Mimi ni mwanafunzi wa Chuo cha Mipango Dodoma main campus nasoma mwaka wa tatu degree ni mnufaika wa Bodi ya Mikopo, tangu mwaka wa kwanza nimekumbana na changamoto ya kutowekewa allocation na sio mimi tu, tupo wengi sana na mpaka dakika hii hatujapata boom ni wiki ya tatu hii tangu tufungue chuo na sisi ni watoto wa walala hoi tunaishi kwa boom.
Wengi wetu tunategemea hizo fedha tulipe Kodi, bima na hata ada kwa ambao hatuna 100%. Wenye nyumba wanatudai kodi, kula yetu ya shida kiukweli inaumiza sana.
Wana JF, ushauri wenu tafadhali. Na kama kuna kiongozi anahusika na suala hili kiukweli huku Chuo cha Mipango hali ni mbaya; kisaikolojia imetuathiri sana wanafunzi kiasi kwamba hata usomaji umekua mgumu kutokana na ugumu wa maisha.
Hatuelewi allocation tutawekewa au hatuwekewi kabisa tusimamishe masomo maana uwezo wa kujilipia ada kwa kushitukiza hivi hatuna. Tunaomba bodi kama imeamua kutufutia allocation iseme tu sio kutoa majibu ya kusubiri wakati utekelezaji hakuna. Bungeni linazungumziwa suala la First Year kutopata mkopo lakini hawajui kama kuna shida ata kwa sisi mwaka wa tatu kutopata fedha zetu za kujikimu na allocation kabisa hazisomi.
Hii inaumiza sana. MAMA SAMIA Rais wetu usikie kilio chetu, tunaenda wapi sisi?