Elections 2010 Hebu ona huu upuuzi

Hakli Elimu wako wapi? Au nao wameshanunuliwa baada ya kuondoka Rakesh Roshan? Namuomba Dr Slaa asisahau kulizungumza hili kwa kirefu akiwa Mwanza.

Lakini kwa upande mweingine, bila kufanya hivi mikutano ya CCM miaka hii huwa haina mvuto, haina wahudhuriaji. Kuna thread humu ndani inasema CCM ililipa wananch waliohudhuria mkutano wa kampeni kule Jangwani jijini Dar.
 
Inasikitisha sana kwa chama kama CCM kufanya mambo ya ajabu. Inasikitisha sana kuona walimu wameruhusu wanafunzi wajihusishe na mambo haya ya ajabu wengi wao pale hawana hata vigezo vya kupiga kura. wengine pale ni wa chekechea, yote hiyo ni kujaza mtu kiwanjani. Huu sio uungwana wa kisiasa.

Halafu nimemshangaa sana huyu Flora mbasha. Hivi hajui kuwa kuna mipaka kati ya mambo ya siasa na Kanisa? Baada ya kupata umaarufu Kanisani sasa anahamishia njaa yake kwenye majukwaa ya kisiasa? Hivi CUF wakimualika kwenye kampeni zao atakwenda? Ndio maana nasema wakati wote kuwa hawa waimbaji binafsi (si wote) wengi wao wapo kwa ajili yakujipatia kipato sio vinginevyo.

Mfano ndio huo huyo Frola kampeni zikiisha utasikia anasema anazindua nyimbo za pasaka, hao ni wajasilia mali tu hamna kiroho wala nini? Njaa hizo zinazofanywa na wakina flora zinadhalilisha kanisa!!!!!

:A S-danger:
 
Vipi hao waendesha piki piki ambao hawajavaa helmet mbele ya trafiki, sheria ya usalama barabarani inasemaje kuhusu hili? Au kwenye kampeni ruksa kuvunja sheria???
 
Naona CCM imeamua kukiuka taratibu za kampeni kwa kuwatoa wanafunzi madarasani ili waende kuipigia kampeni.....
Nasikia kuna baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao bado hawajapata mikopo yao hadi hivi leo. Lakini unashangaa unapoona kuna mabango ya shirikisho la vyuo vikuu hapo likiunga mkono upuuzi huu.
uwepo wa wanafunzi ccm wanakula timing mkuu. Nadhani hawakutarajia uwepo wa watu wengi hivyo wanafunzi huongeza idadi. Kama upo makini hata alipokuwa songea kuzindua mnara wa mashujaa wa vita ya majimaji wanafunzi ndio walifunika!

Kuhusu TAHILISO no wonder mwenyekiti/rais wa taasisi hiyo ni kibaka mmoja kutoka ushirika nadhani ni miongoni mwa viongozi wa uvccm moshi! Jamaa nikibaka hafai hata bure ila ni mmbabaishaji mzuri!
 
tuwasamehe - wengi wao hawajui walitendalo, maskini hata hao wanaojiita wenye upeo na wasomi wa vyuo vikuu, its so sad.

wengi wa hawa watu wanaishi chini ya dola moja kwa siku maskini, ni kazi kubwa sana kukiokoa kizazi hiki lakini hakuna kukata tamaa tunao tu sambamba hatuwezi kuwaacha kondoo wakiangamia mikononi kwa mafisadi wafirisi wa mali asali.

Mbasha anajidhalilisha na nafikiri wa hili anajimaliza mwenyewe - njaa hizi wakuu ni mbaya sana.
 
This is more than desperation, huyu JK na wapambe wake mimi huwa nashindwa kuwaelewa kabisa kuna ile notion kwamba anapendwa na wananchi, ana nyota ya kupendwa (F.c.k if such a thing exist), ni kipenzi cha vijana, amefanya mambo makubwa, hana mpinzani etc. etc. etc.

But why these people are always desperately trying to buy affection?
 
Sasa wale adui wameshikamana vyema ujinga, maradhi (hasa ya akili), umasikini na CCM wakibomoa nchi...kazi ipo
 
Ni njaa yake, kwani kwa hadhi yake alitakiwa kuliimbia taifa na si CCM na wanachama wake. Hao watoto wa shule wanatumiwa vibaya, kwanza wote ni wa kike halafu wakifeli wanataka waingie chuo kikuu kwa favour. Je, wote wamefika hapo au wengine wamekwama sehemu na pia je wote watarudi bila kupewa soseji na meat balls mbili!?

halafu wakipata mimba wataambiwa ni kihehere chao
 
Inasikitisha sana kuona CCM inavyowatumia hawa wanafunzi vibaya - kwanza wengi wao hawajafikisha hata umri wa kupiga kura !!!! Hili swala ni la kupinga kabisa hao, na imekua kama sheria hivi kwenye hizi shule na mwanafunzi usipoenda ni adhabu inafwata..

I don't know!! If we don't act now, I thinks it'll take ages for changes !!
 


sishangai sana kuona upuuzi wote huu coz maneno yake na vitendo vinajidhirisha kuwa hawajali kabisa wanafunzi especially wa kike. nakumbuka alisema KUPATA MIMBA KWA WANAFUNZI NI KIHEREHERE CHAO na hapa anaonyesha vile ambavyo hawajali kwa kuwaruhusu kuhudhuria kampeni muda ambao walitakiwa kuwa mashuleni mbona wakiume hawapo.

dada mbasha pole kwa kuchanganya siasa na dini yatakushinda kama hautajirekebisha mapema. pesa hizo ni za muda tu lakini ni wangapi utakuwa umewapotosha kwa onyesho lako na nina imani sio ilo tu mengine yanafuata

:welcome:


MUNGU IBARIKI TANZANIA​
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,

Wazee wa mashati ya kijani wameishiwa, hawana mapya, ndo maana kujihami wamwekimbilia kuwaleta wanafunzi katika kampeni za uchaguzi. Wanafunzi ambao hata maana ya uchaguzi hawajaijua, wanafunzi ambao sifa ya raia hawaijui, hii ndo CCM, kujaza mapengo kuuonyesha umma wa ndani na nje kuwa wanakubalika. Ili kazi ya KUCHAKACHUA kura isiwe ngumu na ikose upinzani!!!

CCM imelaaniwa kwa maovu na machafu yote waliyotufanyia kwa miaka takribani 50 toka uhuru!! Yanawarudia ndo maana hawawezi kubadili watu otherwise...
Nasema kuchakachua kura ni dhambi yao, lakini tukikataa kuwapa ridhaa hata uchakachuzi utashindikana, maana nina uhakika watachanganya madesa!!! Dawa ni kuhamasisha wooooooooooote ndani ya kaya zetu, tukapige kura kwa kuleta mabadiliko; hawa tumewazoea...

Ukianzia ndani mwako changes will certainly come to TZ!!
 
Mjomba sasa hawa ccm naona wamenunua killa ki2 halafu wanatudanganya eti Tz kuna mfumo wa vyama vingi. Sasa hivyo vyama vingi ni vya kushindani urais na kukosa tu!
Hao ccm kama ndo kukuza kwenyewe elimu ya watanzania masikini kwa kuwapeleka watoto wao wadogo wakaishangilie ccm kwenye jua kali huku wakiwa na njaa wana tofauti gani ana akina Carl Peters wa wajerumani??
Hawa dawa yao ni kuwanyima hatamu tu tuwape wapinzani nao tuwaangalie mambo yao yatakuwaje.Inauma sana kuwapeleka vitoto vidogo kuumia njaa na jua kali eti ili kujaza uwanja uonekane una mashabiki, si wangewapa hata na maji ya kunywa basi au na chakula ili tuone kweli ccm wana upendo wa kweli! Kwa hiyo tuseme hizo shule nyingi zilizojengwa na MMEM ni kwa ajili ya kupatia wafuasi wa ccm kwa kulazimishwa?!!
Na hao walimu ndo walisoma kitu gani huko vyuoni mwao....?Hata kutetea wanafunzi wao hawawezi au ndo nao pia ni makada wa ccm ili wapate kwenda kusimamia uchaguzi.

WASHINDWE NA WALEGEE!!!
 
Asante sana. Nimejua kwa nini hadhara zake zinakuwa kubwa, ni kivutio kwa watu kuona kazi za sanaa! Ni usanii kumbe! Taifa langu umekosa nini hata uwaruhusu watu wakuchezea kiasi hiki! Masomo yanakatizwa kwenda kwenye halaiki ya kampeni za uchaguzi!! Tulitegemea wasomi wa Vyuo Vikuu kuwa kioo cha jamii, lakini unapokwenda kucheza ngoma ili uonekane ni shabiki wa kiongozi, tunalipeleka wapi taifa hili!!!!

Wanafunzi wangu(vyuo vikuu) mmekosa nini hata mkakubali kufanyiwa dhihaka kiasi hicho! Ole wenu
 
Ujinga mtupu. Tangu lini watoto wetu under 18 wanashirikishwa mikutano ya hadhara ya siasa???!! Badala ya kuwasisitiza wasome ni kuwapotezea muda wa masomo ili hali hawapigi kura. Eti wanajidai watawatumia kufikisha ujumbe kuwa awamu ya nne imefanya hili na lile la maendeleo!! Kuna mikopo ya elimu ya juu ambayo mzazi/mlezi wako anatakiwa kuchangia, halafu hakuna hostel za kutosha utalala mitaani na utachangia umeme na maji bado hujakamata daladala la kukufikisha chuo ukiwa na jasho tiiiii, toooo!! Oh, danganyikeni!! Mwongo huyo!! Kweli Tanzania ni zaidi ya ujuavyo!!
 
Nimefarijika sana kuona mkakati wa serikali ya CCM kujenga sekondari za kata,haya tunayoyaona ndio matunda yake,jamani walimu hakuna mashuleni ndio maana hawa kichefuchefu waliweza kwenda kwenye mkutano maana hawakuwa na cha kufanya plus ujinga uliomo kichwani ndio kabisa.
 
Nyie wenyewe mnajua jinsi gani wanafunzi wa shule wasivyo na maamuzi kwenye mambo kama hayo. Mwalimu akishawaambia kuwa leo mtaenda kwenye kampeni za CCM hawana uwezo wa kubisha. By the way, wamezolewa kwenda kujaza watu uwanjani ila nasikitika kuwa wamekosa masomo kwa suala mabalo wala haliwahusu kwa sasa. Kila kitu kwa wakati wake..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom