ingawa hizo habari kuwa
mke alikuwa anagawa mambo ili mume apande zinafahamika
pia kwa baadhi ya ndugu.....
Kwa sasa mke na mume bado wapo pamoja but....
Kauli ya mke inaonekana kumchanganya mume kabisa...
Hakuna anaejua what will happen lakini
kama kawaida watu wanazidi kuzungumza na kila mtu
anazungumza lake......

Wewe ungekuwa ni ndugu wa mume ungemshauri nini???

Akina mama wengi katika mazungumzo wanaona mume
asamehe,na inaonekana kama kesi za aina zipo nyingi sana.
But kwa wanaume naona wanamlaumu mwanamke...

Wewe unaonaje?????????
 
Huu ni uchuro! Nashauri wakae kama kamati na kuliangalia hili kwa kina, wakianza kuhusisha ndugu na marafiki suala litakuwa kubwa kuliko lilivyo sasa.

Kuna factors nyingi za kuangalia, wakati mwingine ni vyema ku stomach mambo ya namna hii na kujipa muda ili uliangalie ukiwa na clear mind.

 
Huu ni uchuro! Nashauri wakae kama kamati na kuliangalia hili kwa kina, wakianza kuhusisha ndugu na marafiki suala litakuwa kubwa kuliko lilivyo sasa.

Kuna factors nyingi za kuangalia, wakati mwingine ni vyema ku stomach mambo ya namna hii na kujipa muda ili uliangalie ukiwa na clear mind.


mi naona kesi hii ni nzito,,,
kilichonishangaza ni kuwa watu wengi wanasema.
kuwa wanawake wengi serikalini na kwenye mashirika ndo zao..
yaani kuna watu hawajashtuka kabisa na kesi hii
 
kumega au kumegwa nje ya ndoa huwa tunaona ni tamu sana, lkn inapofikia hatua kama hii.... ni ngumu
 
Kunamambo ambayo hayahitaji kushirikisha majaji wengi namna hii,umegundua mkeo anamegwa nae kaweka vimaneno vya kudhibisha hayo unasubiri nini kummwaga ? bora kuishi peke yake (heshima itakuwepo) kulio ndoa ya aina hiyo (hakuna heshima).
 
kunamambo ambayo hayahitaji kushirikisha majaji wengi namna hii,umegundua mkeo anamegwa nae kaweka vimaneno vya kudhibisha hayo unasubiri nini kummwaga ? Bora kuishi peke yake (heshima itakuwepo) kulio ndoa ya aina hiyo (hakuna heshima).

unammwaga na kumsusia kila kitu???
Kumbuka kamegwa ili wewe ufanikiwe
so mnagawana vipi hizo mali?
Mimi naona bora na mali umuachie.
We unaonaje?
 
kwa hapa nakosa ushauri wa kuwapa cause kama ni kweli wanafanya haya mambo yatapelekea ndoa yao kuvunjika very soon cause migogoro imeshaanza kujitokeza
la kama jamaa anamega nje aache na mama kama alikuwa anamegwa nje aachane kabisa na tabia hiyo na amwangalie mmewe pekee
swali:
haka ka mama kama kalikuwa kanamegwa nje kwa nini kanamuonea gele mmewe kumega nje??
 
Huu sasa mtihani lkn simple kamegwa kwa maendeleo yenu! so msamehe ukizingatia huku mkuta hajaguswa hivyo ni vema mkaonyana na kuendeleza maisha,ukizingatia hakuwa na nia mbaya alikuwa na lengo na limetimia ktk swala kama hili achana na ndugu malizaneni wenyewe
 
atafute mademu wa mabosi amege,
ahame kazi
aache huyo mke
akapime ukimwi
asirudie tena kugombana na mkewe
 
-wajifunze kutokana na makosa yao ili wasirejee tena.
-kama wana ujasiri wa kuachana basi nibora wakaachana, madhali mambo yashamwagika hadharani ,hiyo ndoa haitokuwa na raha na heshima mbele za majamaa na marafiki, kwa lugha nyengine itakosa baraka za kupendezesha katika jamii ambayo itapelekea mateso ya kiakili kwa wanandoa hao.
-kama huyo mume anajali heshima yake zaidi kuliko mali basi ni bora hiyo mali akamuachia huyo mwanamke.
kama ushauri wangu mbaya tia kwenye taka

quiet
 
hapo hakuna ndoa wala upendo, ndoa wala upendo hausimamishwi kwa misingi ya mali, wazee walisema TAMAA MBELE MAUTI NYUMA, sasa huyo dada alikuwa anataka makuu kwa familia yake na hivyo aliona mchango wake mkubwa katika maendeleo yao ni KUMEGWA
 
We unafikiri bila mimi we ungefika hapo???unafikiri hizo promosheni umezipata bure tu???

Hii kauli ndo tata lakini tusijump kwenye conlusion hapa kuwa ni lazima huyu mama atakuwa anagawa tunda kwa 'wazee'. Hatujui position ya mwanamke kazini- labda yupo juu zaidi ya mwanaume na ana uwezo wa kuongea na 'mabosi wenzie' kumuwekea mambo sawa mumewe au ana pesa na uwezo wa kumuhongea mwenzie au alishawafanyia favour (sio lazima mchezo) wahusika hapo kazini na sasa wanalipa fadhila tu, anything is possible!
 
unammwaga na kumsusia kila kitu???
Kumbuka kamegwa ili wewe ufanikiwe
so mnagawana vipi hizo mali?
Mimi naona bora na mali umuachie.
We unaonaje?[/QUOTE]

Jamani mambo ya ndoa ni vyema tuwaachie wenyewe mara nyingi ushauri wa nje hauna nafasi katika mapenzi
na pia unasababisha chuki wakati wao watakapolimaliza si unajua ugomvi wa kwenye ndoa wanaumaliza Chumbani???? Tusiwaingilie!!!!!!!
 
Nina uhakika hakuna mwanamke anae tembea nje ya ndoa yake bila sababu kama vile wanaume tufanyavyo. Wanawake wana feelings, wanawake wanahitaji kutunzwa na kubembelezwa, pia wanahitaji kujiendeleza katika maisha yao, mwanamke huwa anahitaji pia kupendwa. Tumezoea tabia za kufanya ndoa kama kifungo kwa wanawake.

Wapo watu wenye ndoa zao kuwatimizia wake zao haki ya ndoa inakuwa kasheshe mpaka mwanamke abembeleze tena labda baada ya wk au mwezi , wanaume wengine hata kuacha hela za matumizi nyumbani inakuwa shida. we unategemea kwa vile umeoa basi mwanamke huyo umfanyie ujinga na vituko vya jinsi hiyo kila siku.
Inafika mahali mwanamke na yeye anafanya maamuzi yake kutokana na mahitaji yake.

Kama unamke na humridhishi wataka ajitie vidole wakati vijana wa kufanya shughuli hiyo wapo ? Una mke na watoto hela za matumizi huachi wakati wanaume wenye kujua kuhudumia wapo ?
Kesi hiyo wataimaliza wenyewe bila shida.

 
Hujafafanua kama wana watoto au lah ndo hapo tuanze kutoa ushauri.
 
Back
Top Bottom