Heko RC Said Mtanda. Chama kilikulea, Ukaleleka. Kero za wananchi hazipaswi kusubiri Vikao vya Kamati!

Mpekuzi Tanzania

JF-Expert Member
Mar 11, 2018
590
911
Tanzania inahitaji Viongozi wenye upeo wa aina ya Said Mtanda. Tukiendelea na biashara ya kusubiri vikao kutatua kero za Wananchi kwa visingizio vya demokrasia wanayotaka kina Kagasheki (Wazee ambao muda wa kuishi umewatupa mkono) kama Taifa tutasubiri sana.


"Jana tulifanya mkutano hapa Tarime, katika ule mkutano mlisikia kuna watu walitoa malalamiko kwamba wana pikipiki zao zimekamatwa na wanahisi ni makosa madogo madogo hapa Silali, na kiongozi akasema fuatilia kama ni makosa madogo madogo basi wasaidie, kama ni makosa makubwa makubwa ambayo yanahusiana na sheria basi pia fuatilia tujue.

"Kabla ya kuingia kwenye uchaguzi ni lazima vyama vya siasa vijiandikishe, viteue mgombea, halafu vipeleke mgombea apitishwe, chama kizunguke kiombe kura, mgombea wa chama akishinda ataunda serikali kwahiyo serikali hii inatokana na Chama Cha Mapinduzi kuomba ridhaa ya wanachi kushika dola.

"Ridhaa imetolewa, hivyo wanao wajibu na haki ya kuwasikiliza wananchi. Wanachi wakisikilizwa wanatoa maagizo kwetu, kwamba wewe tumekuajiri kwenye serikali yetu kama Mkuu wa Mkoa, wananchi wanalalamika kwamba wana pikipiki zao huko Silali, nakuelekeza Mkuu wa Mkoa fuatilia, chukua hatua, wasaidie kama inalazimika kusaidiwa. Sasa wengine wanasema kwanini iwe hivyo?

"Kuna aina mbili ya kutoa maelekezo, aina ya kwanza ni kupitia vikao halali vya chama, hata pale mkoani huwa ninaagizwa kupitia Halmashauri Kuu ya Mkoa au Kamati ya Siasa ya Mkoa kwamba kikao kimekaa tunakuagiza Mkuu wa Mkoa ushughulikie suala la Silali, tumesikia wananchi wetu wana malalamiko ya maji tena naandikiwa kwa barua, kikao cha tarehe fulani kimekaa. Ninasikiliza na kutekeleza.

"Aina ya pili, tunaposema chama ni viongozi wa chama na wanachama, viongozi wanaweza kuja katika maeneo kama haya kufanya ziara, aidha Katibu Mkuu, Mwenyekiti, au Makamu Mwenyekiti wa chama akakutana na kundi la wananchi wanalalamika juu ya suala hilo la pikipiki. Kama kiongozi wa chama amekwenda kwenye mkutano, je ni akili ya kawaida mpaka arudi Dodoma kikao cha Kamati Kuu au Halmashauri Kuu kikae kimuagize kwenda kushughulikia suala hilo Silali?

"Yeye kwakuwa ni muwakilishi wa chama amesikiliza kero na serikali hii imeundwa na chama anayo haki ya kutoa maagizo, maelekezo, ushauri, maoni, kwa viongozi wa serikali wa eneo hilo wamalize kero hiyo.

"Mwenezi amekuja hapa kuimarisha chama, anakuja Tarime kakuta watu wana bango CSR, hivi arudi mpaka Makao Makuu ya Chama mpaka wakafanye kikao ndio atoe maagizo kwamba tuwasikilze, inaingia akilini?

"Yako mambo makubwa ya vikao, yako mambo mengine kwa nafasi yake kama kiongozi wa chama akiyakuta anatuelekeza. Kwahiyo baada ya kunielekeza pale jana, leo si nimekuja kufanya kazi na nyie?" -
RC Said Mtanda
 
Back
Top Bottom