HESLB.. Bodi ya Mikopo una Virus

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
Katika Kipindi hiki cha Wanafunzi wa elimu ya juu wakijiandaa na masomo yao na kutegemea mikopo bodi ya mikopo, Ila cha Kushangaza ni kwamba Website ya bodi ya Mikopo imevamiwa na Virus, Tunaomba msaada wa watu wahusika na IT wote wa bodi ya mikopo, tunaomba ushirikiano wenu.
 
Kama Idd simba alivyosema juzi - watanzania tumedumaa/tumedumazwa kiakili! Je ni kweli?
JK kashindwa, na hili liko wazi na shahidi ni yeye mwenyewe alipoikana ilani iliyomuweka madarakani - live wote tukiona na kusikia. Sasa anakuja mtu anasema kafanya mengi! Kama yangekuwepo mengi asingeikana ilani yake!
Hoja kwamba tumgemchagua nani mwaka 2005 - jibu ni rahisi - wote walioruhusiwa kugombea urais walikuwa na uwezo wa kuwa marais, Hivyo kwa kuwa mlimchagua JK sasa amevurunda basi kumbe kati ya wale waliobaki mmojawapo angekuwa rais.

Watanzania tunajidumaza kiakili kufikiria eti rais lazima atoke CCM! CCM imekuwa kichaka cha kila aina ya ufisadi, mimi ningekuwa mwanaccm ningekuwa najificha nikisikia mtu anataja CCM ili nisije nikaitwa fisadi.

WaTZ tunaacha kuwachagua watu toka kambi ya upinzani kwa hisia tu - eti hawatafanya vizuri. OK mtasema Mbowe hana rekodi mnayoijua - je Mrema? Mtu aliyepata kushika uwaziri na unaibu waziri mkuu! hamumjui? Si mnajua mafisadi wangepewa siku saba kurudisha pesa zetu; si mrema alianza kunusa ufisadi wa akina patel katika kashfa ya mashamba ya mkonge?

Wengine wanasema eti tukiwachagua wapinzani nao wataenda kula tu! Huo ni udumavu wa akili - kwa nini wawahukumu kwa hisia zako tu? OK hata kama wataenda nao kula, je nchi imeumbwa iliwe na CCM tu?

La msingi, na ndiyo uzuri wa demokrasia halisi, unamchagua mtu akivurunda unamtoa unamuweka mwingine, akivurunda naye unamtoa unamuweka mwingine, naye akivurunda labda yule wa kwanza atakuwa amepata fundisho - unamrudisha, akivurunda tena unamuacha..... and so on .....!
WaTZ tunag'ang'ania CCM tuuuuuuuu ingawa tunakiri inafanya vibaya! UDUMAVU WA AKILI HUO

mh! sasa hii inaingiliana vp na mtandao wa HESLB kuwa na virus?!!!.......mode, tafadhalini tunaomba mngeimuvuzisha hii kwenda siasa
 
mh! sasa hii inaingiliana vp na mtandao wa HESLB kuwa na virus?!!!.......mode, tafadhalini tunaomba mngeimuvuzisha hii kwenda siasa
kosa limerekebishwa; ilikusudiwa kuwa kwenye thread ya tulikosea kumchagua JK.....
Pole kwa usumbufu
 
Hasa kwa tunaotumia avast antivirus inakupa warning kali na unalazimika kufunga website
malware name: HTML.Ilframe.C(trj)
malware type: Trojan horse.
Webmaster ebu rekebisha kosa hilo haraka sana!
 
wakuu kama kuna mtu mwenye uelewa juu ya mikopo inavyotolewa anijuze kidogo hasa kwenye kipengele cha TOTALWTPERCENT
 
Naona kitu kipo hosted udsm, taabu kweli kweli!
JojiPoji weka hicho kipengele chote watu wakusaidie.
 
Mimi na wewe hatujui kabisa maana naona kuna 100A, 10A 30A C D and alama nyingine sasa hatujui kabisa
 
Michael vipi wewe umepata hiyo website? mimi tokea jana nahangaika sipati Adobe inakataa kufunguka. Kama kuna mwenye msaada tueleweshane.
 
Back
Top Bottom